Kilimo kinakatisha tamaa, lakini usikate tamaa

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
Mwaka jana nimelima mahindi mkoa wa Kagera ambayo nimevuna (kwa hasara) mwezi march mwaka huu.

Nimepata hasara kwa sababu hali ya hewa haikuwa shwari, wengi tumekosa mvua za kutosha mwanzoni hali iliyopelekea kuharibikiwa mazao yetu (sio mimi peke yangu)

Kwa sasa shamba hilo nimepanda maharage, nashukuru mungu hali ni shwari..
============

Kilimo hasa cha kutegemea mvua chataka moyo! Lakini lazima tupambane kwani wote hatuwezi kuwa waalimu au mawaziri.

Nikiwa katika pitapita zangu juzi kati wilaya za kigoma (hasa kasulu & kibondo) nimeona watu wana mahindi mashambani swaafi kabisa mpaka niliwaonea wivu kwa kweli!
na huko sidhani kama kuna rekodi za matokeo mabaya ya mavuno.. Kwanza inaonekana ardhi za huko zina rutuba sana

Hebu wenyeji wa huko mnipe mawili matatu nataka nihamie huko mie![emoji4]
 
Ardhi ya Kigoma haina rutuba sana hasa Kibondo na Kakonko ila ardhi ya Kasulu ina rutuba kuliko maeneo hayo mengine.Maeneo ambayo hayakulimwa kwa miaka mingi sana ndiyo yenye rutuba na hayo ni yale ya vichakani , hayo ya kuona barabarani ni nguvu ya Mbolea ya ruzuku in short bila hiyo ungewaonea huruma hasa Kibondo maana ekari moja mtu anaweza kuvuna gunia 3 za mahindi ila kwa maharage Kibondo na Kasulu ni superb zao hilo linakubali bila mbolea
 
duh! Sawa mkuu nitatembelea maeneo hayo nipaone
 
Kila mradi ni Ghalama.
Kilimo kinatakiwa uwe na uhakika wa maji.
Unaweza kuchimba kisima kirefu na kuweka pampu ya sola kwa ajiri ya kwa na uhakika wa mazao kustawi.

Mradi wa kisima kirefu wastani unaghalimu m10. Pamoja na visaidizi vyake.
 
hapa sasa yafaa walau upate shamba lenye rutuba ili kupunguza gharama za mbolea, udeal na dawa na maji
 
Shamba lolote kwa hali ya hewa ya maeneo mengi ya Tanzania unaweza kupata mazao vizuri kama kuna maji.
Kuna njia za kuirutubisha ardhi isiyo na rutuba.
Ilimradi ardhi hiyo isiwe na mawe mengi.
 
njia ya kurutubisha ardhi ni ipi hyo[emoji848]
 
Aulize humu humu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Ma-Bwana na Ma-Bi-shamba wapo wa kumwaga tu.
Tatizo tunafanya kilimo kwa kutowashirikisha kwa kuhofia ghalama, wengine wanakushauri bure kabisa.
Ukienda Viwanja Sabasaba DSM au Mikoani wiki za maadhimisho yake, utapata ushauri wa Kitaalamu wa Ardhi, Mbegu na Mazao kalibu yote yote bure kabisa.
Kama inavyokuwa kwa fani nyingine, Kilimo cha kisasa cha faida kinahitaji sana mawazo shirikishi toka kwa wataalamu husika.
 
Tatizo in uoga kabisa mfano kuna group moja la WhatsApp yupo na Mtu wa Mbegu from seedco kuna group la tractor tupo na sales manager kutoka kampuni tofauti za tractors kikubwa tuache woga tuulize

Back
Top Bottom