LGE2024 Kilombero: Wanachama wa CHADEMA wakamatwa wakidaiwa kufanya vurugu

LGE2024 Kilombero: Wanachama wa CHADEMA wakamatwa wakidaiwa kufanya vurugu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mshikemshike umeanza

Imeelezwa kuwa wanachama takribani 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kilombero, mkoani Morogoro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kuwafanyia vurugu wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kijiji na kata

Akizungumza na Jambo TV leo, Jumanne Novemba 19.2024, Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Kilombero Remig Frank Maginga amesema wanachama hao wanatoka katika kata mbili tofauti za Sanje na Mangula Mwaya ambapo wote 19 wanashikiliwa kwenye kituo cha Polisi Ifakara tangu Novemba 18.2024

Soma Pia:
Maginga aliyekuwa akizungumza na Jambo TV akiwa kwenye viunga vya kituo hicho cha Polisi sambamba na viongozi na wanachama wengine wa chama hicho walioweka kambi kituoni hapo ili kufuatilia mchakato wa dhamana, amesema kukamatwa kwa wanachama na wafuasi hao wa CHADEMA kumetokana na hatua za wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa kuwaengua wagombea wa chama hicho kinyume cha taratibu

Amesema idadi kubwa ya wagombea wa CHADEMA na vyama vya upinzani kwa ujumla wake wameenguliwa kwenye jimbo la Kilombero, hata hivyo pamoja na uwepo wa changamoto zote za uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 lakini miongoni mwa jambo lililowashangaza ni kuona wagombea wao wanaendelea kuenguliwa hata baada ya zoezi la uteuzi kukamilika

Inadaiwa kuwa wanachama hao hawakuridhishwa na majibu yaliyokuwa yametolewa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo, kwa kuwa walidai kuwa si wao waliowaengua badala yake zoezi hilo limefanywa na msimamizi msaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo (Mkurugenzi), na kwamba wao wamerejeshewa taarifa tu kwa ajili ya utekelezaji

Hata hivyo, licha ya uwepo wa sintofahamu hiyo lakini Maginga amekanusha madai ya wanachama na wafuasi hao wa CHADEMA kuwafanyia vurugu maafisa hao wa uchaguzi badala yake amesisitiza kuwa watuhumiwa hao 19 walikwenda kwenye ofisi hizo wakijuwa wazi kuwa ni ofisi za umma na kwamba ni imani yao kuwa viongozi wanaotumia ofisi hizo wanao wajibu wa msingi wa kujibu hoja na maswali wanayouliza na wananchi

Imeelezwa kuwa wanachama takribani 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kilombero, mkoani Morogoro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wakituhumiwa kuwafanyia vurugu wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kijiji na kata

Chanzo: Jambo TV
 
Back
Top Bottom