piry Lasway
Member
- Jul 13, 2021
- 6
- 2
Kilimo ndio uti wa mgongo kwa taifa letu, kwani kupitia kilimo taifa linajitosheleza kwa chakula,pato la taifa linakua, kipato cha jamii na mtu mmoja mmoja kinakua, ajira zinapatikana za kutosha,
Taifa letu ili linufaike zaidi kupitia sekta hii ya kilimo,basi haina budi kuongeza bajeti ya kutosha kwenye wizara ya Kilimo,kusomesha zaidi maafisa kilimo na wawe wa kutosha kuanzia kijiji,tarafa, wilaya,mkoa na kikanda.
MAMBO YATAKAYOFANYA KILIMO CHETU KUWEZE KUINUFAISHA TAIFA LETU NA JAMII KWA UJUMLA NI;
(1) Serikali kupitia wizara ya kilimo iwe inatoa mafunzo kwa wananchi vijijini namna ya kufanya kilimo chenye tija, kwa mazao yote ya chakula na kibiashara.
(2) Kuwe na vipindi vya kwenye redio, runinga na magazeti kwa ajili ya kutoa elimu na mafunzo juu ya kilimo cha kisasa, kilimo chenye tija.
(3) Maafisa kilimo kuendesha mafunzo na warsha mbalimbali kwa wananchi ili waelimike juu ya kilimo chenye tija.
(4) Serikali kupitia sekta za kifedha,kuwawezesha wakulima kupata mikopo ya bei nafuu na isiyo na riba ili kufanya uwekezaji wa kutosha kwenye kilimo,kuanzia wakulima wadogo,wakati na wakubwa.
(5) Mashuleni kuwe na somo la kilimo kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo vya kati na vyuo vikuu, wanafunzi wafundishwe mbinu bora za kilimo cha kisasa,na ata kuwe na mashindano ya kidarasa, kishule, kitarafa, kiwilaya, mkoa, kikanda na kitaifa.
(6) Vijana watakao onyesha upendezi wa kufanya kilimo,basi wasaidiwe na kupelekwa kwenye vyuo vinavyohusiana na kilimo, kusaidiwa mtaji na pembejeo tayari kuanza kilimo, pia serikali wakati huo itafute masoko ya mazao yatakayo zalishwa.
(7) Wananchi wawe wanapewa majarida,vitabu kutoka kwa maafisa kilimo waliopo mikoani, wilayani,tarafani na vijijini, pia waendeshe semina kwa ajili ya mafunzo ya kilimo cha kisasa,pia iandaliwe safari kutembea mashamba makubwa, mashamba darasa na kwenye vyuo ya kilimo kama SUA kupata madokezo toka kwa wakufunzi wa kilimo.
Kufanya hivyo kutachochea ari ya kufanya kilimo na uzalishaji utaongezeka kwa kiasi kikubwa.
Ukuaji wa sekta ya kilimo itaongezeka na kunufaisha jamii na taifa letu kwa ujumla,pia kutapunguza kwa kiasi kikubwa ukosefu wa ajira nchini mwetu.
Ni wajibu wetu kama taifa kwa kushirikiana na wadau wengine kuona namna ya kuboresha kilimo chetu.
Na Priscus Lasway, mawasiliano ni ;
Email ni piryjacob@gmail.com,
Simu namba 0752250938/0624873870.
Asante.

Upvote
1