SoC02 Kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

Philbert Meshack

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
4
Reaction score
3
Kilimo ni shughuli ya kibinadamu inayojumuisha uzalishaji wa mimea na ufugaji wa wanyama. Miongoni mwa mazao ya chakula yanayolimwa ni pamoja na mahindi, ndizi, maharage, mihogo, mtama, uwele, njegere, choroko, karanga na viazi. Mazao ya biashara yanayolimwa ni pamoja na karafuu, pamba, alizeti, kahawa, chai na katani. Pia wanyama mbalimbali kama vile ng'ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku na bata hufugwa. Hapa nchni jamii zote zinajihusisha na kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara. Pia jamii nyingine zinajihusisha na ufugaji kwa kiwango kikubwa sana. Makabila yanayoongoza kwa ufugaji wa wanyama mbalimbali kama vile ng'ombe, mbuzi na kondoo hapa nchini ni pamoja na Wamasai na Wasukuma.

Nchini Tanzania sekta ya kilimo ni muhimilili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi kikubwa cha pato la taifa, robo tatu ya bidhaa mbalimbali zinazouzwa nje ya nchi yetu zinatokana na kilimo. Pia kilimo ni chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira kwa zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania. Tanzania inazalisha takribani 97% ya chakula ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemeana na kiasi cha mvua kilichopatikana.

Kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya kilimo nchini Tanzania. Changamoto hizo ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanasababisha kutokea kwa mafuriko na ukame. Pia matumizi ya zana duni za kilimo ambayo husababisha kupatikana kwa mavuno kidogo nayo ni changamoto pia. Uwepo wa magonjwa mbalimbali ya wanyama na mimea pia ni miongoni mwa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hii. Magonjwa ya kitropiki kama vile malaria na mafua hudoofisha afya za wakulima wengi sana hasa kwa wale wanaoishi mbali na vituo vya afya. Changamoto hizi kuwaathiri Watanzania kwa kusababisha ongezeko la wimbi kubwa la ukosefu wa ajira, umaskini na utapiamlo.

Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa kwa sababu asilimia kubwa ya Watanzania wamejikita kwenye kilimo. Ili kuboresha na kuimarisha kilimo na ufugaji nchini Tanzania hatuna budi kufanya yafuatayo;

Elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima. Nguvu ya kutosha inatakiwa kuwekwa ili kuwawezesha wakazi wa mijini na vijijini wanapata fursa ya kupata elimu muhimu kuhusu kilimo na ufugaji. Hii itawarahisishia kujua njia bora na za kisasa za kuongeza uzalishaji wa mazao. Pia wanaweza kuendelea kupata mafunzo kutoka kwa maafisa wa kilimo na kwa kuhudhuria semina mbalimbali za kilimo. Hii itawasaidia sana wakulima wengi wadogo wadogo kwa wakubwa kuweza kupata mafunzo yatakayowawezesha kuimarisha kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na biashara kwa ujumla.

Wakulima wapatiwe mikopo yenye riba nafuu. Wakulima wengi wanakumbana na matatizo ya upungufu au ukosefu wa mtaji na umaskini. Baadhi wana mitaji midogo midogo ya kuendesha shughuli za kilimo. Wengine hawana kabisa. Wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo watu binafsi, mashirika yasio ya kiserikali na serikali kwa ujumla wanatakiwa kutoa mikopo nafuu kwa wakulima mbalimbali ili kuwawezesha kuendesha shughuli zao za kilimo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Wakulima wawezeshwe zana bora na za kisasa za kilimo. Kuwapa wakulima zana bora za kilimo kama vile matumizi ya trekta, mbolea na mbegu bora za kisasa inaweza ikawa suluhisho la upungufu wa chakula miongoni mwa wakulima. Hii ni muhimu kwa sababu wakulima wengi sana bado wanatumia zana duni za kilimo kama vile jembe la mkono na panga.

Wakulima wanatakiwa kujiunga na vyama vya ushirika. Wakulima wanatakiwa kuungana pamoja ili kuanzisha vikundi mbalimbali vya ushirika kwa sababu hii itawasaidia na kuwawezesha kupata mikopo , mbegu bora za kisasa, zana bora za kisasa za kilimo na mafunzo. Pia itawasaidia kupata ujuzi kutoka kwa mtu mmoja mmoja kwenda kwa mwingine kwenye chama.

Kuimarisha na kuboresha masoko ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na kilimo na ufugaji. Serikali na wadau wengine wa kilimo wanatakiwa kuandaa na kuboresha masoko ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na kilimo na ufugaji ili kuboresha maisha ya wakulima na wafugaji wengi kwa kuweka bei inayostahili. Hii itawasaidia wakulima na wafugaji wengi kujipatia kipato zaidi kwa sababu watakuwa na uhakika wa kuuza bidhaa zao sokoni kwa bei stahiki.

Wakulima wanatakiwa kuongeza na kupanua mashamba. Ni kweli kabisa kwamba wakulima wengi nchini Tanzania wanajihusisha na kilimo cha mashamba madogo madogo. Kwa hali hii ni dhahiri kwamba hawawezi kupata mazao mengi kwa ajili ya chakula na kuuza. Wakulima wanatakiwa waachane na kilimo cha mashamba madogo madogo na badala yake wajikite kwenye kilimo cha mashamba makubwa makubwa ili waweze kupata mazao ya kutosha kwa ajili ya chakula na biashara kwa ujumla.

Kilimo cha umwagiliaji kihamasishwe miongoni mwa wakulima wengi nchini. Nchi yetu ina rasilimali nyingi sana ikiwemo maji (mito, mabwawa, maziwa na bahari ya Hindi). Kwa hali hii ni dhahiri kwamba kilimo cha umwagiliaji kinawezekana hususani majira ya kiangazi au kwenye sehemu ambazo hazipati mvua za kutosha. Kilimo cha umwagiliaji kinasababisha upatikanaji wa chakula katika kipindi chote cha mwaka kwa sababu wakulima anaweza kuendelea kuzalisha mazao mbalimbali hata wakati wa kiangazi.

Serikali inatakiwa kuboresha miundombinu ya barabara na huduma za maji maeneo yanayozunguka mashamba mbalimbali ya wakulima. Miongoni mwa matatizo yanayoikumba sekta ya kilimo nchini Tanzania ni pamoja na ubovu au kutokuwepo kwa miundombinu ya umeme, maji na barabara maeneo ambapo mazao mbalimbali yanapolimwa.

Hakuna barabara za kuunganisha maeneo ya mashambani na mijini ambapo mazao mbalimbali yanatakiwa kusafirishwa kwenda kuuzwa. Kuna barabara duni ambazo hazipitiki hususani kipindi cha masika. Hali hii husababisha mazao mbalimbali kuharibika yakiwa shambani. Pia hali hii husababisha wakulima wengi kuuza mazao yao kwa bei ndogo isiyowanufaisha. Serikali inatakiwa kuwajali wakulima kwa kuboresha huduma za maji na barabara imara maeneo yanayozunguka mashamba yao.

Kwa kuzingatia hayo yote tunaweza kuboresha na kukuza sekta ya kilimo nchini na kuifanya iwe miongoni mwa nguzo muhimu katika kujenga uchumi imara kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Imeandaliwa na Filbert Majaliwa
0692766916, 0657513171
 
Upvote 6
Mkuu Uzi wako ni mzuri lakn ni wachache wanaofatilia madini Kama haya,Mimi ni mkeleketwa wa KILIMO
 
Ndugu mleta mada, wakulima Wana changamoto zifuatazo:
1. Wazalishaji wa mbegu chotara (F1) hawajawafikia wakulima wengi hasa wa mbogamboga. Hata wakiwafikia, wakulima hawana uwezo wa kununua mbegu hizo.
2. Kuhusu vikundi ni kwamba mbinu hii haifai maana wakulima wanaangushiwa risk zote ambazo mwisho wa siku humfaidisha mfanyabiashara wa pembejeo
3. Wataalam wa kilimo wa Serikali wanafanyishwa shughuli tofauti na taaluma yao.leo utakuta wanakusanya ushuru kwenye barriers, kesho yuko kwenye sensa, n.k. kingine ni kwamba hawapewi mafunzo ya kuji-update. Kwenye hili ni bora serikali ikaribishe maafisa ugani wa kujitegemea
4. Kuna hawa watu wanaojiita wafugaji. Wanaamini kila kinachoota kwenye ardhi ni malisho. Hili limedumu kwa miaka lakini sioni wafugaji bado wanatamba.
5. Kuna huu ugonjwa wa kuzuia mazao yasiuzwe nje ya nchi, wengine wanasema mkulima asiuze mahindi ya kuchoma bila kujua kwamba kilimo ni biashara kama biashara nyingine yenye kufuata kanuni ya ingiza mzigo toa mzigo.
Naishia hapa kwa sasa
 
Asante sana kwa taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…