Kilio kwa Meneja wa PSSSF Kagera

Kilio kwa Meneja wa PSSSF Kagera

Hae Mosu

Member
Joined
Dec 23, 2019
Posts
43
Reaction score
33
Habari ya kazi! Pole na majukumu.Mi nina dukuduku ambalo linasumbua watu wengi hasa watu wanaohitaji huduma hasa mafao Ya Uzazi.

Tatizo lililopo ofisini kwako hapo ni kwamba kumekuwa na usumbufu mkubwa kwa watumishi wa umma wanapokuwa wanafuatilia mafao yao hasa ya uzazi kuanzia kwenye upokeaji wa fomu tu wanakuwa wanazungushwa sana na watumishi wako hapo ofisini na hata wanapopokea huwa hawazifanyii kazi.

Mfano; mtumishi aliyejaliwa kujifungua mtoto mwaka jana,2020, mwezi wa tatu,mpaka sasa anakuwa hajapata mafao yake na akipiga simu kunakuwa na ushirikiano hafifu na hata akienda makao makuu ya Kanda, Mwanza kufuatilia kunakuwa ni kupoteza muda kwako taarifa zinakuwa hazijawasilishwa.

Hivyo, nakusihi ulifanyie kazi hasa anza na dawati linalopokea fomu ujue kuna shida gani hapo..

Nikutakie Majukumu mema.
 
Kwanini wanafanya manually na wakati technolojia imekua hivi jamani? Watengeneze system mtu aupload vitu vyake vyote kwenye system.
 
Mleta uzi nimekupenda sana, umetoa ushauri kwa njia ya kiungwana sana, kudos
 
Hawa haweleweki kama wanalipwa au la!bora waseme mafao ya uzazi yapo au hayapo kuondoa usumbufu wanaoupata wanufaika,mtu anakamilisha utaratibu wote lakini pesa halipwe kilikoni?
 
Hii ishu bado unasumbua na majibu hayaniridhishi kabisa Kwa maana yule anayepokea simu (dada) amekuwa na majibu ya ovyo ovyo
 
Back
Top Bottom