Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Kwa miaka sitini ya uhuru mkulima hajawahi pata bei stahiki ya mazao yake. Haya tunayoyaona leo ni matokeo ya kumnyonya. Watu waliacha kulima kahawa na chai sababu ya kunyonywa. Lakini sababu hao si mazao ya chakula hatukuona athari zake.
Lakini ukweli hata kwenye mahindi na mazao mengine ya chakula watu wameacha kulima. Kwanini ulime wakati kununua ni bei rahisi zaidi? Bora bodaboda au ukauze karanga kuliko kulima.
Matokeo yake hakuna anayewekeza kulima mashamba makubwa, kutumia matrekta au kulima kwa umwagiliaji licha ya kuwa na maji tele.
Tunachoona leo ni matokeo ya watu kukimbia na kuacha kuwekeza kwenye kilimo sababu ya bei za unyonyaji. Dhuluma hailipi.