KERO Kilio cha Mwalimu Kuhusu Kutohamishiwa Taarifa za Kiutumishi kwa Zaidi ya Mwaka Mmoja

KERO Kilio cha Mwalimu Kuhusu Kutohamishiwa Taarifa za Kiutumishi kwa Zaidi ya Mwaka Mmoja

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari Wanajamii,
Ninaandika kwa uchungu kielezea changamoto ninayoipiia sasa ya KUTOHAMISHIWA TAARIFA ZANGU ZA KIUTUMISHI KATIKA HALMASHAURI YANGU MPYA pamoja na ukweli kwamba nilihama kutoka halmashauri yangu ya zamani mwanzoni mwa mwaka jana.

Nimelifuatilia suala kwa muda mrefu bila mafanikio. Afisa Utumishi katika halmashauri yangu ya zamani amekuwa na jibu moja tu kuwa yeye alikwishapeleka taarifa OR-TAMISEMI na kwamba mamlaka hiyo ndiyo inayohusika kwa sasa.

Jambo linaloacha maswali mengi ni kitendo cha watumishi wengine waliopata uhamisho nyuma yangu kuhamishiwa taarifa zao za kiutumishi wakati tuliotangulia bado. Na changamoto hii inaonekana kuwa kubwa kwa waliohama kutoka mkoa wa Tanga kwa sababu siko peke yangu ninayepitia changamoto hii. Maana tuliohama nao kutoka mikoa mingine wao wamekwisha hamishishiwa taarifa zao ikiwemo niliyebadilishana naye.

Jambo hili la kutohamishiwa taarifa zangu za kiutumishi limekuwa likinisababishia baadhi ya changamoto zikiwemo kushindwa kutambulika katika mifumo mbalimbali katika halmashauri yangu mpya na hivyo kukosa baadhi ya fursa.

Naomba ushauri wenu juu ya namna bora ya kushughulikia changamoto hii bila kuathiri majukumu yangu.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom