Kilimo, Green Houses, Irrigation Information

mimi ni mkulima, nimependa kazi zao, nina safari ya iringa wiki ijayo, nitawatembelea kujua mengi.
 
Kuna utajiri kwenye kilimo,
Ila kwa bei yao ya Greenhouse za 7mil it is unfair!!

Unaweza ukawa sahihi kwa upande mmoja. Kwa upande mwingine ni vizuri kutumia mchanganuo. Nailoni zitumikazo ni maalum, mipira ya matone, mbolea, mbegu, madawa, vyote ni aghali. Hata hivyo, ukiangalia ki-mchanganuo, mil 7 zitarudi na zaidi kwa msimu wa kwanza na baada ya hapo ni faida kwa miaka mitano.
 
Mkuu,

Nimesema ni expensive sio kwa kulinganisha na huduma zitakazopatikana kutokana na hiyo Tshs 7Mil, bali suppliers wengine wa same products.

Mfano Balton wanatoa kwa Tshs 6Mil.

Kuna mdau mmoja wa hapa JF anaitwa mamaNa anatoa kwa approx. Tshs 4Mil (Angalia https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...08513-jenga-greenhouse-kwa-gharama-nafuu.html).

Pia wapo wakenya ambao ukizitoa kwao na kuzileta hapa haifiki hata Tshs 6Mil,

Jaribu kuwaambia hawa watu wawe fair kidogo ili huu utajiri utokanao na kilimo tuupate sio baada ya kurudisha cost kubwa!!
 
Last edited by a moderator:

Ninakushukuru sana kwa ushauri. Hata hivyo, wote uliowataja ninawafahamu. Tuna tofauti ya materials tunazotumia. Plastic za green house vile vile zina tofauti ya quality kulingana na aina ya mazao. Jambo la kuangalia vile vile kwenye eneo la technolojia hii ni kuwa huwa green houses zina expiry dates mara nyingi ni miaka mitano. Kuna green house za kuzuia aina fulani ya mionzi na nyingine zinauzwa used ambazo zina riskis.

Gharama zetu zinaweza kupungua kutegemea unalima nini, wapi, na wewe una uwezo wa kutupatia au kuchangia nini katika ujezi. Wakati wenzetu wanacharge flat rate ya mil 6 kwa 8m x 15m. sisi kwa 7mil unaweza kupata wooden green house ya 8m x 30m. Ninakushukuru kwa kutumia muda wako katika taarifa yetu. Wateja wetu wanaunafuu zaidi kuliko hao wote huenda kwa kuwa nimetoa ghrama ya makadirio inapotosha kidogo. Ukiwa tayari tutakupa gharama halizi.
 
Funguka tena zaidi basi kaka yangu,
Mnakua na any "after sales services" labda kumtembelea mteja wenu kuangalia maendeleo yake?
Hiyo bei inahusisha gharama za Upimaji wa Maji, Udongo, e.t.c? Kama haihusishi basi mnafanya kwa Tshs ngapi?
Vipi kuhusu gharama zingine kama installation of water (re)sources kama visima, mabwawa, simtank, e.t.c

Wajua hata hiyo link uliyoweka haina mchanganuo sana wa hivi vitu na tungependa kuvijua kwa undani ili kuepuka "hidden costs" zitakazokuja kutokea baadae!!
 

Kilmo chetu hapa tanzania haina ulazima wa kuotesha ndani yaani greenhouse tunachotaka ni namna gani ya umwagiliani wa mimea ktk njia ambayo ina punguza gharama na matumizi ya maji tu.
 
Kilmo chetu hapa tanzania haina ulazima wa kuotesha ndani yaani greenhouse tunachotaka ni namna gani ya umwagiliani wa mimea ktk njia ambayo ina punguza gharama na matumizi ya maji tu.

Umwagiliaji upo wa namna nyingi kutegemea aina ya mazao. Sisi sasahivi tuna vifaa vya umwagiliaji wa matone. Bei ya mabomba ya matone inafikia shs 950/= kwa mita moja na bei hiyo inaweza kuongezeka kutegemea imeingia dar kwa rate gani ya dola. eka moja hutosha mita 1000 kwa wastani japo itategemea aina na mimea na vipimo vitakavyotumika. Upo sahihi kwani kuna aina ya mazao yanalimwa nje ya green house na yanaingiza faida zaidi ya yaliyolimwa ndani ya green house. Ukuaji wa haraka wa mimea na ubora ni mingoni mwa faida ya green house na kuna baadhi ya mazao na mbegu ni lazima yalimwe ndani ya green house.
 

Hebu tupe update kwa sasa bei ikoje nimeitafuta hii sana, weka kwa kilimo cha nyanya.
Nimejaribu kucalclate,kwa makadirio ekari 60m*68m=4080m2
hapo utakuwa na line za ureru wa mita 60 zitakazo lala mwanzo hadi mwisho, pia kwa upana utakua na jumla ya mistari 113 yenye kuachana sm60, hivyo 113*60m=6780m
hivyo itakua mita6780 (makadilio)
 

Bei anza na Greenhouse ya mita 08 x 15 ambayo itakuwa na miche ya nyanya 600 sawa na kilo 12,000 kwani kila mche mmoja una uwezo wa kutoa kilo 20. Uwekezaji wa mwanzo waweza kuw ni shs 7 milioni kwa shamba kitalu lenye size ya mita 08 kwa 15 na uvunaji ni miezi nane mfululizo wakati unaweza weka vitalu shamba 20 katika eka moja vyenye ukubwa huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…