Christina samamba
Member
- Jul 22, 2022
- 20
- 38
Usonji ni tatizo la kinafsi na la kihisia linalowatokea watu wengi tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na watu wengine .kifupi watu wenye usonji hawana uwezo mnzuri katika swala zima la mawasiliano.
Usonji ni tatizo linalojitokeza mapema utotoni ambapo mtoto huwa na upungufu fulani kulinganisha na watoto wa kawaida kama vile kupenda kujitenga na watu kuwa na matatizo ya lugha na shida ya kuwasiliana na wengine .
Mtoto pia huweza kuwa na tabia ya kurudia kitu anachokifanya kama vile kupenda kukaa kwenye kiti kilekile mzazi anaweza kugundua kama mwanae ana tatizo hili anapofikisha umri wa miaka miwili ,chanzo halisi cha usonji hakujulikana ingawa matatizo ya kijenotiki (Neurodevelopmental disorder)uhusishwa na tatizo hilo pamoja na kurithi mtaalamu wa tiba Kwa vitendo.
Idara ya magonjwa na Afya ya akili katika hospitali ya taifa muhimbili (MNH) Godfrey Kimati ambaye yuko katika kitengo cha Afya ya akili kwa watoto ,anasema "watoto hawa ni muhimu kupelekwa hospitalini kupatiwa matibabu na pia kupata elimu kama ilivyo kwa watoto wengine".
Kuwa hudumia watoto watoto wenye usonji ni gharama kwani wengine wakihudumiwa angalau viungo vyao viwe sawa kupitia huduma kutoka madaktari bingwa (Specialists) na si wazazi wote wanaweza kumudu gharama hizo hususani watu wenye kipato cha chini ndiyo maana wakati mwingine wazazi hujikuta wakiwafungia watoto ndani kukwepa gharama hizi.
Afadhali kidogo upande wa mjini ambapo watu wanauelewa wakutosha na hata shule pia zipo mfano Dar es salaam shule ziko mbili msimbazi mseto na Mbuyuni Arusha ,morogoro na Geita
Ila hali ni tofauti kidogo Kwa vijijini kutokana na ukosefu wa shule watu wenye usonji kijijini wanakosa nafasi ya kupata elimu na wazazi wengu huwaficha watoto wao majumbani Kwa kuhofia kuchekwa na hata kuona aibu kuwa na watoto wa namna hiyo.
Mfano wa "kisa cha kubuni cha binti furaha ".Binti furaha alizaliwa katika familia ya mzee Matata ,Binti furaha ni mtoto pekee kwa mzee matata na mama furaha ila furaha alizaliwa akiwa na usonji (Autism).
Maisha yake yote binti furaha Alikuwa akifungiwa ndani siku zote hakupatiwa nafasi ya kuchangamana na watoto wenzie hali iliyopelekea tatizo hilo la usonji kuzidi kuwa kubwa zaidi.
Binti furaha alipofikisha miaka 6 mama yake alijitahidi kumshawishi mumewe ili waweze kumpatia nafasi binti furaha ya kwenda kujiunga na wenzie shuleni.
"Mume wangu unaonaje mtoto wetu sasa tukampeleka shule ili aweze kupata nafasi ya kupata elimu kama watoto wengine "Suala hili lilikuwa gumu sana kwamzee matata "Hivi mama furaha una akili wewe huyu mtoto ni mlemavu tena bora angekuwa mlemavu wa macho ,miguu au kiungo chochote kile ila mtoto wako ni mlemavu wa akili ."Lakini mume wangu binti yangu furaha si chizi wala punguani kusema haelewi chochote nimejaribu kuwa naye karibu nimegundua binti yangu anauwezo mkubwa tu kama watoto wengine.
Mzee matata alicheka sana "ahahaaahaaa sawa mama furaha fanya unavyoona inafaa" ,Baada ya ruhusa ya mzee matata akajaribu kumchukua binti yake na kwenda naye katika shule ya msingi mito mipana iliyokaribu na Nyumbani akiwa njiani kuelekea shule watu wengi walimshangaa binti furaha na wengine walisikika wakisema" hee!
Kumbe yule binti wa mzee matata khee watu wachawi nyie kwahiyo wameamua kumfanya mtoto ndondocha ili kufanikiwa ndiyo maana kila miaka wao wanakuwa wanapata mavuno manzuri na wateja wakutosha kumbe sababu ndiyo hiyo.khee dunia hadaa Kweli".
Mama furaha baada ya kufika shuleni anakutana na mwalimu mkuu na kuzungumza naye kuhusu swala la binti furaha kuanza shule pale,"Mama furaha ni wazo nzuri la kutaka binti yako kuanza shule sema hapa shuleni kwetu hakuna miundombinu rafiki ya kumuwezesha binti furaha kuweza kupata huduma ya elimu .
Pia hatuna walimu waliobobea katika kuwapatia mafunzo watoto wenye usonji ,Ningetamani kumpatia nafasi binti furaha sema mazingira siyo rafiki kwake".
"Mwalimu Kwahiyo inamaana elimu Kwa upande wa binti yangu haitawezekana kijiji chetu cha mlima mrefu hakuna kabisa kitengo maalumu Kwa upande wa shule mpaka mjini na mjini ni mbali na nyumbani na inahitajika uangalizi wa kutosha kwake .
Kwani hili serikali hawalioni watoto wetu wenye usonji wanakosa nafasi ya kupata elimu kama watoto wengine kutokana na miundombinu hafifu na uhaba walimu waliobobea kwenye kuwasaidia watoto hawa" .
Mama furaha alirudi nyumbani kwake na binti yake na suala la elimu kwa upande wa binti furaha likaishia hapo miaka ilipita.
Binti furaha alizidi kuwa mkubwa na kufikisha miaka 20. Kijana utu mtoto wa mzee Katazo ambaye alikuwa masomoni mjini akisomea udaktari alirudi Nyumbani kwao kijiji cha mlima mrefu,Siku moja alipita kwenye Nyumba ya mzee matata na kumkuta binti furaha akirudishwa ndani baada ya kutoka nje ,"furaha mwanangu mbona unapenda kunisumbua hivyo mama yako,"shikamoo mama kijana utu alimsalimu mama furaha marahaba mwanangu umerudi lini?
Kutoka masomoni" muda kidogo mama "mbona kama unalalamika kwani kwani ndugu yangu furaha ana shida gani?
Yaani mwanangu ni msumbufu tu huyu mtoto wee acha tu".
"Mama hivi furaha ameishia kiwango gani cha elimu ?"Mama furaha kwa mshangao na huzuni "mh baba yangu furaha hakupata nafasi ya kupata elimu kabisa.maana hakuna shule kwaajili yao hapa kijijini".
Kijana utu alitafakari sana namna ya kumsaidia binti furaha ili aweze kupata nafasi ya kusoma kama binti wengine.
Kijana utu alipata nafasi ya kazi kwenye hospitali kubwa ya mjini hivyo alihitaji kuondoka na kwenda mjini ,"mama na baba kabla sijaenda mjini ningependa nipate kuoa mke kutoka hapa kijijini kwetu" wazazi walikubali,wazazi walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kumjua binti huyo .
"Ni nani binti huyo ? "Mzee katazo aliuliza ,wazazi wangu ni binti furaha wazazi wote walishituka "haiwezekani kabisaa mabinti wote kijijini Unataka kuoa binti asiyeeleweka binti chizi siyo chizi haeleweki kabisa".
"Baba mimi sijali chochote kile mnachozungumza yule binti ndiyo chaguo langu", kijana utu nia ya kutaka kumuoa binti furaha ni kutaka kumsaidia kutoka kwenye kifungo cha mila potofu na giza nene la ukosefu wa elimu lililowafunika wanakijiji cha mlima mrefu.
Taarifa hii ilipopelekwa mama furaha alishangaa sana "hapana haiwezekani kijana utu Mwenye elimu yake ya kutosha kutaka kumuoa mtoto wangu mimi?,Mzee matata upande wake ilikuwa tofauti kidogo unakataa nini sasa huoni anatupunguzia mzigo maana binti furaha alikuwa mzigo mnzito kwangu anasababisha nashindwa kuendelea kwasababu yake bora aolewe tu".
Maneno haya yalimkera sana mama furaha "Binti yangu si mzigo kamwe huyu ni mtoto wangu mimi Ni lini alikufanya ushindwe kufanya kazi zako wakati hukuwahi kumuona kama mtoto mbele ya macho yako" .
kijana utu akizungumza mbele ya wazazi wote wa pande zote Kwa uchungu "Hivi ni nani aliyewambia mtu mwenye usonji ni mtu mlemavu kiasi kikubwa cha kufanya mbague na kushindwa kumpa haki zake za msingi ,sasa ifike wakati ubaguzi na manyanyaso kwa watu wenye usonji yafike mwisho .
"Binti furaha ni mwanamke ninaye mpenda nitamuoa yeye na si vingenevyo" .Hivyo kijana utu alimuoa binti furaha na kwenda naye mjini akampatia nafasi ya kupata mafunzo ya ushonaji wa unguo hivyo aliweza kujiajili mwenyewe hakuna aliyeamini haya upande wa kijiji cha mlima mrefu mafanikio ya binti furaha yalikuwa chachu ya mabadiliko Kwa watu wa kijijini .
Mwalimu mkuu alihamasisha uwepo wa kitengo maalumu cha watu wenye usonji shuleni kwake.
watu wanaoishi na usonji wanakutana na changamoto nyingi sana licha ya kubaguliwa wakati mwingine wanakosa haki zao za msingi kama ya kupata elimu na kupendwa na hata wakati mwingine watu wanaamini watu wenye usonji hawafai kuoa au kuolewa ,kitu ambacho si sawa kabisa .
Changamoto nyingine kubwa zaidi ni kuwa hakuna shule za kutosha au vyuo vya mafunzo kwaajili ya kuwasaidia watu hawa wa usonji pia walimu ni wachache sana waliobobea katika kuwafunza watu wenye shida ya usonji
Hivyo inahitajika jitihada ya kutoa elimu zaidi kwa watu wote sio kujikita zaidi mjini kuliko kijijini,kunahitajika usambazaji wa huduma ya elimu kwa kujenga vyuo vya mafunzo na kuongeza vitengo maalumu mashuleni kwaajili yao.

Upvote
10