Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Wadau wa kilimo hebu tuseme tunataka nini itufanyie serikali ya awamu ya tano. ni matatizo gani itutatulie na mambo gani ituboreshee? Mimi binafsi nahitaji kilio changu cha kila siku hapa chini kisikilizwe na kufanyiwa kazi.
Vijana na watu wengi hawapendi kulima kwa sababu mbili. Kwanza ni kukosekana kwa masoko ya uhakika wa mazao ya kilimo na bei kuwa ya chini. haya yote yanasababishwa na serikali kuzuia watu kuuza mazao nje ya nchi wakati uzalishaji na potential ya kuzalisha ni kubwa sana.
Ninaweza sema Tanzani kuna deflation ya bei ya chakula. Deflation ina madhara yake, kwanza inapunguza uzalishaji na kusababisha unemployment. Deflation ya chakula inanufaisha wachache na kuumiza wakulima ambao ndiyo wengi. Imekuwa nafuu kununua kuliko kulima. Hii inamaanisha wakulima huzalisha kwa hasara.
Je ni kweli kufungua mipaka kutaleta njaa?. Nchi yetu inazalisha ziada ya msosi pia naamini inaweza kuzalisha hata mara mia ya kiwango cha sasa kwa ardhi na maji tuliyo nayo. Hivyo kufungua mipaka kutaongeza uwekezaji kwenye kilimo, kutaongeza uzalishaji na matokeo yake ajira kuongezeka. Pia vijana wengi wataanza kujiajiri na kilimo maana kitakuwa kinalipa.
Sasa kwanini wanazuia? Kama tunavyojua mabadiliko ya kisiasa huanziaga mijini. Serikali kwa kuona hilo huamua kuwapumbaza watu wa mjini kwa kuhakikisha bei ya chakula ipo chini na njia moja ni kufunga mipaka. Wanafanya hivyo kwa expense ya 80% ya watanzania. Hata hivyo watu wengiwamjini pia hulima au wangependa kuwekeza kwenye kilimo. So hii strategy inatutafuna sote.
Ili kukabiliana na ajira serikali inatakiwa iruhusu uuzaji wa mazao nje, itatengeneza ajira nyingi sana. Na siyo kufungua kinafiki. Kufungua harafu kuweka kodi ya kuexport kubwa ili kudiscourage watu.