MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Mh Makamu wa Rais pole sana na majukumu.Mimi ni mwananchi w Kijiji cha mpugizi, kata ya Mwaru, Wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida.Kwanza tunakushukuru sana mama yetu kwa ulipoamua kuja ziarani mkoa wa Singida mwaka jana.
Wewe binafsi ulitiahidi wananchi wa Kijiji cha Mpugizi kua utatusaidia mabati 200 kwa ajili ya kuezeka Zahanati yetu ambayo imechukua miaka 4 bila kukamilika hadi sasa.
Mh Makamu wa Rais, cha ajabu tangu umemkabidhi mh Mbunge wetu ELIBARIKI KINGU pesa za kununulia mabati hayo 200 tumeishia kuziona kwenye video tu ukimkabidhi. Ila mpaka leo ninapilalamika hapa yafika mwezi mzima hizo pesa za kununulia mabati hazijatufikia wala mabati yenyewe hatuyaoni.
Mama yangu mpaka sasa tunajiuliza tumekosea nini wananchi wa Mpugizi?
Kama pesa alipewa mkononi kuna utaratibu gani wa kuchukua muda mrefu kununua mabati?
Umbali tulipo huku polini mpaka kufika kituo cha afya cha Sepuka ni kilomita 40, kinamama zetu wanapata shida sana wakati wa kujifunfungua na wewe ulisikia kilio hicho mama.
Tuliona msaada wako umeokoa kinamama wetu wanaopata shida kwa kuwapunfuzia safari ndefu hadi kituo cha afya cha Sepuka tulifurahi sana kutokana na upendo na uadilifu wako mama.
Na kama Mbunge wetu alifanyia pesa hizo kazi nyingine basi tungejulishwa Mheshimiwa ili tuanze kuchangishana tumalize shida hii wanayopata mama zetu.
Tunakupenda sana mama yetu SAMIA SULUHU. Tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais wetu mpendwa sana Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, tunampenda sana na usemi wake wa HAPA KAZI TU.
(MIMI MWANAKIJIJI MZALENDO WA MPUGIZI)
NITASEMA KWELI DAIMA,UONGO KWANGU MWIKO.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.