Kilimo User Guide

KXY

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2011
Posts
885
Reaction score
341
Habari zenu Wajasiriamali!

Leo nimekuja na wazo la kutengeneza muongozo wa mkulima(user guide). Wazo hili limekuja baada ya mimi banafsi kunufaika na maelezo (nondo) yanayotolewa humu kuhusu ujasiriamali kwa ujumla. Lengo kuu ni kutoa summary ya vitu vingi ambavyo vishaelezewa humu na kupunguza maswali ya kujirudua rudia wakati vitu vimeshaelezewa kwenye jukwaa.

Mi natoa mfano(template) na wadau mtachangia mawazo yenu:

Zao:

Mahali linapostawi:
jiografia ya sehemu na mifano

Mbegu: Aina za mbegu na gharama zake (au miche)

Kupanda: nafasi kati ya mmea na mmea (spacing)

Palizi: mara ngapi na baada ya mda gani shamba lisafishwe

Mavuno: baada ya mda gani na mara ngapi

Gharama: makadirio ya gharama kwa eka 1 na mchanganua kwa kifupi

Mapato: makadirio ya mapato kwa eka 1

Maelezo ya ziada: maelezo ya kutoa picha halisi ya kilimo cha zao husika, changamoto n.k


Nawakaribisha tujadili:

Useful links:
Biashara ya Miti
Ushauri kilimo na ufugaji
Mtaji 10 Million
 
Source: Tanzania Tree Seed AgencyMgawanyiko wa kanda za hali ya hewa Tanzania kwa ajili ya kupanda miti ya aina mbalimbali:

[TABLE="width: 445, align: center"]
[TR]
[TH]Kanda za hali ya hewa (Climatic zones)
[/TH]
[TH]Maelezo
[/TH]
[TH]Mifano
[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]1
Maeneo ya miinuko yenye unyevunyevu (wet montane)
[/TD]
[TD]Safu za milima zaidi ya mita 1,800 juu ya usawa wa bahari na mwanzo wa ukanda wa theluji, ambapo kuna mvua nyingi isiyopungua milimita 1000 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 13°C. Kuna ukungu na mawingu mara kwa mara.
[/TD]
[TD]Lushoto, Magamba, Narok, Ngorongoro, Mufindi, Tukuyu n.k
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]2
Maeneo ya miinuko yenye ukame (Dry montane)
[/TD]
[TD]Maeneo ya milima kati ya mita 1800 na 1,500 juu ya usawa wa bahari na mwanzo wa ukanda wa theluji ambapo kwa kawaida mvua si chini ya milimita 760 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 15°C
[/TD]
[TD]Shume Njombe, Iringa, West Kilimanjaro Meru kaskazini, Hanang n.k
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]3
Maeneo ya miinuko ya wastani (Transitional montane)
[/TD]
[TD]Maeneo ya milima kati ya mita 1,500 juu ya usawa wa bahari na mwanzo wa ukanda wa theluji yenye hali ya hewa kati ya kanda (1) na (2).
[/TD]
[TD]Sungwi, Olmotonyi, Rongai, Mbulu, Mbeya n.k.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]4
Nyanda za juu zenye unyevunyevu (Moist plateau)
[/TD]
[TD]Maeneo kati ya mita 600 na mita 1,200 juu ya usawa wa bahari yenye mvua kati ya milimita 760 na 1,400 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 15°C
[/TD]
[TD]Geita, Mpanda, Tabora, Kigoma, Moshi n.k.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]5
Nyanda za juu zenye ukame (Dry tropical)
[/TD]
[TD]Maeneo kati ya mita 600 na 1,200 yenye mvua chini ya mm 760 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 18°C.
[/TD]
[TD]Dodoma, Itigi, Shinyanga, Mwanza, Tabora n.k.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]6
Maeneo ya hali ya joto na unyevunyevu (Wet tropical)
[/TD]
[TD]Maeneo maalum katika mwambao wa pwani chini ya milima yenye mvua nyingi, na maeneo ya tambarare yaliyoko mashariki mwa baadhi ya milima. Mvua milimita 1,140 au zaidi kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 18°C
[/TD]
[TD]Rau, Turiani, Matombo, Minziro, Ukerewe, Korogwe, Muheza n.k.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]7
Mwambao wa pwani (coastal belt)
[/TD]
[TD]Ukanda wa pwani chini ya mita 600 juu ya usawa wa bahari. Sehemu zingine huingia bara hadi kilomita 300. Mvua kwa kawaida ni milimita 760 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha joto ni 18°C
[/TD]
[TD]Dar es salaam, Kibaha, Bagamoyo, Lindi, Mtwara Ifakara.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…