SI KWELI Kimara, Stop Over: Basi na lori yagongana uso kwa uso na kuungua moto, Oktoba 31, 2022

SI KWELI Kimara, Stop Over: Basi na lori yagongana uso kwa uso na kuungua moto, Oktoba 31, 2022

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Ajali imetokea muda huu katikati ya Kimara Stop over na Suka eneo la Garage. Ni kwamba bus linatokea Dodoma na lory la cement vimegongana uso kwa uso na magari yote yameungua moto na vichwa vya watu vinapasuka kwa mlio kama bomu!

Tuombe Mungu atujalie mwisho mwema

 
Tunachokijua
Ajali hii ili inadaiwa kutokea Kimara Stop Over Oktoba 30, 2016, ilihusisha magari mawili Basi la abiria kutoka Dodoma kampuni ya Safari Njema lenye namba za usajili T990 AQF na roli lililokuwa limebeba saruji lenye namba za usajili T 534 BYJ na kusababisha kifo cha mtu 1 na majeruhi 16.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Muliro Jumanne amesema;

“Taarifa hizo siyo za kweli, zipuuzwe na tarehe ya leo 31. 10. 2022, hakuna ajali Iliyotokea eneo hilo ya namna hiyo”.

JamiiForums imebaini kuwa taarifa hizo si za kweli, zinaweza kupuuzwa.
Back
Top Bottom