Jullyalfred
New Member
- Aug 12, 2022
- 1
- 1
Kilimo Kwa jamii nyingi hususani za kitanzania kinategemewa kuwa ukombozi mkubwa dhidi ya umaskini na hasa kwaajili ya maendeleo ya nchi kwa ujumla.Bado kuna utajiri wa ardhi katika nchi yetu ambapo kama watu wakiamua kuwekeza itakuwa ni moja ya njia ya kuchochea maendeleo hasa katika biashara.
Kwa tafakari pana kidogo jamii inaweza kuangazia katika moja ya vilimo vifuatavyo ambavyo vinaweza kuwa tija katika maendeleo ya jamii husika na nchi kwa ujumla:
Kilimo cha ngano,hiki ni kilimo ambacho kinaweza kuongelewa Kwa mapana na marefu pia kwasababu asimilia kubwa ya watu hata kidunia ni watu wengi wanategemea ili kuendeleza maisha na biashara zao za kila siku.Mfano mikoa inayolima ngano nchini Tanzania ni kama ifuatavyo Iringa,Kilimanjaro,Arusha Rukwa na Manyara
Endapo watu watajikita sana katika kilimo hiki basi nchi yetu ya Tanzania inawezekana kwenda mbali zaidi kiuchumi kwasababu watu wanategemea ngano kutengeneza asilimia kubwa ya vitafunwa kama vile chapati,maandazi,keki,biskuti,donati n.k ambayo hutumika majumbani ,mashuleni na katika hoteli mbalimbali. Hivyo basi hiki ni kilimo ambacho watu pamoja na wawekezaji wanapaswa kukiangalia kwa jicho la Tatu.
Kilimo cha mahindi,hii ni moja ya fursa ambayo watu wanaweza kukiangalia vizuri pia kwasababu Kwa namna yoyote Ile hakikwepeki hasa kwa jamii nyingi za Kitanzania.Baadhi ya watu wanatumia mahindi kutengeneza na kuzalisha bidhaa mbalimbali viwandani kama vile Unga ambao watu wengi wanatumia kupika ugali pamoja na kuzalisha Unga lishe hasa Kwa watoto kama vile Unga wa ulezi pamoja na matumizi mengine kadri ya uwezo wa watu na ujuzi.Hivyo basi kilimo hiki kitawezesha watu kuepukana na adha dhidi ya njaa na ukosefu wa chakula.
Lakini pia kilimo hiki cha mahindi kinaweza kuwa zao kubwa la biashara kwa ujumla ndani na nje ya nchi kwasababu kuna baadhi ya nchi ambazo hali ya hewa haikubaliani na mahitaji ya kilimo hiki hivyo watu wanaweza kuuza huko na kuendeleza maisha yao ya kila siku.Mfano wa nchi jirani ni kama Kenya ambapo hawana ardhi kubwa ya kilimo cha mahindi hivyo ni fursa mojawapo ya kufanya biashara na kuwekeza katika kilimo cha mahindi Kwani kina taja sana Kwa maendeleo hasa Kwa vijana ambao swala la ajira limekuwa changamoto kubwa kwao.
Kilimo cha miwa,pia hiki ni kilimo ambacho kinaangaliwa na wengi lakini ni vyema kinaangaliwa zaidi hasa Kwa vijana kama fursa kwao kwani ni ukweli usiopingika kwamba uzalishaji wa sukari unahitajika Kwa kiasi kikubwa sana kwasababu matumizi yake ni makubwa sana.Mfano wa mikoa ambayo inajikita katika kilimo hiki ni kama vile morogoro katika wilaya ya kilombero na kilimanjaro. Sukari inahitajika katika matumizi mengi kama vile ya vitafunwa mfano donati,maandazi na biskuti. Pia inatumika katika utengenezaji wa vimiminika mbalimbali kama vile soda na juisi hasa viwandani.
Hapa tunaweza kuona kwamba hata maendeleo ya viwanda Kwa asilimia kubwa inategemea na uwekezaji katika kilimo na juhudi za watu katika kilimo.Sukari inatumika na kushauriwa na madaktari wengi hasa Kwa wagonjwa wanaopata sukari ya kushuka na pia miwa imekuwa ikitumika kutengeneza juisi ya miwa ambayo ni nzuri na yenye ladha nzuri pia.Kwa kuwekeza katika kilimo hiki kitasaidia sana hasa katika biashara ili kusaidia bei ya sukari isipande sana na kila mtu aweze kumudu kununua hasa Kwa jamii wenye kipato cha chini kwasababu matumizi yake hayakwepeki.
Kilimo cha mpunga,hiki ni kilimo ambacho kinaweza kuitwa kama kitega uchumi na moja ya nafaka ambayo watu wengi wanaweza kukiangalia na kuwekeza,mpunga ukikobolewa unazalisha mchele ambao jamii kubwa ya watu wanatumia kama chakula.Hivyo basi mikoa ambayo inajikita katika kilimo hiki cha mpunga Kama vile Mbeya na Morogoro kuna haja ya watu kuendelea kuwekeza Kwa wageni na watanzania Kwa ujumla ili kukidhi mahitaji ya nchi katika upande wa biashara ili kuweka uwiano katika bei ili bei isishuke sana au kupanda sana ili kuwezesha wananchi wote kukidhi bei ya kununua bila kuathiri uchumi wa nchi na Soko la biashara kwa ujumla na kuhimiza na kuleta maendeleo yenye tija kwa ujumla katika jamii za kitanzania.
Hivyo basi mbali na vilimo tajwa hapo juu bado kuna vilimo vingine ambavyo vijana wanaweza kujishughulisha kama vile kilimo cha mbogamboga kwasababu ni dhahiri kabisa kuwa watu wanategemea sana mbogamboga za majani ili kupata mlo wa siku hasa watu wenye kipato cha chini lakini pia mbogamboga zinashauriwa kuliwa kwa wingi kwaajili ya afya njema.Pia kilimo cha matunda mbalimbali kinaweza kukomboa watu kiuchumi lakini pia kurahisisha upatikanaji wa matunda wakati wote kama vile maembe,machungwa,nanasi,ndizi,maparachichi n.k.
Hivyo kama vijana ambao wanakosa ajira wanapaswa kuangalia kwa umakini sana sekta ya kilimo kwani inaweza kuwakifikisha mbali zaidi kujipatia kipato na kuendeleza maisha yao ya kila siku.Lakini pia serikali inapaswa kuzidi kuwaunga mkono na kufundisha mbinu zaidi za kuongeza uzalishaji na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Pia kutokana na ukame ambao baadhi ya maeneo yanakosa mvua ya kutosha miradi ya kilimo cha umwagiliaji kinaweza kutumika kama mbadala wa mvua ili kuhakikisha kuwa uchumi hauyumbi na hivyo kutokuathiri maendeleo ya nchi zenye uchumi wa chini ambazo hujulikana kama nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania na hii itasaidia kufikia uchumi wa kati na hatimaje kuwa moja ya nchi zilizoendelea katika miaka ijayo kupitia sekta ya kilimo kama njia mojawapo ya kuhimiza maendeleo na pia kutokuwepo kwa uyumbaji mkubwa wa uchumi lakini pia kuondokana na adha ya njaa na pia kufikia malengo ambayo nchi yetu ya Tanzania imejiwekea.
TANZANIA YA MAMA SAMIA SULUHU, KAZI IENDELEE

Upvote
1