SoC04 Kilimo ni kumuwezesha mkulima

SoC04 Kilimo ni kumuwezesha mkulima

Tanzania Tuitakayo competition threads

the slave

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Kama kijana ninaendesha maisha yangu kupitia kilimo naamini mawazo yangu yatasaidia kuboresha kilimo ambacho ni chanzo cha ajira ya karibia asilimia 60%ya watanzania.

Yafuatayo ni maboresho ambayo yataweza kusaidia kuleta tija katika nchi yetu kupitia kilimo

Serikali kutafuta mbadala wa viatirifu katika mazao,kwa maana viatirifu vingi vimekuwa na mashaka katika ufanyaji kazi wake na hii kupelekea mkulima kupoteza nguvu pamoja na mtaji katika ukulima wake mfano miaka ya nyuma tuliweza kutumia dawa kwa kipimo sahihi na ikafanya kazi iliyokusudiwa Lakin sasa madawa mengi unaweka kwa kuzidisha kipimo na bado yasilete matokeo yaliokusudiwa na kuleta hatari katika kipato na afya ya mlaji kwa namna moja ama nyingine.

Serikali kuweka utaratibu wa upatikanaji wa mbegu bora kwa wingi na kwa wakati kwa kila mkulima, kwa kufanya hivyo kutaondoa shida ya mkulima kujaribu jaribu mbegu ambazo upelekea kupoteza muda na kipato na yote uchangiwa na serikali kutotenga fungu kubwa la bajeti katika upatikanaji wa mbegu mf.mkulima wa hekari tano unampa mfuko moja wa mbegu ya ruzuku ambao auwez kumsaidia chochote katika shughuli zake.

Kutojaribujaribu kutoa mikopo kwa wakulima,kupitia mikopo ya kilimo tumeona serikali ikitoa kiasi kidogo cha mikopo kwa kupitia vikundi na hivyo kumnyima uhuru mkulima wa kukopa kiasi ambacho kitamuwezesha kuendesha shughuli zake kwa uhakika na ikiwezekana kupunguza riba ili awe na uhuru kuliko kumpa mkopo ambao benki ndo itakuwa mnufaika mkuu kuliko mkulima mwenyewe.

Uendesha wa semina kwa kutumia mashamba darasa ikiwezekana kwa kila kijijin ili kumpa ujuzi sahihi na njia sahihi za kuweza kuendesha kilimo kwa tija na ubora uliosahihi hii itamsaidia kujua kila hatua kwa usahihi na umakini.

Elimu ya uhifadhi wa mazao,elimu juu ya uhifadhi wa mazao pia ni muhimu kutolewa kwa wakulima ili kusaidia upatikanaji wa chakula muda wote na upatikanaji wa chakula salama, tumeona uhifadhi mwingi ukipigiwa kelele cha kuangamiza taifa la kesho kwa sumu za uhifadhi wa mazao ambayo usababisha maradhi yasioambukiza kama Kansa na kadharilika. Kwa hiyo serikali iweke nguvu kubwa katika elimu juu ya uhifadhi wa chakula itasaidia upatikanaji na usalama wa chakula kwa watumiaji

Umwagiliaji, tumeona mabadiliko ya tabia nchi yakileta madhara mengi katika kilimo,kwa hiyo umwagiliaji ni mbadala wa mageuzi makubwa katika kilimo cha sasa, ombi langu kwa Serikali isichoke kuweka vyanzo vya umwagiliaji karibu na wakulima hasa hasa vijijin kuliko kuweka mradi wa watu wachache.

Na mwisho kabisa auwezi kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi ikiweka chanzo kimojawapo cha mapato ya serikali inatokana na mageti ya maliasili yaliotapakaa kila vijiji kwa ajili wa kukusanya ushuru wa magunia ya mkaa then unahitaji utunzaji wa vya vya maji ni uongo, tunahitaji kubuni njia nyingine ya mapato na sio kutegemea ukataji wa miti kama kipato. Kwa kafanya hivyo tunaweza kuboresha kilimo na hali ikarudi kama zamani enzi za ukulima bila kutumia nguvu nyingi.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom