Kilwa: Maafisa TRA hatiani kwa kukadiria kodi madumu 200 kati ya 500 ya Mafuta ya kupikia

Kilwa: Maafisa TRA hatiani kwa kukadiria kodi madumu 200 kati ya 500 ya Mafuta ya kupikia

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Mahakama ya Wilaya ya Kilwa imewatia hatiani Maafisa Forodha wa TRA Wilayani humo, Sultan Ali Nasor na Silver Maximillian kwa makosa ya Matumizi Mabaya ya madaraka na kutofanya Tathmini Sahihi ya Kodi iliyosababishia Mamlaka Hasara ya Tsh. Milioni 9.269.

Washtakiwa walifanya tathmini ya kodi kwa madumu ya mafuta ya kupikia 200 tu badala ya 500 ya lita 20 kila moja, yaliyoingizwa kutoka Zanzibar, mali ya Mfanyabiashara Athumani Ahmadi Simba.

Bw. Simba alishtakiwa kwa kushindwa kulipa kodi ambapo alikiri kosa na kulipa Tsh. 9,269,066.38/-, huku Washtakiwa wengine wakihukumiwa Miaka 3 jela kwa kosa la kwanza na la pili kila mmoja au kulipa faini ya Tsh. 250,000/= kila mmoja kwa kila kosa, na kifungo cha nje mwaka 1 kila mmoja kwa kosa la 3.

Chanzo: TAKUKURU
 
Dp world ndo suluhisho la ubadilifu wa aina yoyote technology ni muhimu bandalini mzigo hunajulikana hata kabla ya kupakuliwa serikali inapata kodi yake sahihi.
 
Aisee kifungo ni nje mwaka mmoja na faini laki mbili na nusu hzi sheria katunga nani?
 
Dp world ndo suluhisho la ubadilifu wa aina yoyote technology ni muhimu bandalini mzigo hunajulikana hata kabla ya kupakuliwa serikali inapata kodi yake sahihi.
Baada ya ujio wa DPW, Je, hiyo mifumo ya kodi itakuwa inasimamiwa na malaika kutoka mbinguni??Je, malaika ndio watakaohusika ktk ukadiriaji wa viwango vya kodi??
 
Back
Top Bottom