Kilio cha haki!

malenga mwitu

New Member
Joined
Dec 10, 2011
Posts
3
Reaction score
3
Nawaomba members wapenzi wa kiswahili na sanaa ya ushairi tubalidishane maoni na baadhi tungo za kishairi ili kuboresha lugha na kuinua hadhi yake. naomba nipeni maoni yenu kuhusu "kilio changu cha haki" ni mtungo niliotunga nikimtafuta kimwana mwenye maadili na tayari kupenda ili nimpe penzi langu lote.(mimi ni mwanachama mpya) ahsanteni wanachama.

PENZI LA DHATI
Bisimillahi Rabuka, illahi Mola muweza,
Bayana nalalamika, upweke menilemaza,
Jamani nahuzunika, nani tanituliza?
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Asiwe mwenye papara, ninachelea chiriku,
Kimwana wa hapa bara, mgeni nitamshuku,
Kidosho mwenye busara, asokuwa zumbukuku,
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Ninamsaka tabibu, alo na mwingi mahaba,
Yangu roho aitibu, kwa mapenzi yaso haba,
Awe wa kwangu swahibu, upweke umenikaba,
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Awe na bora umbile, na twabia adilifu,
Mtoto mwenye sumile, mwenye haiba faafu,
Nitalivaa penzile, shingoni lau mkufu,
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Nitamtwika jukumu, yangu roho kutuliza,
Ashike hino hatamu, bongoni kuniliwaza,
Maneno yake matamu, upweke kuifukiza,
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Awe na mwingi heshima, kwa wadogo na wakubwa,
Kimwana mwenye hekima, asiyetokwa ubwabwa,
Alo tayari kwa dhima, kutenda yalo makubwa,
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Atanituza Rabana, kipenzi cha moyo wangu,
Matoni nikimuona, yatanitoka matungu,
Hakika tutapendana, malaika ua langu,
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Kaditama wa tamati, kalamu ninailaza,
Wazo langu siliati, narudia kutangaza,
Khaherini mabenati, dhima hino mewatweza,
Namtafuta kisura, mwenye penzi la hakika.

Solomon ole Musere
'Malenga mwitu'
Chuo kikuu cha Kenyatta.
 
UMEMPATA!(JIBU)

Hapa kwetu wamejaa, warembo wa kuvutia
wenye sura za kufaa, hutojuta kuwaoa
Ni wengi kila mtaa,Kazi kwako kuchagua
Umempata kisura, mwenye penzi ulotaka

Mimi kwako ni mwenyeji, ngoja nikuchagulie
ni mwanamke mweledi, mwenyewe ufurahie
Wema sepetu stadi, Mchague akulee
Umempata kisura, mwenye penzi ulotaka
 

Gazeti Umenifurahisha sana aisee we KIBOKO duuh.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…