Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Moja ya fikra pumba nilizowahi kushuhudia hii.
 
Mbona inawezekana brother? Acha kudhani haiwezekani kisa haijakutokea wewe.Ekari moja ya mahindi inaweza kutoa hata gunia 30 na zaidi za kg 100 zikilimwa kitaalamu sasa akikuta bei ya kilo moja sokoni ni Tsh 1000 hiyo si ni milion tatu kamili?

Afu gharama ya kulima watu wamekariri ohh hela ya kukodi ardhi wakidhani kila mtu analima kwa kukodi kumbe kuna watu wanalima mashamba ya wazazi wao au ya watu waliowapatia tu walime mfano mzuri ni mimi mwenyewe nalima zaidi ya ekari 7 na hakuna hata moja niliyoikodi sasa ondoa gharama ya kukodi weka hivi

[emoji116]
Kulima ekari 1 Tsh 80,000
Mbegu 60,000
Kupanda 50,000
Kupalilia 100,000
Mbolea DAP 60,000+Urea 54000+CAN 43,000
Mifuko 15,000
Kuvuna avune mwenyewe
Kusafirisha atumie mkokoteni au punda [emoji23][emoji23][emoji23]

Jumla Tsh 462,000#

Hata hapo nimepiga cost za juu kwenye mbolea maana kuna mashamba mengine hata mbolea ya dukani hayahitaji kutokana na rutuba yake murua kabisa


Kuna watu wananunua mbegu tu na mifuko tu , kulima wanalima wenyewe kupalilia wanapalilia wenyewe ,kuvuna wenyewe na wanavuna good tu wakipata bei poa wanapiga pesa nzuri tu.

Lakini pia unaposema kilimo hakilipi eti kinalipa kwa matajiri kwani hao matajiri walizaliwa matajiri? Kupata kunazidiana ndiyo maana kuna wakulima wana mtaji wa kilimo bilion 2 wengine laki 2 na kila mtu anapata faida kwa viwango vyake , nikiweka laki 2 nikapata laki 5 au 6 faida hapo laki 4 sasa utasemaje hakuna faida? Kikubwa kumaintain juhudi na kutafuta namna ya kutatua changamoto zinazokukabili kama mkulima utafanikiwa tu.

Hata mimi niliota kulima ekari 1 ila nikafanikiwa leo hii ukiniambia nilime ekari moja naona unanitania leo nipo ekari 7 japo sijafika ekari 10 but mwaka huu namwomba Mungu nifike 10 na zaidi malengo ni siku moja nilime ekari 100 hata na zaidi na nitafanikiwa nisipokata tamaa
 
Upo mkoa gani..? kwa hekar mbili hizo gunia ni possible, mi mwenyewe nafanya kilimo cha mahindi ila bei zinatuangusha masalani kwa sasa gunia linauzwa 40k
 
Nakuunga mkono mimi nalima takribani ekari 20 ila huku niliko rutuba ipo vizur Dap haihitajiki na tunavuna wastani wa gunia 10-25 kwa hekari,huku mvua sio changamoto hata kidogo shida kubwa ni network ya masoko ndo inatutesa sana,huwezi jana tu nimetoka kuuza gunia 25/1000k kwa ajili ya dogo shule utaona jinsi bei zinavotufelisha.
 
unawaponza watu mzee baba
 
Mkuu popote ulipo kunywa kahawa na kashata ntalipa. Au kwa kuwa upo Tarime kula nyama kwa kichuri bill ni yangu.

Umeleta hoja ya maana sana kwetu sisi vijana tunaohangaika kutwa kucha kutafuta kazi za laki 4 kwa mwezi. Ukizoea hizo project za kilimo ndogo ndogo zinakupa mahitaji karibu yote muhimu.
Binafsi nadeal na mahindi na mpunga. So nasupport hoja yako from real experience na currently nalipa hadi ada ya chuo kwa kilimo.
Ila kama hutojali naomba unisaidie namna ya kupata hiyo mbegu ya DK niijaribu coz me nmekua nikiitumia seedco.
 
Unalima wapi mkuu?
 
πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ we jamaa nimecheka hi komenti yako.
 
Nalima ila kilimo kinahitaji pesa sana aisee nashangaa sana mnavyowasema vijana wanaohangaika kutafuta ajira,unamwambia afanye kilimo atalima na nini wakati hata pesa hana!! Kilimo cha hekari 2 hakiwezi kuja kukutajirisha labda upate chakula cha familia tu.
Binafsi nimelima hekari 60 za mahindi unadhani kijana gani anayejitafuta anaweza kuwa pesa za kulima hekari zote hizo?
Acheni kuwabeza vijana wanaohangaika na bahasha,kilimo sio rahisi kama mnavyofikiri
 
Waambie wasiwabeze vijana
 
Acha kutishia watu wewe huku kilwa kijana ukiwa na laki 3 unalima shamba la ufuta heka 5 safi kabisa
 
Na hiyo mishahara haina uwiano na ile ya watawala ili waendelee kuwa weak
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…