Samahani ndugu naweza kupata namba zako?.Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
Thanks wadau wote.
Mrejesho:
Thanks kwa wote:
- Kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
- Kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki (July 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
- Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
- Mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
- Mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
- Watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
- Expectations zangu mwaka huu ni 35 (eka) x 400 (kg) x 2500 (bei/kg) =35,000,000.
- NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).
UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA UINGIE UCHEZE
Samahani ndugu naweza kupata namba zako?.
Nawezaje kupata connection ya kumuuzia mo.WELL. Ufuta ni biashara nzuri sana hapa tz. mnunuzi mkubwa wa hapa ndani ni Mohamed Enterprises hapa DSM.
Ekari moja inakupa gunia 8@85-90 kgs so ni kama kilo 680 kwa ekari moja.
Nami nitafuatilia suala hili na mwakani ninampango wa kuanza na ekari 10 kwa mkoa wa lindi. kuhusu mbegu na wadudu nakushauri uende vyuo vya kilimo vilivyopo maeneo ambayo kilimo cha ufuta kinafanyika. kwa mimi nitaenda naliendele agricultural institute cha mtwara nadhani wananisaidia. Kila la heri.
Duh mwamba unaijua mpaka nakiu nimetoka juzi hapo saivi nipo nachingwea kwenye mbaaziWapi hiyo Mkuu..? Baadhi Ya maeneo katika wilaya Ya Kilwa Kama NAKIU wameanza kuukata...kwa ajili Ya kuupanga katika mianzi
Liwale maeneo gani mkuuNimekuwepo lindi- Liwale huko wanapata debe 24- 36 kwa heka pia huku songwe maeneo ya mkwajuni napo kipato kipo hivyo pia ukienda maeneo ya bonde la ziwa rukwa napo wengi huwa kipato kina range kwenye debe 18-36
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ishu ya soko ipo hivi;
1. Kuna wanunuzi hasa wahindi huja mashambani wakati wa mavuno (Lindi and Mtwara are my case study)
2. Unaweza funga mzigo wako ukauleta dsm kwa mohamed entreprises ni mnunuzi mkubwa na ukisafirisha utapata faida zaidi
3. Waweza tafuta mzigo mkubwa wa kutosha kontena kuanzia 3, 4, nk na ukauza nje ya nchi na nchi inayonunua sana ni india.
mimi nilikuwa na mpango wa kulima next yr but ntaanza na mazoa jamii ya choroko na mbaazi. hivi naandaa shamba.
msimu unaenda huu, vp ushapata wadau?! au kampeni zimekuwa ngumu maana yataka moyo..changamoto hazikosi ndugu😁😁Wale tunaolima Ufuta Mwaka huu tutafutane
Nakuja pmWale tunaolima Ufuta Mwaka huu tutafutane
Habari yako mkuuNiko mkoa wa Katavi,Wilaya ya Mpanda,kijiji cha Stalike...Nimelima heka 30...Namalizia kuvuna
Sent using Jamii Forums mobile app