Kilio chetu kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Nishati

Kilio chetu kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Nishati

Nsema

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
275
Reaction score
479
Sisi ni Wataalamu 183 tulifanya kazi ya Uthamini katika uhamishaji wa wananchi kwenye Mradi wa GN 754 Mbarali Mbeya ambao ulikuwa unahusisha Wananchi kuhamishwa Ili kupisha hifadhi ya Ruaha na Bonde evu la Ihefu.

Waheshimiwa Mawaziri wa Wizara ya ardhi Jerry Silaa na Mhe. Waziri na Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko tunaleta Malalamiko yetu ya kutolipwa Posho zetu za muda mrefu. Kwenye Mradi huu mara ya mwisho kulipwa ilikuwa mwezi Julai 1, baada ya hapo tulifanya kazi bila Posho yoyote hadi Novemba 2 ambapo kazi ilisitishwa kutokana changamoto ya Posho, Mafuta na service za magari.

Kuanzia hapo hadi leo tumekuwa tukifuatilia malipo yetu kwenye ngazi mbalimbali bila mafanikio yoyote ambapo hadi Sasa miezi inakaribia 11 bila mafanikio.

Waheshimiwa Mawaziri na makatibu wakuu tunakuja kwenu kuleta kilio chetu. Kwasababu tulifanya kazi Mazingira magumu sana na tumehangaika sana kufuatilia malipo na hatuoni kama tutalipwa.

Tunaiomba Serikali ya Mama Sikivu itusaidie kupata malipo yetu kwasababu tuliingia madeni makubwa Ili kujikimu wakati wa kazi, na tulifanya kazi kwa moyo wetu wote.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom