SoC02 Kilimo ni fursa

Stories of Change - 2022 Competition

yansen

New Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
4
Reaction score
5
KILIMO NI FURSA

Neno mkulima limetokana na kitendo cha kulima,hivyo mkulima ni mtu yeyoyote anaejishughulisha na shughuli za kilimo.

Shughuli hii imekuwepo tokea karne nyingi zilizopita kwakuwa maisha ya mwanadamu yanategemea chakula na chakula kinazalishwa kupitia shughuli ya kilimo. kumbe basi bila kilimo hakuna chakula na pasipo chakula hakuna uhai,pia mazao yatokanayo na kilimo ndio hayo hayo yanayotegemewa kutoa malighafi za viwandani, ujenzi N.k,hivyo basi bila kilimo kuna baadhi ya viwanda haviwezi kufanya uzalishaji,mfano viwanda vya karatasi,sukari, pombe,nguo N.k,hivyo hata wafanya kazi hawawezi kufanya kazi pasipo kuwepo mkulima anayezalisha malighafi hizo za viwandani.

Nikizungumzia neno kilimo nazungumzia kwa mapana yake kwakuwa kuna kasumba ambayo imekuwa katika akiri za watu wengi walio na elimu na wasio na elimu yakwamba mtu ukiitwa mkulima basi ni mtu ambae anajishughulisha na kulima ardhi tu nakupanda mazao kisha kuvuna mazao.

Neno hili limekuwa likitumika kinadhalia sana kiasi kwamba linapotosha maana mtambuka ya kilimo,tunapozungumzia kilimo tunazungumzia mfumo wa uzalishaji mimea, tunajumuisha na shughuli za ufugaji wa wanyama na ufugaji wa wadudu kama nyuki pia tunajumuisha ufugaji wa samaki na uvuvi,hii ndio inabeba maana kamili ya kilimo.

Hivyo basi kwa dhana hii nipende kuzungumzia namna kilimo kinavyoweza kubadiri maisha yetu kutoka hari ya chini kutupeleka hari iliyo bora zaidi hasa kwa vijana walio wengi pengine wanamitaji midogo wanataka kukuza mitaji au hawana kabisa mitaji wanataka kutengeneza mitaji ili kwa baadae watimize ndoto zao.

Naandika andiko hili kwa vijana warika zote kuona umuhimu wa kilimo kama mkombozi wa malengo na ustawi wa uchumi kwa kila mmoja mmoja.

Kwanza kabisa ijulikane kilimo kimegawanyika katika aina tatu,aina ya kwanza ni kilimo cha saizi ndogo wazungu wanaita small scale agriculture,kuna kilimo cha kati wazungu wakikiita medium scale agriculture,na kilimo kikuu wazungu wakikiita large scale agriculture.

Hivyo basi kupitia aina hizo kama kijana anaehitaji kujikwamua ni ukubwa gani wa kilimo anapaswa kuchagua ilikupiga hatua?

Kabla yakuchagua, je unatambua unataka kujishugulisha na kuzalisha zao gani la kilimo? ,je kama hauhitaji kuzalisha zao unataka kujishughulisha na ufugaji? Je umesha tambua unaenda kuanzisha ufugaji wa aina gani?wanyama?Au ni ndege? au ni samaki, au ni nyuki?nivyema kabla haujaamua kufanya shughuli ya kilimo ukatambua nini hasa unahitaji kukifanya katika kilimo itakuwa vyepesi kukupa nafasi yakuendelea. Katika sekta ya kilimo kuna fursa nyingi ambazo kama mtu ukituliza ubongo nivyepesi kufanikiwa.

Zifuatazo nifursa ambazo nimezigawa katika makundi kadhaa nikianzia katika kilimo cha mazao ya shambani,mazao ya misitu na mazao ya mifugo.

A/-Mazao ya shambani,kupitia fursa hizi kijana anaweza kujikita katika kilimo cha mpunga,kilimo cha maharage,kilimo cha mahindi,alizeti,karanga,pamba,korosho,ufuta, N.k
kupitia fursa hii inawezekana kuanza na kilimo cha kati ambacho katika kutekeleza mpango hutekelezwa kwa malengo ya kulima kwaajiri ya biashara wala sio kwaajiri ya matumizi ya chakula, kila zao hulimwa maeneo husika na mikoa husika,nakutokana na misimu na majira ya mvua, kwahiyo unatakiwa kabla hujaanza kuingia kufanya kilimo ujue niwapi utaenda kuanzisha hiyo shughuli yako ili ikupatie manufaa, uzuri wa aina hii unaweza kuendesha kilimo kwa kutumia gharama ndogo kulingana na bajeti yako ulio jiwekea kwamba unahitaji kulima kiasi gani cha eneo,

B/- Mazao ya misitu,kupitia fursa hizi unaweza anzisha kilimo cha kupanda miti ya mbao,miti ya nguzo za umeme,,miti ya matunda mfano machungwa,parachichi,maembe,papai,limao N.K, vyote hivi vinawezekana. Pia unaweza anzia kilimo cha size ya kati kulingana na bajeti yako ulivyo iweka.

C/- Mazao ya mifugo,kupitia fursa hizi kuna ufugaji wa nguruwe,mbuzi,kuku wa kienyeji,kuku wa kisasa wa nyama na mayai, ngombe, pia ufugaji wa samaki kwenye mabwawa,ufugaji wa nyuki N.k.

Hizi zote nifursa ambazo zikitumika vizuri hakika zinabadirisha mstakabali mzima wa mambo ya kiuchumi kwa watu wengi walio ajiliwa na wasio ajiliwa,na ndio maana wakasema kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu.

Nafahamu kwa maelezo hayo juu kuna baadhi ya watu wataanza kujiuliza inawezekanaje mtu asiye na mtaji aweze kufanya kilimo kinacho zungumziwa hapo?Ndugu yangu kijana mwenzangu maelezo yaliyoelezwa humu ni mengi na sio kila lililoelezwa unaweza lifanyia kazi, chagua fursa moja unayo ona itakutoa sehemu A kukupeleka sehemu B kulingana na bajeti yako baada ya hapo utanishukuru au utawashukuru wajukuu zangu, mfano mzuri tuchukue kwamba wewe unae soma andiko hili nikijana usiye na mtaji, lakini bahati nzuri umebahatika ukawa na shilingi elfu ishirini tu mfukoni huo ni mtaji mkubwa sana,unahitaji kwanza ujiamini,uondoe uoga kisha uthubutu utafanikiwa,mfano katika kuchagua fursa basi chukua wazo la mazao yatokanayo na ufugaji,kisha chukua ufugaji wa kuku wa kienyeji,tumia elfu 20 kama mtaji,nunua kuku mtetea mmoja tu ambae sio mkubwa sana wa miezi Minne atauzwa elfu 8 nunua chanjo newcastle ya kumkinga na kideli kwanza elf6 au 7 mpige chanjo,muache ale maisha baada ya miezi mitatu atakuwa sio kuku mmoja,watakuwa kuku 6-7 au 10 kutokana na uangalizi wako,hao kuku 6 -7 au10 kama watakuwapo matetea hata 4 tu baada ya miezi mitatu sio kuku 6-7 au 10 tena nizaidi ya kuku 30 pigia hesabu hiyo kama utafanya kwamalengo baada ya miezi 9 mpaka 12 hakika utakuwa mbali sio chini ya kuku 70 au zaidi ya hapo,utakapo kuja kuwauza haitakuwa elfu20 tena hiyo.

kumbe basi mtaji mdogo sio kikwazo cha mtu kuanzisha shughuli kikwazo ni utiari na uthubutu wa mtu husika.

Inawezekana kuna mtu mwingine anasoma andiko hili anajiuliza inawezekana vipi nianzishe kilimo wakati mtaji wa kulima ardhi Sina?,kulima mpaka ukodi shamba,uandae shamba N.K,ndugu yangu kijana mwenzangu,kwataarifa yako asilimia kubwa ya watanzania tuliopo mjini tumezaliwa vijijini au vijijini ndio lilipo chimbuko letu,huko vijijini unaweza pata hata eneo la kuanzia mfano mashamba ya familia utalima utakuza mtaji baada ya hapo unaweza pata mtaji hata wa kukodi hekari miamoja,uthubutu ndio kila kitu wala sio mtaji.kumbuka pia wahenga walisema mtaji wa masikini ninguvu zake mwenyewe na ili uweze kupata sharti uumie.

Mwisho nipende kusema kilimo ni biashara kama biashara zingine,kilimo nishughuli kama shughuli zingine,kuna fursa nyingi katika kilimo nilizoeleza na zile ambazo sijabahatika kuzieleza katika andiko hili,ukifanya kilimo katika ubora wake na ukawaida wake hakika hautojutia kufanya shighuli hii,pia nitoe wito kwa jamii yote kutambua kilimo ndio ajira pekee iliyo wazi isiyohitaji kusubiri zitangazwe nafasi ili uombe,niwakati wako sasa kuthubutu ili uweze kuongeza pato lako na kukuza uchumi wa familia yako na taifa kwa ujumla,shughuli ya kilimo haibagui yeyoyote anao uwezo wa kuifanya, changamkia fursa hata ukiwa ofisini fursa katika kilimo ninyingi chukua fursa ongeza kipato chako.

Kwa vijana wenzangu waliopo vijijini na mjini kama ilivyoelezwa kwenye andiko hili kilimo kina nyanja nyingi,nafahamu kuna watu hawataki kusikia kuhusu kulima basi sikia kuhusu kufuga.

Mazao yatokanayo na kilimo bado yana nafasi kubwa katika uchumi wetu wa hapa TANZANIA na kila kitakacho kuwa tiari kimezalishwa basi tambua hiyo ni pesa.
 
Upvote 4
Kura yangu nakupa,Uzi umetulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…