SoC01 Kilimo mkakati na kujikomboa kupitia kilimo

SoC01 Kilimo mkakati na kujikomboa kupitia kilimo

Stories of Change - 2021 Competition

TechTino

Member
Joined
Oct 16, 2016
Posts
71
Reaction score
25
KILIMO - BIASHARA

Sekta ya kilimo ni sekta inayotegemewa sana katika kukuza uchumi na kuendeleza maisha ya watanzania walio wengi. Hata hivyo sekta hii imeendelea kutawaliwa na wakulima wadogo wadogo ambao ni takribani asilimia 70 ya watanzania wote. Kwa upande mwingine kilimo kinachangia kati ya asilimia 10-14 ya hewa ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabianchi na wanaoathirika zaidi na athari za mabadiliko tabianchi ni wakulima wenyewe kwa kuwa wao hutegemea kilimo kwa asilimia 100. Tanzania ina fursa ya kupambana na mabadiliko tabianchi hasa kwa kuboresha njia za kilimo.

UTANGULIZI– CHANGAMOTO
Changamoto nyingi zikiwamo udongo usio na rutuba, magonjwa ya mimea, wadudu na ukame husababisha wakulima wengi kuhangaika katika kuzalisha mazao kiuendelevu mwaka hadi mwaka. Katika ngazi ya kitaifa, changamoto hizi zaweza kusababisha ugumu katika kuelewa hali ya mazao na malisho, matarajio ya hali ya chakula, uhakika wa masoko na kiwango cha uzalishaji katika msimu husika.

Maamuzi iwapo chakula cha ziada kinahitajika kuagiza toka nchi nyingine kukabiliana na upungufu katika msimu husika yamekuwa yakifanywa bila kuwa na takwimu za kutosha juu ya mwenendo wa msimu na hali ya mazao shambani. Kumekuwepo mifano pia ambapo chakula kimeagizwa toka nchi za nje wakati ambapo kuna chakula cha kutosha nchini, hali ambayo ilisababisha kuwepo chakula kingi na kusababisha matatizo ya kifedha kwa wakulima wadogo kutokana na kuanguka kwa bei za mazao yao.

CHANGAMOTO ZA KILIMO
Sekta ya Kilimo ni muhimili wa Uchumi wa Tanzania, karibu asilimia 70 ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea shughuli za Kilimo. Mchango wa Sekta ya Kilimo kwenye Pato la Taifa umekuwa wastani wa asilimia 26. Sekta ya Kilimo kwa ujumla inaliingizia Taifa wastani wa asilimia 30 ya mapato ya fedha za Kigeni.

Hata hivyo, Uzalishaji wa mazao ya chakula na biaashara Nchini unakabiliwa na changamoto kama ifuatavyo,Wakulima wengi wanalima bila kufuata kanuni za kilimo bora, kutokana na huduma duni za Ugani na Utafiti, hawalimi na kupanda kwa mistari, kuweka Mbolea na madawa na kupalilia kwa wakati.

Changamoto hizo ni kama ifuatavyo:

Wakulima kukosa fursa ya kukopeshwa na taasisi za kifedha; Wakulima wadogo wadogo wanakosa fursa ya kupata mikopo toka taasisi mbalimbali za kifedha ili kuwekeza kwenye kilimo na hii inasababishwa na kutokurasimishwa kwa ardhi zao na kupatiwa hati miliki.

Kucheleweshwa kwa pembejeo za kilimo; Ili wakulima waweze kuzalisha zaidi na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu sana kuwa na pembejeo bora za kutosha na kwa wakati. Asilimia kubwa ya pembejeo za kilimo ambazo hutolewa na Serikali huwafikia wakulima zikiwa zimechelewa na hivyo kutokuwa na msaada wowote kwa wakulima.

Viongozi kutosimamia sheria na miongozo ya kilimo na mazingira; Kumekuwa na mapungufu makubwa katika usimamizi wa sheria ndogo ndogo za kilimo na misitu na kupelekea kilimo kufanyika katika maeneo yasiyotengwa na kusababisha uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji.Uharibifu wa misitu hasa unaotokana na kilimocha kuhama hama kimekuwa kikichangia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima wadogo wadogo.

Wakulima hutumia Teknolojia duni za Kilimo - Jembe la Mkono na Mbegu za asili.

Mfano wa zana duni za kilimo (Jembe la mkono)

9kKkHHreoWmSeZ1VN6Vv6c6jbSEEiJG5AZJhK9X6SSPeIvHzVxlbNTd1MMVtYZb5p2-wUniBcZDgvkSDvNE3XBFVUfFXaWHDLLOU4lkkm2ZwIxhReWe4f0pOtVeB7SMElYcuH8I


Wakulima wengi hulima kwa kutegemea mvua bila ya kuendeleza kilimo cha Umwagiliaji, ambacho kina uhakika wa kuvuna mazao mengi.

Upatikanaji na Matumizi hafifu ya Pembejeo za Kilimo – Mbolea, Mbegu bora na Madawa hayapatikani kwa wakati unapo yahitaji.

Miundo mbinu mibovu ya barabara na mawasiliano
Wakulima walio wengi wanaishi vijiji ambavyo bado havifikiki kirahisi kwa misimu yote ya mwaka na hivyo kushindwa kupeleka mazao yao kwenye masoko ya uhakika, matokeo yake wakulima wadogo wadogo wamekuwa wakiuza mazao yao kwa walanguzi wanaotembelea vijiji vyao kwa bei ya hasara na maisha yao kuendelea kuwa duni kila siku. Aidha vijiji vingi bado havina mawasiliano ya simu na hivyo wakulima kukosa fursa ya kufahamu bei ya soko la mazao yao kabla ya kupeleka sokoni.

Mfano wa taarifa ya bei za mazao ambazo hupatikana mtandaoni

6qTed-mnp0CDEzrF-jSDSpE8vdGim1uj93GXTIVJgwYSn0-Vu7Jb238QDVKzyvr0pGCykwx3Ix2BDfQDHRl7bWOSa6avO_IrUejSIkowRa9xS-UcKedBZ3MCXM9qCHw38UKWGkI


Ongezeko la migogoro ya wakulima na wafugaji, Kumekuwepo na migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji inayotokana na aidha kutokuwepo kwa mipango ya matumizi bora ya ardhi au kutosimamiwa vizuri kwa mipango bora ya ardhi na hivyo kupelekea vifo na ulemavu kwa baadhi ya wananchi. Migororo hii ya ardhi imekuwa ikizorotesha juhudi za wakulima katika kuongeza uzalishaji na kupambana na umaskini.

NJIA ZA UTATUZI WA BAADHI YA CHANGAMOTO

Mafunzo ya waganikazi,Ili tuweze kuwa na Mkulima wa Kisasa ambaye atakuwa na kipato cha juu pamoja na kupata fedha kwa ajili ya matumizi mengine ya kununulia mazao kutoka viwandani kama vile nguo, viatu na vyombo vya nyumbani, lazima tuongeze Tija na Uzalishaji wa mazao.

Mageuzi ya sera na Sheria, Kuweka Mfumo bora wa upatikanaji wa Ardhi kwa vijana wanaojishughulisha na Kilimo-Biashara, Kuboresha ufanisi wa Masoko ili kutoa bei nzuri ya bidhaa mbalimbali kama vile Maghala na Mifumo ya taarifa, Kuanzisha masoko kwa maeneo yaliyo tengwa, Kuanzisha Mashamba makubwa ya Kilimo cha umwagiliaji kwa Vijana, Matumizi sahihi na endelevu ya maji katika kilimo cha umwagiliaji na Mfumo wa uzalishaji wenye kutunza Mazingira.

Uhamishaji wa teknolojia na matumizi yake katika mazingira mapya , Kupunguza gharama za zana za kilimo na mbegu, upatikanaji wa ruzuku za Pembejeo toka Serikalini na Utekelezaji wa vipimo sahihi kwa bidhaa zilizozalishwa.

Vijana Kujenga utamaduni wa kuweka akiba ya kifedha , Kuunganisha Makundi ya Vijana na taasisi au wadhamini wa kifedha.

Kusisitiza Utoaji wa asilimia nne (4%) Kwa Vijana zitokanazo na mapato ya ndani ya halmashauri, Kutoa elimu ya Kilimo-Biashara mashuleni , Matumizi Bora ya Mifumo ya Teknolojia na kubadilishana ujuzi na maarifa kwa vitendo miongoni mwa vijana wenyewe.

Serikali itoe kipaumbele katika kuendeleza huduma za jamii vijijini kama barabara, zahanati, shule, masoko na mitandao ya simu. Vile vile kiongozi atakayechaguliwa ahamasishe wananchi kuanzisha vituo vya kuuzia mazao na kusimamia sheria ndogo za kuzuia wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia vipimo visivyo sahihi vinavyowaibia wakulima mazao yao na Serikali kutopata kodi stahiki.

Viongozi wahakikishe kwamba bajeti kwa ajili ya kilimo inaongezwa ili kufikia maazimio ya mkutano wa Maputo (asilimia 10 ya bajeti ya Serikali ielekezwe kwenye sekta ya kilimo. Hii itaboresha upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati, utoaji wa elimu ya ugani kwa wakulima na utatuzi wa changamoto za masoko.

Viongozi waweke mkazo katika kuwajibisha watendaji ambao watashindwa kusimamia mipango na sheria ndogo za usimamizi wa misitu na kilimo. Pia elimu ya kilimo na mazingira iendelee kutolewa kwa wadau mbalimbali ili kila mtu afahamu wajibu wake na kuutekeleza.

Viongozi waweke kipaumbele katika kutengeneza na kuisimamia kikamilifu mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kupima ardhi na wananchi wamilikishwe ardhi zao kisheria.Hii itasaidia wakulima kuwa na hadhi ya kukopesheka na hivyo kuendeleza shughuli zao za kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi.

Serikali wahakikishe kuwa michakato ya ugawaji na umilikishaji wa maeneo ya ardhi kwa wawekezaji inafuata taratibu za nchi, inafanyika kwa uwazi na wananchi wanashirikishwa kikamilifu ili kuepuka migogoro mikubwa kati ya wakulima na wawekezaji, kutokana na wananchi kukosa maeneo ya kutosha kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi.

Ili kuepuka migogoro ya wakulima na wafugaji, Serikali iwekeze katika kuboresha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji ili wafugaji wabaki katika maeneo yao. Hii ni pamoja na kuweka miundombinu ya maji na malisho kwenye maeneo ya ufugaji.
 
Upvote 1
Mkuu mbona bandiko limeishia njiani? Nilitarajia nione conclusion hapo chini
Sijaweka conclusion nimeona maneno yamezidi na siwezi kuyapunguza ila nilichofanya points mbili za mwisho zime conclude!!
 
Sijaweka conclusion nimeona maneno yamezidi na siwezi kuyapunguza ila nilichofanya points mbili za mwisho zime conclude!!
Hapo sawa...! Ila vizuri ungebanabana maneno ili tusome na majumuisho. Ila umejitahidi kuandika, kazi nzuri
 
Back
Top Bottom