Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Safi sana, tatizo kubwa miongoni mwa watanzania ni kuogopa KUTHUBUTU
 
Naomba unipe mwanga kidogo ndg maana nna huo mpango wa kulima vitunguu pia
 
Unatoa uoga kwa watu bila maana wewe.mtu alieleta haya maneno hapa nakiishi hicho kilimo wewe unaleta maneno.haya ni madhara ya kukaa chuoni bila kunaribu na kuja mtaani kuzunguka na bahasha kutafuta viti vya kuzunguka
 
 
iko siku utakuja hapahapa kutuambia hakuna biashara mbaya kama ya kilimo note me kila jambo na wakati wake kuna wakati wa kucheka na wakati wa kulia
Hata ajira watu wanafukuzwa kaz au kuumia kazini bro everything has risks
 

Umekariri hujaelimika.Maisha halisi elimu yake haiko darasani inapatikana mtaani.Ukisubiria ya darasani utabakia kuwa mwana nadharia.Maisha hayana huruma ya nadharia yanaheshimu vitendo.

Nikurudishe darasani.Jikumbushe siku ya kwanza ulipofundishwa kuandika a,e,i,o,u je ulipewa hadithi ya simulizi tu au uliambiwa tenda kwa kuonyeshwa namna ya kufanya.Ukimaliza elimu ya kiwango chochote ile iwe shule ya Msingi,Sekondari ya kidato cha nne,sita au chuo ukajikuta huna chochote cha kufanya tambua tatizo si hicho wanacholalamikia wengi.Tatizo ni wewe au waliokulea.

Yawezekana ukawa wewe kwa kuwa ulitegemea miujiza au baba na mama,wajomba na ndugu wengine.Yawezekana mchango mkubwa ni walezi wako walikulea kama kuku wa kisasa anayesubiri kuletewa kila kitu alipo.Mletaji akiumwa nawe waumwa njaa.Akifa wafa kwa njaa.

Nisamehe najua ujumbe huu unamaumivu makubwa lakini kwa kuwa nakupenda lazima niuseme,vinginevyo utaishia kulaumu tu.Lawama haizai ,uthubutu unazaa.
 
Kulima nilitumia ng'ombe zangu, ila kama ningelinunua basic gharama yake isingelizidi 80,000/= mbolea niliweka ya kupandia tu, nililima ekari mbili sio moja.
Mkuu achana Na kuwashauri masharobaro wavaa mitepesho ngoja waendelee kula ugali Wa shikamoo!
 
Watanzania wengi wanaishi vijijini na shughuli yao kubwa ya kiuchumi ni kilimo, karibu theluthi moja ya watanzania ni masikini na sehemu kubwa ya theluthi hii wanaishi vijijini ambako shughuli kubwa ya uchumi ni kilimo.
We ni kilaza Wa kiwango cha lami hivi hujui watu Wa mijini wanastarehe kwa kunyonya jasho la mkulima!!
Umaskini Wa vijijini unatokana kwa kiasi kikubwa Na Huduma duni za elimu afya umeme Na miundo mbinu.
 
Naombeni soft copy ya kitabu kizuri cha kilimo nichimbe maarifa
 
Kilimo ilikua inaonekana ni kazi za mafukara,sasa hivi kila mtu anakimbilia kulima,magu kabana biashara mjini haziendi km kipindi cha jk.watu sasa wameamua kulima tu.tatizo linakuja wakilima wengi,supply inakua kubwa,demand inashuka,bei inaenda chini.profit inakua ndogo
 

Na wengi hili hawalijui.
 
We ni kilaza Wa kiwango cha lami hivi hujui watu Wa mijini wanastarehe kwa kunyonya jasho la mkulima!!
~Umaskini Wa vijijini unatokana kwa kiasi kikubwa Na Huduma duni za elimu afya umeme Na miundo mbinu~.

Ningekuuliza aina gani ya elimu. Maana kiuhalisia mimi ninayeishi kijijini naweza kukudhibitishia kuwa umaskini wa kijijini ni matokeo ya fikra mbovu za watu, matumizi mabaya ya pesa.
Hata watu wa mjini wana matumizi ya ovyo, tofauti ni vitu tunavyonunua.
Kijijini tunashindana kunywa mataputapu huku mjini wakishindana kuweka sofa za gharama, magari nk wakati uwezo wa kumudu bado
 
We ni kilaza Wa kiwango cha lami hivi hujui watu Wa mijini wanastarehe kwa kunyonya jasho la mkulima!!
Umaskini Wa vijijini unatokana kwa kiasi kikubwa Na Huduma duni za elimu afya umeme Na miundo mbinu.

Wewe ambaye sio kilaza naomba majibu ya maswali haya kwa vielelezo, hivi ni watu wa mjini au serikali ndio yenye jukumu la kuboresha huduma za elimu, afya, umeme, maji, na miundo mbinu ya vijijini pamoja na mijini? Watu wa mjini wanamnyonyaje mkulima? Na kama kuna unyonyaji serikali ipo wapi? Je, sera na sheria za kilimo na biashara zinasemaje juu ya jambo hili?
 
mm nililima mwaka jana matikiti kwani sikufanikiwa kupata kitu zaidi ya matikiti ya machache ya kula home basi ndo niliambulia ndo maana kilimo ni balaa ila sikati tamaa nitaaingia tena kwa upya kulima
Dah!! Pole sana acha nami nijipange
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…