Kilio cha wananchi ambao wamelima miwa yao na hawana pa kuuzia

Kilio cha wananchi ambao wamelima miwa yao na hawana pa kuuzia

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Kuna kilio cha wananchi ambao wamelima miwa yao na wameshindwa pa kuuza kwa sababu viwanda navyo vina sukari na wameshindwa wamuuzie nani.

Serikali tumeiweka sisi wananchi madarakani ili ituongoze na kutuletea maendeleo. Sasa nini kauli ya Serikali kuhusu Wakulima ambao wana miwa yao na wameshindwa pa kuuzia?
 
Serikali iendelee kuaagiza sukari nje ili kukomesha cartel kwenye sukari
 
Umeandika usiyo kuwa na uhakika nayo, viwanda vinanunua miwa kwa wingi mpaka wakulima wanaishiwa, na demand ya sukari mtaani mi kubwa sana
 
Kuna kilio cha wananchi ambao wamelima miwa yao na wameshindwa pa kuuza kwa sababu viwanda navyo vina sukari na wameshindwa wamuuzie nani. Serikali tumeiweka sisi wananchi madarakani ili ituongoze na kutuletea maendeleo. Sasa nini kauli ya Serikali kuhusu Wakulima ambao wana miwa yao na wameshindwa pa kuuzia?
Funguka details zaidi Mnorth korea ili tupate pa kuanzia. Mashamba ya wapi?

Makisio ya ukubwa wa mashamba yaliyo achwa(details utazipata kwenye saccos zao)

Kiwanda lengwa kilichoshindwa chukua miwa(kwa kigezo wanayo sukari na kina L.Mpina wapo mahakamani)

Nashangaa kwanini miezi hii miwa inashindwa chukuliwa?(othwerwise una refer miezi tofauti na sasa)

NB: Mimi ni mkulima,na sasa ndo tupo peak katika uvunaji na uzalishaji

Funguka tupate pa kuanzia,mana kuna Bodi ya Sukari e.t.c
 
WAHINDI wa ndanindani nliwahi ona Wana tengeneza sukari wao wenyewe kwa nyenzo za hali duni ila Sukari inatokea kama hii tunayotumia.

Kama vipi wakulima waingie field kuwekeza kwenye viwanda hvyo.

Ama serikali iwakopeshe au kuwafadhili machine hata kama sio za kisasa zaidi ilimradi ziunde sukari, na IKIBIDI vifungashio ili watengeneze BRAND yao mwsho wa siku wajikwamue kiuchumi.
 
Back
Top Bottom