Kilimo ni kujipanga

Mkirua2

Member
Joined
Oct 15, 2019
Posts
30
Reaction score
30
Katika jambo lolote unalotaka kulifanya, ni muhimu kuweka katika mpangilio unaoeleweka. Yaani ujue mwanzo na mwisho ili unapotoka hatua moja ujue unaenda mbele au nyuma.

Hivyo hivyo kwenye kilimo, ni vyema kijipanga. Unaweza kuwa na eneo kubwa kwa ajili ya kilimo alafu mwisho wa siku ukashindwa kulitumia kwa ufanisi, mwisho wa siku ukawa unapoteza pesa kwa kuandaa shamba lote ili hali ungeweza kulima eneo dogo na kupata matunda mazuri ya kazi yako.

Hivyo basi, ukiwa kama mkulima wa faida, inakubidi uwe na mpangilio katika shamba lako, unaweza kugawa katika maeneo madogo madogo kulingana na vigezo mbalimbali kama aina ya udongo, mwinuko, barabara, muda wa mavuno, uhimili wa magonjwa, uhitaji wa maji na mengineyo mengi.

Hima kwa wakulima au wanaopenda kulima maeneo makubwa, tafuta wataalamu wakusaidie kukushauri na kukupangilia shamba lako katika mpangilio sahihi.

Usikurupuke kulima tu kwa sababu pesa ipo, kila kitu ni mipango.

Kwa ushauri zaidi wasiliana nami.
 
Wewe ni mkulima wa vitendo au makaratasi? Na unalima mazao gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…