Kilio cha Wakulima wa miwa Kilombero

Kilio cha Wakulima wa miwa Kilombero

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Sera ya nchi yetu kwa wakulima ni KUWAWEZESHA ili wainuke kiuchumi.

Wakulima wa Kilombero wamelima miwa yao, wamevuna miwa yao na hwana pa kuuzia. Viwanda vya sukari vimejaza sukari matani na matani hawana pa kuuzia kisa sukari iliyoingizwa bila KODI imetapakaa mitaani.

Sukari imeagizwa bil;a kodi huku tukiuziwa Tshs. 3,000 kwa kilo ili hali nchi ya jirani ya Zambia sukari walioagiza na kulipia kodi wanauza T.shs.2,700. Hii sukari ilipaswa tuuziwe T.shs.1,500 kwa kilo. Sasa nije kwenye mada. Kwa nini wakulima wa miwa wanateswa hivyo kwenye nchi yao?. Wamelima na wamevuna hawana mahala pa kuuzia. Serikali yetu inawatumikia akina nani?.

Ni aibu sana kuona wakulima wa miwa wakiteseka katika nchi yao huku tukiwakumbatia watu wachache hata wale ambao walikuwa na maduka ya stationery na kurusiwa kuagiza sukari.

Hii ni aibu kubwa. Jamani tumuogope Mungu.
 
Mm mtaani kwangu kilo kwa sasa ni 2600.





KAZI ni kipimo cha UTU
 
samahani koryo1952 hayo matani yaliyoko viwandani yalikuwa wapi wakati sukari imefika bei ya 10,000/= huku mtaani?
 
Back
Top Bottom