Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 13,864
- 35,079
Ukiangalia kwa jicho la ndani utaona kuna mawazo kinzani juu ya hili swala la utekaji.
Serikali inasema hilo jambo halipo na watu wanajifanyisha tu maigizo ila utekaji haupo. Rejea kauli ya Rais.
Ukija bungeni spika anazuia jambo hili lisijadiliwe bungeni hata kinafiki tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite.
Unazuiaje mjadala muhimu kama huu kujadiliwa wakati ni jambo linalohusu usalama wa wananchi wako? Walipa kodi wako?
Ukija kwa polisi na vyombo vya dola hawa ndio wananyooshewa vidole na wananchi kama wahusika wakuu wa biashara hii haramu ya kutekana.
Jambo la ajabu ni kwamba utekaji upo na watekwaji wapo tena wengine wanawataja wazi kama dola ndio imehusika na madhila waliyoyapata.
Rai yangu kwa serikali isifanye kama mbuni afanyavyo kujificha kichwa kwenye mchanga akidhani haonekani ilhali mwili mzima uko nje. Serikali kuzuia mjadala huu au kuubeza sio sawa.
Tukae tukijua cheche zilichoma msitu mkubwa! Je, bado Tanzania ni kisiwa cha amani kama tunavyojinasibu?