Kilimo, soko na faida za Uyoga

Mkuu,

Huu uyoga ni organic au? Pia naona watanzania wanakosa utashi au taratibu wa consumption ya uyoga, sijui tatizo ni nini hapa ukiweka mchicha na uyoga mtu achague kama offer niauhakika atachagua uyoga, je ni mazoea au kutokufahamu, uyoga ni mmea au ni fungi?

Panahitajika elimu biashara na marketing ya kutosha uunless othrwise mimi naona ukiweza kuwa na segment ya customers/market ukawalenga watu wa aina fulani inaweza kuwa biashara nzuri.
 

Mkuu ninakubaliana na wewe kabisa, lakini hapo kwenye red nadhani ulimaanisha atachagua mchicha. Ni vyema watu wakajua kuwa sehemu kubwa ya Bara la Afrika, uyoga (edible fungi) ni chanzo kikuu cha chakula chenye protini, lakini baadhi yetu tumelelewa katika jamii iliyotuaminisha kuwa Uyoga ni Sumu. Wakati ninakubaliana na misimamo ya jamii hizo kwa kiasi fulan, napenda kuweka wazi kwa wale wasiojua kuwa si uyoga wa aina zote ni Sumu.

Mimi ni mmoja kati ya watu waliolelewa katika jamii zenye imani hizo, hivyo ninaelewa athari zake katika namna nilivyokuwa naliona zao hili kwa kipindi fulani. Nakumbuka hata baada ya kusoma kwenye masomo ya sayansi kuwa uyoga unaliwa bado sikuwa na nia wala dhamira ya dhati kufikiria kuwa kilimo cha uyoga kinaweza kikafanyika kibiashara na kumkomboa mwananchi wa kawaida .

Ni mpaka mwaka 2010, nilipopata wasaa wa kupata mushroom soup recipe, ndipo mtizamo wangu juu ya zao hili ulibadilika. Hata hivyo nimekuwa mvivu wa kufanya utafiti juu ya kilimo hiki kibiashara mpaka kipindi nilipokutana na wanunuzi wakubwa wanaohitaji zao hili
 

Mkuu

Umeanza kufungua njia

Yes, kama uyoga utaanza kupigiwa debe na tukaona shule zetu zinafundisha ulimaji wa chakula hichi na hata milo ya mashule ikawa na uyoga inaweza kusaidia kuondoa dhana yeyote ile potofu na ku-promote consumption that leads to automatic marketing.
 

Nadhani wengi bado hatutaki kutoka ndani ya box, nakumbuka kuna ndugu zangu niliwaelezea hii kitu kipindi fulani wakabaki wanacheka na kusema wao hawawezi kula UYOGA. Nikawauliza hizo antibiotics mnazokunywa zimetengenezwa na nini? Wakajitetea, nikawauliza ile starter tuliyokunywa kwenye harusi ya ... imetengenezwa na nini? Wakabaki wanashangaa

Mkuu kuna taasisi zimeshaanaza kutoa elimu hii, kama SUA- Morogoro, TIRDO -Msasani Dar es Salaam na Tengeru-Arusha, sema bado elimu haijawafikia wengi.

Hebu angalia jinsi wenzetu wanavyolizungumzia hili zao HAPA

 

Mkuu enteprenure ninamtandao wa wakulima wa uyoga ambao niliwapatia mafunzo mwaka jana na tayari wamekwishaanza uzalishaji. tafadhali naomba unilink na hao wanunuzi ili tuweze kufanya biashara. naomba unipm namba yako ya simu tafadhali0
 

Mkuu kumbe hapo kwenye red sikukujibu. Ndio uyoga huu ni Organic. Halafu hebu angalia hizi ingredients za oyster mushroom uniambie kama nitaweza kuzipata kwenye chakula kingine zaidi ya uyoga

Nutritional Value (per 100 grams) Fresh - Typical Oyster Mushroom

[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 60"]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Calories:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
34.5 g
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Protein::
[/TD]
[TD="width: 47%"]
3.0g
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Fat:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
0.2 g
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Carbohydrate:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
5.8 g
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Crude Fiber:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
0.9 g
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Thiamin:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
0.5 mg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Riboflavin:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
0.5 mg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Niacin:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
10.9 mg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Iron:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
1.5 mg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Sodium:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
83.7 smg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 51%"]
Potassium:
[/TD]
[TD="width: 47%"]
379.0 mg
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Nice staff mimi napendelea sana supu ya uyoga na kwa kweli nitatafuta muda niku pm ili tupate kuwasiliana. Aksante sana kwa maandiko yako.
 
@Enterprenuer=hiyo imekaa vizuri kama kuna m2 practical anaendesha kilimo cha uyoga ani PM ili kufanya mpango wa ku meet niwezeshe kuona jinsi yeye anavyofanya ili iwe rahisi kwangu katika utekelezaji,sabab kuona ni sawa na kusoma mara mbili zaidi.
 
Hii ilikuwa biashara ya marehemu Kawawa pale Madale, sijui kama ilipata mrithi.
 
@Enterprenuer=hiyo imekaa vizuri kama kuna m2 practical anaendesha kilimo cha uyoga ani PM ili kufanya mpango wa ku meet niwezeshe kuona jinsi yeye anavyofanya ili iwe rahisi kwangu katika utekelezaji,sabab kuona ni sawa na kusoma mara mbili zaidi.

Mkuu day24, ukipitia post no.6 kuna mdau anaitwa JBAM, huyu anaweza kuwa na majibu ya kile unachokitaka. Au wasiliana na Hort Tengeru (Arusha) watakuunganisha na mtandao wa wakulima waliofundishwa wakafundishika, na sasa uchumi wa familia zao unategemea zao hilo
 
Hii ilikuwa biashara ya marehemu Kawawa pale Madale, sijui kama ilipata mrithi.
Biashara nyingi za kiafrika zinakosa exit stratergy na succession plan. Sitashangaa kama Mh. alivyotutoka alitutoka na biashara yake. Sasa malila, (just out of curiosity) unaweza ukatuambia soko kubwa la marehemu lilikuwa wapi? Kuna wadau wanaweza waka-fill hiyo gap
 
Kwa wale walio interested na hii biashara kuna grant zinatolewa na Maendeleo Agricultural Enterprise Fund (MAEF). Hii ni project ya FARM AFRICA. Unaweza kuwatembelea HAPA
 
mdau naomba uniPM namba yako, mimi always ni risk taker so nataka nianze hiki kilimo ASAP, nina chumba kidogo tayari kina giza so Haina shida naanza na kidogo kwa kujifunzia, nina shamba kubwa bagamoyo nikiweza hapa nitaukuza mradi huko shambani. Mbegu zinauzwaje? estimation ya gharama za kuanzia ni kama sh ngapi? chumba ninacho kidogo cha mita 2.5m X 2m (ilikuwa store) kitafaa kwa kuanzia? na pia kina tiles haitaleta shida na huo unyevu unaotakiwa?? tafadhali niPM namba yako niko Dar.
 

Mkuu kwa kuwa upo Dar, naomba uwatembelee TIRDO (Msasani)
 
Katika pitapita zangu nikabahatika kukutana na mama akiuza uyoga, nilivutiwa nao na nikaununua kwaajili ya kitoweo nyumbani.

Sasa naomba wenyeujuzi wanisaidie faida za hii kitu kwa binadamu, na kama hasara zipo basi itakuwa kheri nazo mkizitaja hapa, najua niwengi watakaopata faida kwa msaada wenu.

 
They are rich in proteins, so hata kwa mambo flani zinafaa. Mbaya ni kua ipo mingine ina asili ya sumu, siifaham!
Ni hayo tu.
 
Hasara kubwa ya uyoga ni kujua upi unaliwa na upi hauliwi. Kuna uyoga ni sumu na unaweza kudhuru na hata kuua. Lakini ikiwa unauzwa, nadhani muuzaji atakuwa ni mtaalamu wa kujua kile anachofanya.
Aina maarufu ya uyoga unaoliwa ni hii:
Ukiwachia hatari hizo, uyoga una virutubishi kama vile: Vitamins B1, B2, B3, B5 na Vitamin C, Calcium, Phosphorous, Potassium, Sodium na Zinc
 

Huu unafanana na huu wa kwako lakini una sumu mbaya kabisa inahitajika hekima na busara kuchagua uyoga.
Btw, u hali gani?

 
huu unafanana na huu wa kwako lakini una sumu mbaya kabisa........inahitajika hekima na busara kuchagua uyoga.....btw......u hali gani....?
Uyoga mzuri lakini mtihani sana. Tulipokuwa watoto tulikuwa tunajilia tu na Mungu alitulinda. Hivi sasa kama sikuukuta Supermarket, wa kuokota mimi mwenyewe msituni siutaki. Kuna aina hii hatari sana. Wengine wanautumia kama dawa ya kulevya:


Mimi mzima, asante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…