Kim & The Boys afariki dunia

Rest in Peace dear friend. Yetu safari ni moja na hakika itafika siku tutafika nyumbani na kukutana tena.
 
r.i.p jibaba!sura yako nilibahatika kuiona fridays nights live ya E.A. radio kipindi nasoma!
 
Niko kwenye makaburi ya Kisutu ambako ndiko anazikwa saa hii DJ Kim.

Watu ni wengi sana, watoto wa mujini, madjs, watangazaji, wanamuziki na maceb wetu wa bongo wamejitokeza kwa wingi.

DJ Kim aliishi mtaa wa Mkwepu tangu kuzaliwa mpaka kifo, hivyo mtaa huo ulifungwa kwa muda wakati mwili ulipotoka kwenda msikiti wa Jamuhuri.

Vijana wameamua kubeba jeneza kwa mikono tangu msikitini mpaka makaburini.

Ni mtu wangu wa karibu haswa kwa kuzingatia Mkwepu ni mtaani kwangu.

Mungu aiweke roha yake mahali pema peponi.
 


bluray..
Hapa kuna umuhimu
wa kuandika kitabu pia cha historia
ya entertainment tz,bongo flava
na mengineyo,
itakuwa msaada mkubwa
kwa wengi.
 
Mazishi yamemalizika, jamaa alikuwa mtu wa watu na watu wamejitoa kumsindikiza safari yake ya mwisho. Mazishini leo palikuwa mahali pa kukutana, watu wa zamani waliopotezana muda mrefu, wamekutanishwa na Kim kwa mara ya mwisho.

MaDJs wa zamani karibu wote ndani ya nyumba, watangazaji wa vipindi vya muziki wa zamani na wapya, wanamuziki wa kizazi kipya, madanser, wale vijana wote mission town walikuwepo bila kuwasahau ma Sheikh kadhaa waliiongoza maziko.

RIP DJ KIM!.
 
RIP bradha KIM.

??? kuna wagoloko humu eti wanauliza Kim ni nani? inaelekea kipindi kile walikuwa huko madongo kuinama wanawinda ndezi, hawajui hata kuvaa viatu halafu leo wanajifanya wajaaanja hapa JF..ny*k* zenu..
 
Ulale pema peponi Kamanda, Ulale Pema peponi kamanda, Imekuwa Hudhuni kwa Ndugu na Masera ......
 


- Mkuu Bluray, heshima sana hapo maana umesema mengi niliyotaka kusema kuhusu marehemu, ingawa nitasema kidogo anyways a longtime friend ninamkumbuka Kim toka akiwa dogo akiishi pale pembeni mwa Mbowe Hotel, baba yake alifanikiwa kuwashawishi Wahindi wakamuachia kasehemu hivi kati kati ya maghorofa yao kwa chini hivi next to Marmeids, ambapo zamani kabla ya kuingia kuruka nyoka RSVP Disco la Dj Kali Kali RIP, na DJ Jerry Kotto, ilikuwa lazima kula kipande cha kuku mguu wa kuku na chips, ndugu yangu Mkandara nafikiri anakumbuka sana enzi hizo akijulikana mjini kwa jina la Thriller!

- Enzi za Holiday Inn, na wakulu kama Katimba, Luis, Spearman, Jerry Kotto, Chris Phaby The Lover, Fitina, Pailonga, Wandiba RIP, Bob Rich, Ray Abdu, Justin Pamba, Choggy, Rich Mazula Ebbo Nighte Woo Jack, DJ Lucas, Bitozi Feruzi kabla hajaruka akili na kuanza kuokota makopo, Bitozi Saimon Makene, Mkulu Inno Galinoma, Hussein Macheni, Joe Kusaga duh longtime, hiki ndicho kipindi marehemu Kim, alianza kunyanyuka katika ulimwengu wa Disco, ninakumbuka mara kwa mara nikienda home kwao enzi hizo tunaita kwenda "kufyonza ngoma" yaani kurekodi miziki mipya ya Disco tena kwenye tape maaana enzi hizo CD ilikuwa ni ndoto!

- Namkumbuka kijana mdogo Kim, akianza kazi Benki ya NBC hapa kona ya sanamu akitokea kwenye maisha very humble, pia akianza mambo ya kupiga Disco, akishirkiana sana na Disco toto la YMCA la kina Nigger Jay na Borncity na hasa Franco na Gibbson na Mkulu wangu Shebby B, kabla Sudi na Super Deo hawajaingia na kuchukua pale. Na ninamkumbuka akiamua kuacha kupiga Disco na kujihusisha sana na promotion za Concerts za muziki wa kizazi kipya. Mara ya mwisho nilikutana naye akiwa na DJ mwingine wa zamani DJ John Bure, wakanitaka sana niwape tafu ya namna ya kununua vyombo vyao vya kisasa ili waweze kuanzisha studio ya muziki!

- Mungu akutangulie mbele Mamen Kim, wote tuko njiani na Mungu pia awape nguvu wazazi wake na hasa sister wake ambaye walikuwa karibu sana toka utoto, na pia salaam za rambi rambi kwa familia yake nzima, I mean this one really hurts! Mkuu Invisible, ashante sana kwa huu ujumbe ambao nilipewa jana usiku na Baharia Biron Kapange, aliyekua naye mpaka anaaga dunia, Mungu amlaze mahali pema peponi!

Respect.


Field Marshall Es!
 

Pole baharia wangu, thanks for the history, msiba wetu sote.
 
Mkuu wa kaya samahani ndio nani na alikuwa ana promote nini?? nimejaribu kua google vinakuja vitu tofauti kbs.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amina.
Kwa macheck bob wa enzi hizo alikuwa ni mtu mmoja maarufu sana.
Mungu ailaze roho yake peponi amin
 
- Amekuwa aki-promote muziki wa kizazi kipya kwa muda mrefu sana sasa ingawa hakufanikiwa sana kwenda juu, lakini aliweza kujipatia heshima katika huo ulimwengu na hasa kwa wale tunaojua alikotokea kimaisha, alitokea mbali sana na Mungu Amuweke Mahali Pema Peponi!

Respect.


FMEs!
 
RIP Kaka Kim n ze Boyz Abdulhakim Magomelo... Kama kuna mwenye picha yake ya enzi hizo tafadhali aweke hapa... Huyu jamaa anastahili kitabu... Kwani alikuwa Muasisi wa Muziki wa kizazi kipya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…