Kiluvya, Mbao FC, Mji Njombe, CDA zapanda Ligi Daraja la Kwanza

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Timu za Kiluvya United ya Pwani, Mbao FC ya jijini Mwanza, Mji Njombe kutoka mkoa mpya wa Njombe na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma zimepanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuongoza katika misimamo ya makundi yao ya Ligi Daraja la Pili (SDL).

Kwa kuzingatia Kanuni ya 5 (8) ya Ligi Daraja 9SDL Toleo la 2014, hatua ya pili Ligi Daraja la Pili kutafuta Bingwa na sasa timu hizo zitacheza kusaka Bingwa wa ligi Daraja la Pili.

Mji Njombe itacheza na timu ya Kiluvya United tarehe 14 Machi mwaka huu katika uwanja wa Amani Makambako, na mchezo wa marudiano kufanyika tarehe 18 Machi, 2015 katika uwanja wa Mabatini Mlandizi.

Nayo Mbao FC ya Mwanza watawakaribisha timu ya Mji Mkuu FC mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, na mechi ya marudiano itachezwa Machi 18, 2015 katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Fainali inatarajiwa kufanyika Machi 22 mwaka huu jijin Dar es salaam (uwanja wa mchezo utatangazwa baadae) kwa kuzikutanisha timu zilizopata pointi nyingi katika michezo hiyo miwili ya awali.

Chanzo; Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
 
Sidhani KAMA zimepanda! Ila zitacheza nusu fainali! Hatimaye kupata timu mbili zitakazocheza Fainali ambayo mshindi atakuwa bingwa wa Ligi Daraja la 2 ila zinapanda zote mbili....
Daraja la kwanza zimeshuka mbili so zinapanda 2. Ila Ni KAMA nlivyosikia Toka kwa wadau
 
Hapana Pukudu Mphamvu yuko sahihi.Hizi timu nne zimepanda daraja toka daraja la pili (SDL) kuingia daraja la kwanza (FDL).Hongera zao na tuwatakie kila la kheri katika mpambano wao kuingia ligi kuu VPL.
 
Last edited by a moderator:
Hapana Pukudu Mphamvu yuko sahihi.Hizi timu nne zimepanda daraja toka daraja la pili (SDL) kuingia daraja la kwanza (FDL).Hongera zao na tuwatakie kila la kheri katika mpambano wao kuingia ligi kuu VPL.

Nimefatilia nimeona mkuu Jamal Malinzi Mkuu Mphamvu Yuko SAHIHI kabisa tatizo ni hivi vilocal stations kimoja kilitangaza hivyo asubuhi! Mkuu Jamal Malinzi SASA mbona FDL zinashuka timu 2? Tu na je SDL zimeshuka ngapi? Na ni Timu ngapi zinapanda SDL.
?
 
Last edited by a moderator:

Msimu huu imebidi zishuke mbili FDL zipande nne kwa sababu ya transition ligi kuu VPL kutoka timu 14 kwenda 16.Mwaka huu ligi kuu VPL kati ya timu 14,zinashuka mbili tu na kupanda nne African sport,Maji maji,Mwadui na Toto Afrika.Lengo daraja la kwanza FDL zibaki timu 24 na daraja la pili SDL zibaki timu 24.Tunashukuru kwa utaratibu huu karibia kila mkoa Tanzania una angalau timu moja kwenye ligi.Hii inasaidia kuhakikisha nchini mwetu mpira hauchezwi mikoa michache bali unachezwa nchi nzima (we are spreading the game)
 
Last edited by a moderator:

Hongera sana! Kwa Hilo mkuu kiukweli uwepo wa FDL umechangamsha na kuleta msisimko wa aina yake! Ligi daraja la kwanza msimu huu Ilikuwa nzuri ila inahitaji MAREKEBISHO hasa kwenye maamuzi! SDL, ilikuwa Nzuri ila imepata hamasa zaidi kwenye mzunguko wa pili! Ni vizuri mkatafuta wadhamini! Jamal Malinzi Mara zote unasema wewe ni muumini wa soka la vijana! Je unaonaje mkipitisha kanuni ambazo zitalaImisha Timu zitakazoshiriki SDL Kuwa na IDADI fulani YA wachezaji wa under 17? Na hata FDL kulazimisha timu Kuwa na wachezaji vijana kadhaa?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…