Kilimo, Miundombinu, Uzalishaji Kuipaisha Awamu ya Sita

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mtaalamu wa wa Uchumi na Fedha, CPA Issa Masoud, ametaja sekta tatu zinazoipaisha nchi kiuchumi, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Masoud alizitaja sekta hizo kuwa ni kilimo, usafirishaji na sekta ya huduma, ambazo zimeboreshwa kupitia uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali.

CPA Masoud alisema Rais Samia ameonyesha dhamira ya kuzalisha ajira na kukuza uchumi, kupitia kilimo, baada ya kuwawezesha vijana na wanawake 812, kushiriki kilimo biashara kupitia mashamba makubwa yanayosimamiwa na programu ya Jenga Kesho Bora (BBT). Alisema takwimu zinaonesha kwamba Tanzania ina nguvu kazi kubwa ya vijana ambao ni asilimia 75 nchini.​

“Ni mtaji mkubwa sana ambao Mheshimiwa Rais pamoja na Serikali yake wameuona kwamba hawa ndiyo nguvukazi, ndiyo wazalishaji wakubwa, lakini wengi unakuta wapo nje ya gurudumu la uzalishaji,” alisema.​
Alisema uwekezaji uliofanywa kupitia mashamba makubwa ni mkakati mahsusi na muhimu wa kuliwezesha kundi kubwa kukuza uchumi.

“Mimi ningesihi sana, wale ambao wanapenda kilimo, kwa sababu Tanzania imewekwa kama ndiyo kitovu cha chakula kwa bara letu la Afrika na ukiangalia hata sasa hivi vyakula vimepanda sana bei kwa sababu nchi nyingi zinachukua chakula kutoka Tanzania,” alisema.​

Alisema kupanda kwa bei za vyakula ni fursa kwa Watanzania kuwekeza zaidi kwenye uzalishaji wa chakula, badala ya kulalamika.​
Alisema nchi nyingi zinakabiliwa na uhaba wa chakula hivyo zinalazimika kukimbilia Tanzania kununua, hivyo ni fursa ambayo inapaswa kuchangamkiwa.

Kuhusu usafirishaji, alisema ujenzi wa miundombinu mingi nchini utarahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa, jambo linaloharakisha upatikanaji wa huduma.​
Anatoa mfano kwamba ujenzi wa meli kwenye maziwa makubwa, upanuzi wa bandari, uboreshaji wa viwanja vya ndege, reli ya kisasa, barabara na madaraja; ni ishara ya kurahisishwa kwa huduma ya usafiri na usafirishaji nchini.
Sekta nyingine aliyoitaja CPA Masoud ni ya huduma akizitaja za kifedha, simu na mtandao (internet); ni maeneo yanayochochea ukuaji wa uchumi na pato la mwananchi mmoja mmoja.​

Alisema Tanzania iko kwenye nafasi nzuri ya matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao, ikiwamo kutuma na kupokea fedha kwa simu pamoja na mawakala wa huduma za kibenki. “Kuna trilioni nyingi za fedha zinazunguka kwenye simu,” aliongeza CPA Masoud. Aidha, alisema uwazi wa mapato na matumizi ya fedha za umma, ni eneo muhimu linalotoa picha ya uongozi wa Rais Samia.​

Alisema ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeonyesha dhamira ya uwazi wa serikali ya Dk. Samia.​

“Ukiona ripoti ya CAG unapata dhamira halisi ya Rais katika kuijenga nchi. Unaona anachoamini ni uwazi. Hili ni muhimu sana kwa sababu kwenye uwazi utapata vitu vingi na ushauri mwingi pia,” alisema CPA Masoud alitoa kauli hiyo wakati ambao bajeti ya kilimo na upanuzi wa miundombinu zikiongezeka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…