DA HUSTLA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2012
- 3,805
- 4,107
Inabidi tutengeneze documentary ya muziki wetu.- Mkuu Bluray, heshima sana hapo maana umesema mengi niliyotaka kusema kuhusu marehemu, ingawa nitasema kidogo anyways a longtime friend ninamkumbuka Kim toka akiwa dogo akiishi pale pembeni mwa Mbowe Hotel, baba yake alifanikiwa kuwashawishi Wahindi wakamuachia kasehemu hivi kati kati ya maghorofa yao kwa chini hivi next to Marmeids, ambapo zamani kabla ya kuingia kuruka nyoka RSVP Disco la Dj Kali Kali RIP, na DJ Jerry Kotto, ilikuwa lazima kula kipande cha kuku mguu wa kuku na chips, ndugu yangu Mkandara nafikiri anakumbuka sana enzi hizo akijulikana mjini kwa jina la Thriller!
- Enzi za Holiday Inn, na wakulu kama Katimba, Luis, Spearman, Jerry Kotto, Chris Phaby The Lover, Fitina, Pailonga, Wandiba RIP, Bob Rich, Ray Abdu, Justin Pamba, Choggy, Rich Mazula Ebbo Nighte Woo Jack, DJ Lucas, Bitozi Feruzi kabla hajaruka akili na kuanza kuokota makopo, Bitozi Saimon Makene, Mkulu Inno Galinoma, Hussein Macheni, Joe Kusaga duh longtime, hiki ndicho kipindi marehemu Kim, alianza kunyanyuka katika ulimwengu wa Disco, ninakumbuka mara kwa mara nikienda home kwao enzi hizo tunaita kwenda "kufyonza ngoma" yaani kurekodi miziki mipya ya Disco tena kwenye tape maaana enzi hizo CD ilikuwa ni ndoto!
- Namkumbuka kijana mdogo Kim, akianza kazi Benki ya NBC hapa kona ya sanamu akitokea kwenye maisha very humble, pia akianza mambo ya kupiga Disco, akishirkiana sana na Disco toto la YMCA la kina Nigger Jay na Borncity na hasa Franco na Gibbson na Mkulu wangu Shebby B, kabla Sudi na Super Deo hawajaingia na kuchukua pale. Na ninamkumbuka akiamua kuacha kupiga Disco na kujihusisha sana na promotion za Concerts za muziki wa kizazi kipya. Mara ya mwisho nilikutana naye akiwa na DJ mwingine wa zamani DJ John Bure, wakanitaka sana niwape tafu ya namna ya kununua vyombo vyao vya kisasa ili waweze kuanzisha studio ya muziki!
- Mungu akutangulie mbele Mamen Kim, wote tuko njiani na Mungu pia awape nguvu wazazi wake na hasa sister wake ambaye walikuwa karibu sana toka utoto, na pia salaam za rambi rambi kwa familia yake nzima, I mean this one really hurts! Mkuu Invisible, ashante sana kwa huu ujumbe ambao nilipewa jana usiku na Baharia Biron Kapange, aliyekua naye mpaka anaaga dunia, Mungu amlaze mahali pema peponi!
Respect.
Field Marshall Es!
Pia ni muhimu kuanza kuweka kumbukumbu katika nyanja mbali mbali hapa Tanzania.
Sent using Jamii Forums mobile app