SoC01 Kilimo ni nguzo mama kuelekea uchumi wa viwanda

SoC01 Kilimo ni nguzo mama kuelekea uchumi wa viwanda

Stories of Change - 2021 Competition

malunde_mc

Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
9
Reaction score
5
Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba.Kilimo kina maana pana sana inayojumuisha uzalishaji wa mimea,ufugaji wa mifugo pamoja na uvuvi.Tanzania takribani 70% ya wakazi wake hujishughulisha na kilimo.

Zifuatazo ni faida za kilimo.
Kupatikana kwa chakula :-Kilimo kinawezesha kupatikana kwa chakula pale kinapofanywa kwa njia zilizoboreshwa uzalishaji utatosheleza mahitaji cha chakula.Watanzania si wote wakulima wengine wanafanya kazi ofisini na wanaishi mijini hivyo vyakula vinapozalishwa kwa wingi bei inakuwa nzuri na itakayowafanya walaji kuimudu.

Ajira:-Kilimo kimekuwa kikiajiri 70% ya watanzania wenye fani mbalimbali hivyo kuipunguzia serikali tatizo la ajira.
Pato la taifa:-Kilimo kinachagia 40%kwenye pato la taifa hivyo kimekuwa kikisaidia sana kwenye kukuza pato la ndani pamoja na kulipa kodi mazao yanapopelekwa sokoni.

Kukuza viwanda:-Malighafi nyingi zinazozalishwa viwandani kwa kiasi kikubwa vinatokana na kilimo,hivyo kilimo kikiboreshwa na kuweza kutosheleza mahitaji ya viwandani itapelekea bidhaa nyingi kuzalishwa ndani ya nchi yetu.

Kuondoa/kupunguza umasikini:-Umasikini wa nchi pia unaweza kuondolewa /kupunguzwa kupitia kilimo hasa kinapofanywa kwa mikakati na kuzalisha mazao ya kutosheleza mahitaji ya nchi na mengine yakauzwa nje ya nchi ambapo wanaichi watajipatia fedha za kufanyia maendeleo.
Zifuatazo ni njia za kuboresha sekta ya kilimo.
Kutolewa kwa elimu ya kilimo cha kisasa:-Serikali na sekta binafsi zina jukumu la kutoa elimu kwa wakulima ili wasiendelee kutumia zana duni na kulima kwa mazoea badala yake wafundishwe mbinu za kisasa ili wajipatie mazao mengi yenye ubora yatakayowaingizia kipato.

Masoko ya uhakika:-Wakulima wanahitaji masoko ya uhakika watayouzia mazao yao ambapo kwa sasa hakuna masoko ya uhakika na wakulima wanahangaika watauza wapi mazao yao.Serikali ina jukumu la kutafuta masoko yenye wanunuzi wa uhakika kwa bei nzuri.

Serikali kufuta/kupunguza kodi katika pembejeo:-Ili kilimo kiwe na tija na kifanyike kwa ubora kuna haja ya kufuta/kupunguza kodi katika pembejeo hasa mbegu,viuatilifu na mbolea ili zipatikane kwa bei nafuu.Wakulima wengi kwa sasa wanashindwa kumudu bei ya pembejeo na viuatilifu.

Serikali kuanzisha madawati kwenye balozi zetu huko ughaibuni:-Madawati hayo yatakuwa na jukumu la kutafuta masoko ya mazao yetu hii itapelekea nchi kuingiza pesa za kigeni kwa wingi.Ili hili lifanikiwe serikali ina jukumu la kuziagiza balozi zitafute masoko kwa wingi na pengine zishindanishwe.

Hivyo,Kilimo kikiwekewa mikakati madhubuti kitakuwa mwarobaini ama tiba ya tatizo la ajira ambapo kitawafanya vijana na wahitimu wa vyuo nchini kujikita kwenye kilimo .Pia kukiwa na mazingira rafiki katika kilimo itachochea maendelo kwa nchi na wananchi kwa ujumla.

KILIMO NI NGUZO MAMA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom