illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Kweli jamani kila mtu anatakiwa atafute riziki kihalali, ila vitu vingine vinaudhi, vinaumiza, niliamua kuwa mkulima kwa lengo la kujiongezea kipato, nikaamua kushirikiana na mzazi wangu aliyeko huko kijijini, tulianza kilimo cha viazi kwa kuanzia nilianza na hekari tano. Baada kulima kwa muda, mazao yakawa tayari kwa ajili ya kuvuna, wakulima wenzetu walituambia kwamba tusipate tabu ya kuvuna kwani kuna madalali huwa wanakuja wanachagua kisha wanaleta wateja ambao huvuna wenyewe.
Nikaona ni Jambo la kheri tuliwasiliana na dalali ambaye alituahidi siku ya kuja na wakulima wote tukawa tunamsubiri, mara nikaona kigari aina ya Paso kinakuja shambani kimeandikwa “wajinga ndio waliwao” akashuka pande la mtu suruali amevalia tumboni, tukatambulishwa kuwa jamaa ndiye dalali wakulima akiwemo mzazi wangu wanamnyenyekea utadhani nini sijui, kumbe yule bwana jukumu lake kukagua mazao shambani kisha anapanga bei, na ukitofautiana naye utapata wakati mgumu kuuza mazao yako kwani atawaeleza madalali wengine pia kwani wana mtandao.
Jamaa alikuja kwenye shamba letu wakati tunasubiri “ofa” jamaa akachukua panga na kuanza kufukua huku akisema “hamna kitu hapa chelema Tupu hizi, hapa labda niwape laki nane” nikamwambia hiyo hailipi akasema kama hailipi, hakuna mtu atatununua labda tukale wenyewe. Nikamuuliza, unataka kununua kwa lazima na kwa bei unayoitaka? Akajibu akasema yeye ndio don kijijini pale tulichukuana upepo, ukizingatia tabu anazopata mkulima halafu jitu levi tu linakuja na kuanza kutoa bei anazotaka na kwa lugha ya kebehi, aliinua mkono kwa lengo la kunipiga kibao nilimpiga Ngumi nyingi mfululizo.
Imebidi ahairishe zoezi la kukebehi na kulangua mazao. Wamesema atakuja tena Jumamosi ijayo nimemwambia mama tuelekee mjini kwani anaweza kuwa amejihami 😁 kilio cha wakulima, madalali wanatunyonya, hawalipi kodi ni wabaya.