Kilimo na matumizi ya bidhaa za tumbaku upigwe Marufuku

Situmii sigara wala cannabis ila mazingira nilipo kuna wavuta sigara vijana wengi sana na baadhi naona wanalalamika vifua vinawabana na wanakohoa sana usiku.
Na huo moshi wa sigara, akiuvuta asiyevuta, bado una madhara kwake pia. Takwimu za wanaokufa kwa kuvuta moshi wa sigara pasipo kuvuta sigara inafikia watu milioni 1.2 kwa mwaka dunia nzima.
 
Kama suala ni kuchangia pato la taifa, basi nina uhakika hata bangi ikihalalishwa inaweza kuchangia pato la taifa pengine hata kuzidi tumbaku.
 
Kama suala ni kuchangia pato la taifa, basi nina uhakika hata bangi ikihalalishwa inaweza kuchangia pato la taifa pengine hata kuzidi tumbaku.
Kiufupi sisi kama nchi tunapelekeshwa na mataifa ya nje..yakisema hii na haramu tuna haramisha..yakisema hii ni halali hata kama inaumiza afya za watu wetu tuna halalisha.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…