Narubongo,
Hapa cha kuangalia zaidi ni investment ya kufikia kiwango hiki cha ukulima. Mtu mmoja mmoja tutabaki kuwa subsistence farmers na ndio nauliza, je, haiwezekani investment kama hii kuwaunganisha interested parties kuwekeza ndio kutimiza mahitaji ya kifedha?
Niliangali clip nyingine kuhusu mining, machine zenyewe zikatajwa kuwa ni kati ya lati 7 na million 1 USD, na chimboni kuna sio chini ya machine 15 zinafanya kazi kila siku. Sasa hapa mtu mmoja mmoja kweli sio wengi wanawez lakini hapa hapa JF kila leo mtu anauliza afanye nini na mil5 zake? ndio labda kuna wengine wengi ambao wanaweza kuwekeza katika miradi na wao kupokea tu mafao yao mwisho wa mwezi/mwaka nk. cha msingi ni kuwa na huu utaratibu wa kuwa na fursa ya kujua ni miradi ipi ipo implemented/ ipo njiani na mtu kujipanga kuwekeza.
Ndio labda tunayo stock exchange, lakini upana wake ni mdogo na ni ya mashirika yaliyo simama tayari na sio hizi prospecting ideas.
Saccos kila kona ya mji, lakini sijasikia umoja unaowaunganisha watu kufanya kitu fulani, kuwaunganisha watu wenye nia ya kulima pamba, kulima matunda nk, SACCOS wanasubiri mtu huyo mmoja mmoja aje kuomba pesa za "kujikimu", na sio za kuendeleza mradi katika viwango hivi vya kimataifa.