SoC03 Kilimo - Ustawi wa Taifa letu

Stories of Change - 2023 Competition

COSPHECASO

New Member
Joined
Oct 22, 2018
Posts
1
Reaction score
1
Kilimo ni sekta muhimu katika kukuza na kuendeleza ustawi wa Taifa letu. Kwa Sasa kilimo kinaajiri siyo chini ya 60% ya watanzania na inachangia sii zaidi ya 30% ya pato la Taifa.

Kundi kubwa la wakulima wanaishi vijijini pia hawa ni vijana na wanawake wasio na mitaji.

Wakulima hawa wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo (1). Magonjwa ya mazao shambani mpaka magharani (2). Zana duni (3). Ukosefu wa masoko ya uhakika ya ndani na nje (4). Ukosefu wa mitaji (5). Gharama kubwa ya viuatilifu (6). Sera zisizowalinda wakulima dhidi ya mazingira mabaya ya kimazingira(mfano mafuriko) na kiuzalishaji(mfano madarari wa mazao).

Changamoto za wakulima ni nyingi sana na ni pana sana. Mimi kwa mtazamo wangu ninaona kua mambo yafuatayo hapa chini yakizingatiwa yataboresha sekta ya kilimo kwa ujumla pamoja na kuleta uwajibiaji wa kila mmoja katika mnyororo wa thamani.

1). Elimu kwa wakulima na wote wanaohusika katika mnyororo wa thamani lazima izingatiwe na iwe kipaumbele kwa ajili ya maboresho ya kudumu kwenye sekta ya kilimo.
Tunashukuru serikali imeanza kuliona na kulitekeleza eneo hili kwa kuwapa mafunzo vijana katika vyuo atamizi ambayo hii itageuza mtazamo mzima wa jamii kuhusu kilimo. Itawafanya vijana na wote watakaokua wamepata mafunzo hayo kuwajibika na kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Kupitia elimu wakulima wataweza kugeuza mitazamo yao na itawasaidia hata namna zao za kufikiri kuhusu kilimo.

2). Mitaji/ruzuku zitolewe kwa wakulima waliopewa elimu ya kilimo. Mitaji hii lazima ilenge kuleta mapinduzi ya zana bora za kilimo pamoja na viuatilifu bila kusahau kulima bila kutegemea mvua.

Kwa kua matarajio ni kua vijana hawa watakuwa wamefundishwa kulima kibiashara, basi vijana/wakulima hawa watakua na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi katika kuchagua aina ya mazao yanayoendana na uhitaji wa soko pamoja na namna ya kuyaongezea mazao ubora ili yasipotee kwa kuharibika baada ya kuvunwa.

Aidha msisitizo lazima uwe ni kuzalisha na ziada. Kwa kua lazima kaya au kiundi cha wakulima kiwe na uhakika wa kushiba kwanza ndipo watakapoweza kuwaza kuhusu kuuza ziada.

3). Maboresho ya sera zitakazowalinda wakulima pamoja na wote wanaohusika katika mnyororo wa thamani. Tunahitaji sera ambazo zitawalinda wakulima dhidi ya wezi/walanguzi wa mazao ya wakulima ambao wao huwalipa wakulima bei ndogo kisa wao kwenda kupata bei kubwa sokoni.

Wakulima walindwe dhidi ya majanga ya asili kwa kuwafidia au kuwakatia bima za mazao yao pale yanapokua yamekumbwa na majanga ya asili kama mafuriko au ukame. Kwenye hili la fidia tumeshuhudia Serikali iliwahi kufanya wakati ule wa kiangazi kikali kwa wafugaji wa Kiteto na kwingineko. Lakini pia kuhusu bima serikali imewezesha baadhi ya benki zinatoa huduma ya bima ya mazo japokua bado uelewa ni mdogo kwa wakulima.

Pia wakulima wanapaswa kulindwa dhidi ya migogoro ya Ardhi. Japo serikali na taasisi zake wanaendelea kuwajibika juu ya hili hasa kwa maeneo ya hifadhi yaliyokua na migogoro ya aridhi ya muda mrefu na wakulima/ wananchi. Baadhi walihamishwa na baadhi wamemegewa maeneo ya hifadhi hizo.

Aidha kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake ili kuhakikisha kilimo kinaongeza mchango wake katika pato la taifa.

Nawasilisha. Wasalaamu.
 
Upvote 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…