Utangulizi
Sekta ya kilimo ni moja ya sekta nyeti duniani, ambayo inauwezo wa kuzalisha ajira nyingi kuanzia shambani hadi maofisini. Kilimo kimegawanyika katika makundi mawili ya mazao ambayo ni mazao ya biashara na mazao ya chakula .
Jamii nyingi za Afrika zimejikita Zaidi kwenye kilimo cha chakula badala ya kilimo cha kibiashara, ambapo familia nyingi zinzjihusisha na kulima eneo dogo kwa lengo la kujipatia mavuno ambayo yatakidhi mahitaji yao ya kila siku hasa chakula
Kuna uwezekano mkubwa sekta ya kilimo kuwa chachu ya mabadiliko na maendeleo ya kiuchumi katika jamii za kitanzania na kidunia kwa ujumla. Mambo yafuatayo yakizingatiwa yanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo;
Kuondoa dhana ya kwamba kilimo ni sekta ya watu walio feli shule; katika jamii nyingi hasa za kutanzania imezoeleka kwamba shughuli za kilimo zinapaswa kufanya na watu waliofeli shule na masikini. Dhana hii huambukizwa kwa mtoto kuanzia nyumbani hadi shuleni, ambapo mtoto hukalilishwa kwamba akifeli mitihani atarudi kuwa mkulima hali ambayo humpelekea mtoto kukua akiwa na dhana ya kwamba endapo atafaulu kwenye masomo yake hastahili kulima bali akaajiliwe ofisini.
Hivyo basi Serikali na sekta binafsi ambazo zinajihusisha na kutoa elimu kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu zinapaswa kukizungumzia kilimo kwa dhana chanya, ikiwezekana iwe moja ya somo la ziada mashuleni, Vivyo hivyo kwa wazazi.
Serikali na taasisi za kifedha kuweka mikopo yenye masharti nafuu kwa wakulima; Watu wengi ambao wanawiwa kujiingiza kwenye sekta ya kilimo hukata tamaa wanapokutana na vikwazo vya masharti magumu ya mikopo hasa upande wa riba na dhamana. Kutokana na kwamba sekta ya kilimo ni miongoni mwa sekta nyeti ni vyema wakulima watengenezewe mazingira rafiki ya kupata mitaji ili waweze kufanya kilimo kitaalamu na kwa ufasaha Zaidi.
Matumizi ya sayansi na teknolojia kwenye kilimo; Ili kilimo kiweze kuwa na tija kwa mkulima matumizi ya sayansi na teknolojia hayakwepeki, na hii hujidhihirisha kwenye Nyanja za uzalishaji wa mbegu bora ambapo matumizi ya mbegu izo hupelekea mavuno kuwa mengi, kitaru nyumba hii ni teknolojia ambayo humuwezesha mkulima kulima eneo dogo na akapata mavuno mengi, mifumo ya umwagiliaji
Teknolojia hii humsaidia mkulima kulima misimu ya mwaka mzima bila kutegemea mvua. Na zingine nyingi kama kulima kwa kutumia matrekta, combani harvester,kulima bila kutumia udongo, matumizi ya pestsides drones.
Masoko ya uhakika; Uhaba wa masoko ya ndani na nje ya nchi ni sababu kubwa inayo mkatisha tamaa mkulima kuzalisha mazao mengi kwa kuogopa hasara zitokanazo na ukosefu wa soko la mazao hayo. Ni wajibu wa sekta binafsi na serikali kutoa elemu sahihi ya masoko kwa wakulima na kusisitiza wakulima kuingia mikataba rasmi na wanunuzi kabla hawajalima zao husika .
Kuboreshwa kwa sera ya tozo (ushuru) kwenye mazao; Kiwango cha tozo anachotozwa mkulima wakati wa kusafilisha mazao yake kupeleka sokoni ni kikubwa hali inayopelekea mkulima kupata faida ndogo sana kulingana na gharama alizotumia shambani. Hivyo basi serikali iweze kuona namna ya kupunguza au kuondoa kabisa tozo za mazao.
Endapo mapendekezo yaliyo elezewa hapo juu na mengineyo kama hayo , ni wazi kwamba fursa nyingi zitaonekana kutoka kwenye kiliomo, mfano; Ajira zitaongezeka kwenye jamii kuanzia mashambani hadi ofisini.
Hali hii itapelekea pato la taifa kuongezeka pia, kwa kuwa uzalishaji utakuwa mkubwa na watenda kazi watakuwa wengi kwenye sekta hii. Ubunifu wa teknolojia mbalimbali za kilimo utaongezeka ,kutokana na kwamba mahitaji yake yatongezeka pia kwasababubu sekta ya kilimo itakuwa imekua kwa kiasi kikubwa. Na hii itachochea vijana wengi wabunufu kujitengenezea ajira pia. Na hii itapelekea kuwepo kwa mnyororo wa thamani na ajira kuwa mkubwa kwenye sekta moja.

Upvote
2