SoC02 Kilimo chenye Tija

Stories of Change - 2022 Competition

Official sei

New Member
Joined
Jun 30, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Awali ya yote nipende kuwashukuru waanzilishi na wasimamizi wa jamii forum, kwa mchango wao mkubwa wnaotoa na kusaidia jamii katika kuhakikisha na kuleta mabadiliko katika kila sekta.

Ningependa kutoa maoni yangu katika kuelezea Ni jinsi gani tunaweza kutumia kilimo katika kuleta tija kwenye maendeleo:

Kitu pekee Cha kumshukuru mungu Ni kwamba Tanzania tumejaaliwa ardhi kubwa yenye rutuba nyingi ambazo zina saidia ukuaji wa mazao mbali mbali.

Kutokanana na uwepo wa kiasi kikubwa cha rutuba pamoja na ardhi ya kutosha hii jamii inapaswa kutumia vizuri rasilimali hii ili kuhakikisha kilimo kinaleta maendeleo katika jamii.

Hili linawezekana kwa jamii kuchukua hatua mbali mbali zitazochochea kufaidika katika kilimo hiki,

Kwanza, ili ufaidike katika kilimo lazima upate elimu na taarifa za kutosha kuhusu na aina na kilimo unachotaka kufanya,kila kitu kina Sheria,taratibu na kanuni zake ili kiweze kuwa Bora na chenye kufanikiwa, kwahiyo lazima uwekeze katika kupata maarifa sahihi katika kilimo au mazao unayotaka kujishughurisha nayo hii utasaidia Sana kujua Ni jinsi gani unaweza kutatua na kuepuka baadhi ya changamoto za kilimo.Mfano kwa kupata elimu juu ya mbegu Bora, ardhi Bora, njia za kukuza mimea, matumizi sahihi ya dawa za kilimo hii itasaidia kuhakikisha kilimo kinaenda sawa na kuongeza uzalishaji.

Aidha, lazima uhakikishe unawekeza rasilimali nguvu kazi, pesa, muda ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi, uwekezaji ama uzalishaji una husisha uwepo wa rasilimali ambazo zitatumika kiufanisi ili kuleta matokeo sahihi. Mfano kwa kuwekeza pesa za kutosha hii itasaidia uwepo wa watendaji wenye ufanisi, teknolojia nzuri, ardhi ya kutosha, pia muda utasaidia katika kuhakikisha rasilimali nyengine zinafanya kazi kwa ufasaha.

Pia, mkulima Ina mpasa kufatilia na kutafuta soko kabla ya uzalishaji ili kuwepo kwa uhakika wa mauzo ya mazao hayo, kwa kufatilia soko la mazao ambayo mkulima angependa kujihusisha hii itasaidia kuwepo kwa nguvu ya kujituma na kuwepo kwa uhakika wa mauzo endapo ata zalisha mazao hayo. Mfano kwa kufatilia soko utapata kujua mipangilio ya Bei za mazao hayo, uhitaji wa matumizi ya mazao hayo, ushindani wa soko, mbinu za uzalishaji, njia za uuzaji au uwasilishaji mazao sokoni.

Kitu chengine, Uwepo wa Sera na kampeni pia shughuli mbali mbali za kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu kilimo, pia serikali inaweza kuwekeza muda kuhakikisha inatoa elimu, inaanzisha kampeni na utaratibu wa kutoa elimu ikiwemo faida, jinsi ya kupambana na changamoto za kilimo, mbinu za kilimo nk kwa kufanya hivi w2 wengi wata hamasika na kuona kilimo ni ajira tosha kwa jamii pia itaongeza kipato Cha taifa kutokana na mauzo ya mazao hayo. Mfano Kama shughuli zinazoendelea siku za kutoa ruzuku, mashamba, na zawadi kwa wakulima Bora zina mchango mkubwa Sana katika maendeleo ya kilimo.

Kuhahikisha kuwepo kwa usimamizi mzuri wa kilimo, kwa kuhakikisha Kuna Bei inayowapa faida mkulima na mnunuzi wa mazao, mkulima kulipwa pesa kwa wakati, kuwepo kwa ushirikiano mzuri baina ya serikali, wakulima na wanunuzi hii itatengeneza mazingira Bora kabisa ya sekta hii ya kilimo hivyo basi kilimo kitaongezeka thamani zaidi. Mfano serikali inabidi kuweka mikakati ya kuhakikisha inapunguza muda wa malipo, inatoa taarifa sahihi kwa wakulima na wanunuzi wa mazao kwa kufanya hivyo kilimo kitaleta tija katika jamii.

Hata hivyo, kuwepo kwa vyama vya kilimo, hii itasaidia wakulima kupeana taarifa na hata kuwepo kwa mfuko wa umoja wa wakulima ambao utawezesha mkulima anapopatwa na uhaba wa fedha ili kuendeleza kilimo Bora, basi umoja huo kusaidia mkulima huyo pia hii italeta ushindani mkubwa na ulio bora katika kilimo.

Vile vile umoja wa wakulima utasaidia upatikanaji wa taarifa nyingi kuhusu kilimo na uchambuzi Bora kuhusu kilomo, ambapo endapo vitatiliwa nguvu basi kutakuwa na matokeo mazuri katika kilimo. Mfano kuwepo kwa chama Cha wakulima kutakuwa na uteuzi wa viongozi , watendaji wa kutafuta taarifa, wataalamu wa kilimo, pesa za kutosha pamoja na ushirikiano kwa wakulima hivyo kilimo kitaleta tija kwa jamii.

Kwa utoaji wa elimu kwa vitendo mashuleni, kuwepo kwa utaratibu wa elimu ya kilimo kwa vitendo katika mashule hii itaongeza uelewa, hamasa na hata ufatiliaji wa kilimo kwa vijana.Hivyo basi jamii itaweza kujiajiri katika kilimo kwa kiasi kikubwa. Mfano uwepo wa mashamba, vitendea kazi, elimu, na Sheria katika mashule pia na kuhakikisha vijana wanahusika katika kazi za kilimo kwa ukamilifu hii italeta matokeo mazuri zaidi katika kilimo.

Jambo Lengine, kuipa kipaumbele sekta ya kilimo Kama zilivyo sekta nyengine, kwa kuipa kipaumbele sekta ya kilimo itasaidia jamii kukipa thamani na kujituma pia kutumia mbinu mbali mbali ambazo zitafanya kilimo kuleta faida kiuchumi. Mfano kwa serikali kuweka bajeti nzuri katika kilimo ambazo zitaenda kusaidia Mambo mbali mbali ikiwemo utoaji wa ruzuku,elimu na utafutaji wa masoko itasaidia Sana kukua kilimo katika nafasi ya kiuchumi.

Kwa kuongezea, kuwepo kwa vyama vya utafiti kuhusu masuala ya kilimo ,kwa kuhakikisha kuna uwepo wa vyama vya utafiti vya kutosha na vyenye wataalamu walio bobea kwenye kilimo itaongeza chachu ya maendeleo katika kilimo kwa sababu kutakuwa na mbinu za kutosha za kuhakikisha kilimo kinaleta faida katika jamii. Mfano uwepo wa vyama hivi itasaidia uwepo wa mbegu bora, uwepo wa mbinu Bora za umwagiliaji dawa za kilimo ambapo itasaidia Sana katika kuhakikisha mimea Ina kuwa vizuri ili kuweza kuzalisha mazao mengi na bora.

Na mwisho, kudumisha umoja na mahusiano mazuri ya kimataifa katika maswala ya kilimo, kwa kufanya hivi kutaongeza uwepo wa maarifa makubwa ya kilimo ikiwemo mbinu za kisasa na Bora, itasaidia uwepo wa soko kubwa na la uhakika, kuongeza thamani na nguvu kazi katika kilimo. Mfano ushirikiano wa kimataifa katika suala la kilimo Ni chachu ya kuwepo kwa uwazi wa maarifa, misaada ya kilimo Kama pembejeo, fedha, na muda. Hivyo basi kilimo kitasaidia Sana katika kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja, biashara na taifa kwa ujumla.

Hivyo basi jamii inapaswa kuzijua changamoto za kilimo na kuzitatua ili kuwepo na matokeo mazuri katika sekta ya kilimo.
 
Upvote 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…