Kilimo Kwanza: Wataalamu mko wapi

Kilimo Kwanza: Wataalamu mko wapi

guzman_

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,268
Reaction score
2,330
Protocol observed
Mimi ni muumini sana wa kutumia technologia za ndani na bidhaa zinazozalishwa nchini mana kwa kufanya hivyo naamini kuna watanzania wenzangu nimewasaidia ugali.
Jambo lililo nishangaza juzi nimeenda duka la vifaa vya kilimo. Nimeulizia panga naona limetoka china, Nikauliza jembe nikaambiwa yanatoka Kenya, nikaulizia folk sijui kiswahili wakaniambia China, nimeulizia Toroli nikaambiwa vyote hivyo wanaagiza China. Hivi kweli sisi ni wa kushindwa kutengeneza mapanga kweli. Tumeshindwa kutengeneza majembe kweli ni teknologia gani inahitajika kutengeneza majembe? ambayo hatuwezi na wataalamu wetu wameshindwa kuipa kipaumbele. Naelewa level ya tractor sio yetu ni hivi vidogo vidogo kweli?. Ikanilazimu kugoogle nipate viwanda vya kuzalisha zana za kilimo kiukweli tumelogwa na tumelogwa kweli kweli.
Hebu tajadili sisi Watanzania shida yetu ni nini hasa #MunguAturehemu#.
 
Back
Top Bottom