Moja ya kilio kikubwa mashambani ni mavuno, pamoja na nguvu nyingi zilizowekezwa na watanzania wengi lakini mavuno yameendelea kuwa hafifu ama kukosekana kabisa.
Yote hii inasababishwa na matumizi ya njia duni za kilimo pamoja na kukosekana kwa ardhi yenye rutuba. Sehemu kubwa ya ardhi hiyo imekosa virutubisho muhimu ambavyo vyenye msaada mkubwa katika ukuaji wa mimea.
Virutubisho vya madini ya udongo ni elementi muhimu zilizomo kwenye udongo ambazo huchangia katika uzazi na ukuaji wa mimea.
Elementi hizo ni pamoja na salfa, sodiamu, klorini, naitrojeni, fosforasi, potasiamu, oksijeni, hidrojeni na kaboni. Mimea hutegemea virutubisho hivyo katika kila hatua ya ukuaji na kila elementi ya virutubisho hivyo huwa na matumizi ya kipekee kwa mmea kwenye ukuaji wake.
Kwa maana nyingine kukosekana kwa moja ya elementi kwenye udongo ambao umebeba mmea moja kwa moja huathiri shughuli za kifiziolojia kwa mmea. Tunaweza kuitazama naitrojeni ambayo ni elementi muhimu katika uundaji wa protini, homoni pamoja na vitamini.
Naitrojeni pia huchangia katika udhibiti wa upatikanaji wa madini ya potasiamu na fosforasi kwenye mmea. Kukosekana kwa naitrojeni hufifisha uwezo wa mmea kujitengenezea chakula sambamba na kupelekea ukuaji wenye kudumaa.
Udongo unaweza kupoteza rutuba yake endapo kutakosekana usahihi katika usimamizi na utunzaji, kwa maana kwamba ni rahisi rutuba kutoweka kwenye udongo iwapo hakutakuwepo na matumizi sahihi ya udongo huo. Udongo unaweza kupoteza rutuba kupitia mmonyoko wa udongo, Leaching, mkusanyiko wa chumvi pamoja na njia duni kipindi cha kilimo na msimu wa mavuno.
Mmomonyoko wa udongo unahusisha uondoaji wa udongo wa juu wenye rutuba kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia upepo,maji ama wanyama.
Mmomonyoko huo unaweza kusababishwa na matumizi ya kilimo cha zao moja, ufugaji kupita kiasi pamoja na uchomaji holela wa mazalia ya mimea.
Kilimo cha zao la aina moja kimekuwa kilimo mama kwa wakulima wengi. Kilimo hiki kikifanyika kwa muda mrefu kwenye ardhi/eneo moja huweza kusababisha kupungua baadhi ya virutubisho ambapo huupelekea udongo kupoteza rutuba yake.
Kwa upande mwingine ufugaji wa kupita kiasi umekua ni utamaduni kwa wafugaji, ufugaji huu huhusisha utunzaji wa idadi kubwa ya mifugo kwenye eneo dogo ambayo hufanya mijongeo yenye kujirudia katika eneo hilo na kusababisha ardhi kushindwa kulinda udongo wake.
Hali hii hupelekea mmomonyoko wa udongo ambao huambatana na upotevu wa rutuba kwenye udongo huo. Ufugaji huu pia husababisha kuharibika kwa umbile la udongo na kuushawishi kumomonyoka kwa urahisi. Mmomonyoko wa udongo pia huweza kutokea kipindi cha mvua kali(mafuriko) ama panapokuwa na umwagiliaji mkubwa kupitia mchakato wa upenyeshaji maji kwenye udongo ufahamikao kama leaching. Kwa kupitia leaching maji hupenya kwenye tabaka la juu la udongo ambapo huchanganyika na kuviyeyusha virutubisho vilivyomo kwenye tabaka hilo. Mchanganyiko huo hupenya kwenye tabaka la chini zaidi na kuliacha tabaka la juu bila ya rutuba.
Kama tunavyoweza kuona ni kwa namna gani mmomonyoko wa udongo, leaching na baadhi ya njia za kilimo zinavyopelekea upotevu wa rutuba kwenye udongo. Kwa lengo la kuwa na mavuno yenye kuridhisha kuna mambo kadhaa yanahitajika kufanyika ili kuhakikisha kuwa udongo haupotezi rutuba. Utunzaji, usimamizi pamoja na matumizi bora ya ardhi katika shughuli za kilimo ni miongoni mwa mambo yatakayotuhakikishia uwepo wa ardhi ya rutuba.Kulingana na visababishi vya upotevu wa virutubisho katika eneo husika tunaweza kunusuru upotevu wa virutubisho vya madini ya udongo kwa kupitia mbinu mbalimbali. Mbinu hizo ni pamoja na kuzuia kutokea kwa mmomonyoko wa udongo, kutandaza majani(mulching), kilimo cha mzunguko wa mazao, kilimo cha mazao mseto, nyongeza ya mbolea/samadi na matumizi ya njia bora wakati wa kilimo na baada ya mavuno.
Ni matumaini yangu kuwa tumeweza kufahamu ni kwa namna gani mmomonyoko wa udongo unaweza kupelekea shida ya kutoweka kwa ardhi yenye rutuba. Kilimo cha matuta, malisho yaliyodhibitiwa na kilimo mseto ni miongoni mwa njia ambazo zinaweza kuzuia tatizo la mmomonyoko wa udongo.
Malisho yaliyodhibitiwa ni mchakato wa kuweka idadi sahihi ya mifugo katika ardhi ya malisho. Ikitokea ardhi ya malisho ikawa kubwa, malisho ya mzunguko yanaweza kutumika kwa kuruhusu ukuaji wa nyasi safi juu ya ardhi iliyochoka kutokana na malisho hayo.
Kwa upande mwingine kilimo cha matuta huzuia uelekeo wa maji kwenye mteremko na kuyalazimisha maji hayo kupenya zaidi kwenye udongo hivyo kuweka udongo huru kutokana na mmomonyoko ambao ungesababishwa na maji yenye kutiririka.
Kilimo cha kuzungusha mazao ni aina ya kilimo kinachohusisha ustawishaji wa aina tofauti ya mazao kwenye ardi ileile kwa misimu tofauti katika wakati maalum. Mazao jamii ya kunde yanapaswa kujumuishwa ili kuboresha kiwango cha naitrojeni kwenye udongo. Iwapo eneo hilo litakuwa ni kubwa, tunashauriwa kuligawa katika sehemu kadhaa na kwa kila sehemu tunashauriwa kustawisha mazao tofauti tofauti kwa mzunguko.
Mathalani eneo hilo la kilimo likatokea kuwa dogo basi tunaweza hakikisha kuwa rutuba iliyotumika na mazao katika kila tabaka la udongo inarejeshwa kwa kupanda mazao yenye mizizi ya kina kifupi (kama vile mahindi, matango na maboga) pamoja na mazao yenye mizizi ya kina kirefu (kama vile viazi vitamu, pilipili, na tikiti maji) kwa mzunguko. Kilimo cha mchanganyiko wa mazao ni moja ya kilimo kinachoruhusu ustawishaji wa aina tofauti ya mazao kwenye shamba moja ndani msimu ama mpando huohuo, kwa mfano kwenye shamba lililopandwa mahindi tunaweza kustawisha maharage au migomba ya ndizi pamoja na magimbi. Mara nyingi magimbi au migomba ya ndizi hutoa kinga kwa kufunika uoto wa ardhini, mazao jamii ya kunde mfano wa maharage hutoa naitrojeni kwenye udongo ambayo hutumiwa na mimea mingine.
Matandazo kama vile majani makavu, nyasi na maganda ya mpunga yanaweza kutumika kufunika udongo, matandazo hayo hutumika kama sponji ambayo hufyonza maji ya mvua na upepo na kuzuia mmomonyoko. Mbali na kusaidia katika kuhifadhi unyevu wa udongo, kuzuia ukuaji wa magugu, kuongeza viumbe hai kwenye udongo na kudumisha hali ya joto ya udongo, matandazo pia huoza taratibu na kuongeza rutuba kwenye udongo.
Vinginevyo samadi/mbolea ambayo ni bidhaa ya mwisho ya taka za kikaboni inaweza kuongezwa kwenye udongo na kukabiliana na tatizo la mmomonyoko. Samadi huoza ili kutoa rutuba ya madini kwenye udongo ambayo huunganisha chembechembe za udongo pamoja, hivyo kulinda chembe hizo. Samadi pia huboresha umbile la udungo na uwezo wake wa kuhifadhi maji. Hii ina maanisha kuwa kuna umuhimu pia wa kuongeza mbolea kwenye mashamba yetu ili kuhakikisha ardhi inakuwa na rutuba ya kutosha.
Yote hii inasababishwa na matumizi ya njia duni za kilimo pamoja na kukosekana kwa ardhi yenye rutuba. Sehemu kubwa ya ardhi hiyo imekosa virutubisho muhimu ambavyo vyenye msaada mkubwa katika ukuaji wa mimea.
Virutubisho vya madini ya udongo ni elementi muhimu zilizomo kwenye udongo ambazo huchangia katika uzazi na ukuaji wa mimea.
Elementi hizo ni pamoja na salfa, sodiamu, klorini, naitrojeni, fosforasi, potasiamu, oksijeni, hidrojeni na kaboni. Mimea hutegemea virutubisho hivyo katika kila hatua ya ukuaji na kila elementi ya virutubisho hivyo huwa na matumizi ya kipekee kwa mmea kwenye ukuaji wake.
Kwa maana nyingine kukosekana kwa moja ya elementi kwenye udongo ambao umebeba mmea moja kwa moja huathiri shughuli za kifiziolojia kwa mmea. Tunaweza kuitazama naitrojeni ambayo ni elementi muhimu katika uundaji wa protini, homoni pamoja na vitamini.
Naitrojeni pia huchangia katika udhibiti wa upatikanaji wa madini ya potasiamu na fosforasi kwenye mmea. Kukosekana kwa naitrojeni hufifisha uwezo wa mmea kujitengenezea chakula sambamba na kupelekea ukuaji wenye kudumaa.
Udongo unaweza kupoteza rutuba yake endapo kutakosekana usahihi katika usimamizi na utunzaji, kwa maana kwamba ni rahisi rutuba kutoweka kwenye udongo iwapo hakutakuwepo na matumizi sahihi ya udongo huo. Udongo unaweza kupoteza rutuba kupitia mmonyoko wa udongo, Leaching, mkusanyiko wa chumvi pamoja na njia duni kipindi cha kilimo na msimu wa mavuno.
Mmomonyoko wa udongo unahusisha uondoaji wa udongo wa juu wenye rutuba kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia upepo,maji ama wanyama.
Mmomonyoko huo unaweza kusababishwa na matumizi ya kilimo cha zao moja, ufugaji kupita kiasi pamoja na uchomaji holela wa mazalia ya mimea.
Kilimo cha zao la aina moja kimekuwa kilimo mama kwa wakulima wengi. Kilimo hiki kikifanyika kwa muda mrefu kwenye ardhi/eneo moja huweza kusababisha kupungua baadhi ya virutubisho ambapo huupelekea udongo kupoteza rutuba yake.
Kwa upande mwingine ufugaji wa kupita kiasi umekua ni utamaduni kwa wafugaji, ufugaji huu huhusisha utunzaji wa idadi kubwa ya mifugo kwenye eneo dogo ambayo hufanya mijongeo yenye kujirudia katika eneo hilo na kusababisha ardhi kushindwa kulinda udongo wake.
Ni matumaini yangu kuwa tumeweza kufahamu ni kwa namna gani mmomonyoko wa udongo unaweza kupelekea shida ya kutoweka kwa ardhi yenye rutuba. Kilimo cha matuta, malisho yaliyodhibitiwa na kilimo mseto ni miongoni mwa njia ambazo zinaweza kuzuia tatizo la mmomonyoko wa udongo.
Malisho yaliyodhibitiwa ni mchakato wa kuweka idadi sahihi ya mifugo katika ardhi ya malisho. Ikitokea ardhi ya malisho ikawa kubwa, malisho ya mzunguko yanaweza kutumika kwa kuruhusu ukuaji wa nyasi safi juu ya ardhi iliyochoka kutokana na malisho hayo.
Kwa upande mwingine kilimo cha matuta huzuia uelekeo wa maji kwenye mteremko na kuyalazimisha maji hayo kupenya zaidi kwenye udongo hivyo kuweka udongo huru kutokana na mmomonyoko ambao ungesababishwa na maji yenye kutiririka.
Kilimo cha kuzungusha mazao ni aina ya kilimo kinachohusisha ustawishaji wa aina tofauti ya mazao kwenye ardi ileile kwa misimu tofauti katika wakati maalum. Mazao jamii ya kunde yanapaswa kujumuishwa ili kuboresha kiwango cha naitrojeni kwenye udongo. Iwapo eneo hilo litakuwa ni kubwa, tunashauriwa kuligawa katika sehemu kadhaa na kwa kila sehemu tunashauriwa kustawisha mazao tofauti tofauti kwa mzunguko.
Mathalani eneo hilo la kilimo likatokea kuwa dogo basi tunaweza hakikisha kuwa rutuba iliyotumika na mazao katika kila tabaka la udongo inarejeshwa kwa kupanda mazao yenye mizizi ya kina kifupi (kama vile mahindi, matango na maboga) pamoja na mazao yenye mizizi ya kina kirefu (kama vile viazi vitamu, pilipili, na tikiti maji) kwa mzunguko. Kilimo cha mchanganyiko wa mazao ni moja ya kilimo kinachoruhusu ustawishaji wa aina tofauti ya mazao kwenye shamba moja ndani msimu ama mpando huohuo, kwa mfano kwenye shamba lililopandwa mahindi tunaweza kustawisha maharage au migomba ya ndizi pamoja na magimbi. Mara nyingi magimbi au migomba ya ndizi hutoa kinga kwa kufunika uoto wa ardhini, mazao jamii ya kunde mfano wa maharage hutoa naitrojeni kwenye udongo ambayo hutumiwa na mimea mingine.
Matandazo kama vile majani makavu, nyasi na maganda ya mpunga yanaweza kutumika kufunika udongo, matandazo hayo hutumika kama sponji ambayo hufyonza maji ya mvua na upepo na kuzuia mmomonyoko. Mbali na kusaidia katika kuhifadhi unyevu wa udongo, kuzuia ukuaji wa magugu, kuongeza viumbe hai kwenye udongo na kudumisha hali ya joto ya udongo, matandazo pia huoza taratibu na kuongeza rutuba kwenye udongo.
Vinginevyo samadi/mbolea ambayo ni bidhaa ya mwisho ya taka za kikaboni inaweza kuongezwa kwenye udongo na kukabiliana na tatizo la mmomonyoko. Samadi huoza ili kutoa rutuba ya madini kwenye udongo ambayo huunganisha chembechembe za udongo pamoja, hivyo kulinda chembe hizo. Samadi pia huboresha umbile la udungo na uwezo wake wa kuhifadhi maji. Hii ina maanisha kuwa kuna umuhimu pia wa kuongeza mbolea kwenye mashamba yetu ili kuhakikisha ardhi inakuwa na rutuba ya kutosha.
Attachments
Upvote
2