KILIMO KWA MANUFAA YA UCHUMI WATAIFA LA TANZANIA
Kilimo, ni sayansi na sanaa inayohusisha ufugaji wa mifugo, na kilimo cha mazao mbalimbali ya shambani, ikiwemo mazao ya biashara na chakula.
Kilimo kimekua msingi na uti wa uchumi kwa taifa letu la Tanzania, asilimia 68.9 ya Watanzania waishio mijini ma vijiji wanajishughulisha na kilimo kwa namna tofauti tofauti kutokana na ripoti ya shirika la chakula duniani (FAO), pia kutokana na ripoti hiyo ya FAO, inatabainisha wazi idadi ya mifugo iliyopo kwa sasa ikiwa ni pamoja naTanzania kua nchi ya tatu afrika kua na kiwango kikubwa cha ng'ombe ambao ni 25 milioni, mbuzi ni 16.7 milioni, kondoo 8milioni, nguruwe, 2.4 milioni, na kuku au jamii ya ndege 36 milioni, ambapo sector hii ya ufugaji inachangia kiwango cha asilimia 7.4% ya pato la taifa. Wakati kilimo kinachangia asilimia 26.7% ya pato la tanzania kutokana na ripoti ya shirika la chakula dunia (FAO).
Lengo kutoa takwimu hizi ni kufikilisha umma, ni kwa kiwango gani kilimo kimekua na mchango mkubwa kwa taifa la Tanzania.
Sababu zinazopelekea mkulima kushindwa kulima kwa ajili ya biashara.
1. Kushuka kwa bei za mazao na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji, gharama katika uzalishaji wa bidhaa za kilimo zimekuwa zikipanda kila kukicha huku bei za bidhaa za kilimo sokon zikishuka kila siku, hivyo bhasi kupelekea mkulima kukosa uhimilivu na kilimo na kuamua kulima kwa ajili ya chakula na kichache auze ili kukidhi mahitaji ya familia.Gharama za pembejeo zimekuwa zikipanda na kumuathiri mkulima moja kwa moja.
2. Upanuzi wa makazi na kasumba ya vijana wengi kuona kilimo ni kama mateso na kukimbilia mjini, lazima ifike mahala vijana waondolewe dhana potofu juu ya namna ambavyo wamekua wakifikiri na kuwaza juu ya kilimo, ufugaji na uvuvi pamoja na uongezaji thamani bidhaa za shamba, hii itapelekea vijana kua na mtazamo chanya unaolenga kufanya kilimo kama biashara na si mateso kama ilivyozoeleka hapo awali.
3. Kuongezeka kwa wadudu na magonjwa haribifu kwa mazao au bidhaa shamba, wadudu mbalimbali pamoja na magojwa ya wanyama na ndege kama nguruwe, kuku, yamekua yakiathiri sana ukuaji wa kilimo kwa Tanzania kwani yamekua yakirudisha nyuma hali za wakulima wengi sana katika ufugaji na ulimaji. Pia katika mazao wadudu na magonjwa yamekua kero kwa mazao hali inayopelekea kiwango kidogo cha mazao na kukosa ubora katika soko la dunia au kimataifa, hasa sumu kuvu (Aflatoxin).
Nini kifanyike ili kuboresha kilimo ili kiwe na tija kwa watanzania, yafuatayo yakifanyika kwaufasaha yanaweza kuboresha kilimo na kua ajira rasmi kwa Watanzania.
Sera thabiti zenye manufaa kwa wakulima, kama sera za kilimo zikiwa rafiki na mazingira ya wakulima, zitarahisisha uwajibikaji katika shughuli mbali mbalimbali za kilimo shambani, mfano wa sera ya 2015 ya KILIMO KWANZA, sera ambazo zitawasaidia vijana kujiajiri katika kilimo na kupewa mikopo rafiki itayowawezesha kuingia shamban na kujiri iliwezesha washika dau wengi pamoja na wawekezaji wengi ambao walivutiwa kuingia shambani ili kuendesha shughuli mbalimbali za kilimo ikiwemo usindikaji wa bidhaa mbali mbali na uongezaji wa thamani katika mazao ya shambani.
Kilimo huanzia sokoni, kilimo chenye tija na faoda huanzia sokoni, lazima mkulima awe na takwimu sahihi zinazohusu mazao na bidhaa mbalimbali za kilimo, taarifa sahihi zitamuwezesha mkulima kua na uhakika wa soko juu ya bidhaa zake na kua na bei rafiki kwa mkulima.
Bajeti sahihi kwa wazira ya kilimo, ili kilimo kiweze kukizi mahitaji ya kiuchumi na yanayoendana na nyakati, lazima bajeti sahihi itengwe kwa mahitaji sahihi ili iweze kuboresha secta muhimu kama umwagiliaji, uanzishwaji wa viwanda kwa ajili ya usindikaji na uongezwaji thaman katika mazao na bidhaa mbalimbali za kilimo.
Serikali isaidie utafutaji wa masoko ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na upangaji sahihi wa bei za bidhaa. Uhakika wa masoko ndio utasidia ukuaji wa kilimo kwani bidhaa nyingi za kilimo zitaweza kuuzika na kua na tija kwa wakulima ambao wamefanya kilimo kua biashara, kwan ukosefu wa masoko umekua kikwazo kwa wakulima wengi ambao umekua wakijihusisha na ukulima kama biashara, ambapo huwalazimisha kuuza kwa bei ya hasara inayoharibu mfumo mzima ajira za kilimo hivyo kupoteza mapato kwa serikali ambayo yangetokana na utoajia au uuzwaji wa mazao ya kilimo.
Utoaji wa ruzuku katika pembejeo za kilimo, utoaji wa ruzuku katika pembejeo za kilimo hasa mbolea ambao imepanda bei kwa kutoka na mfumuko wa bei katika bidhaa nyingi ndani na nje ya Tanzania, utoaji huu wa ruzuku utasaidia upatikanaji wa pembejro kwa wepesi kwa mkulima ambapo itakua ni chachu ya maboresho na mapinduzi makubwa katika sekta ya kilimo.
Uwezashaji wa sayansi na teknologia katika kilimo, katika zama hizi sayansi na technologia, kilimo kinahitaji sayansi ilikuweza kukidhi haja ya mahitaji ya kilimo, sayansi inahitajika katika kuzidhibiti wadudu waharibifu wa mazao na bidhaa nyingine katika kilimo, technologia itumike katika kuwekeza katika kivungulio (green house na screen house) katoka katika kamusi ya kiswahili( glosbe)viwanda ili viweze kukidhi mahitaji ya wakulima wengi. Sayansi na teknologia itumike katika ubunifu wa kilimo mwagiliaji na uvunaji wa maji ili kiweze kutumika katika misimu ya kiangazi, pia sayansi katika ulimaji na uvunaji ili kuweza kuzuia uharibufu wa mazo yakiwa shambani.
Kuwajengea uelewa wakulima na ili waweze kulima na kuzalisha mazao yenye tija na thamani kwa wakati (kilimo bustani). Kilimo bustani au (horticulture) ni kilimo kinachomjengea mkulima uwezo wa kiakili na uchumi kwani mazao yake ni ya kibiashara na ya mda mchache na yana thaman kubwa sana, mfano, miparachichi, vanilla, maembe, nyanya na mazao mengine ya kibiashara.
Lazima mkulima aongeze ubora na thamani ya mazao ili bidhaa za kilimo. Hii itatokana na wakulima kujengewa uwezo mbalimbali juu ya namna nzuri ya kuongeza thamani na ubora wa bidhaa mbalimbali za kilimo ili kuendana na soko la kimataifa na kweza kuleta ushindani sokoni. Pamoja na elimu hii pia wafundishwe namna sahihi ya kuzuia sumu kuvu(Aflatoxin) ambayo imekua ikileta madhara kwa afya ya binadamu na mazingira.
SULUHISHO
Ili kilimo kilete tija kwa mkulima lazima mkulima aanze sokoni ndio aingie shambani kwan tayari anakua ana taarifa za masoko na namna anaweza kabili bei za mazaosokoni.
Mwandishi Janke

Upvote
3