Kimbunga Ida: Idadi ya vifo yapanda hadi watu 41 katika majimbo manne ya kaskazini mashariki mwa Marekani

Kimbunga Ida: Idadi ya vifo yapanda hadi watu 41 katika majimbo manne ya kaskazini mashariki mwa Marekani

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Baadhi ya wakazi wamekwama katika maeneo ya chini ya nyumba zao yaliyofurika maji pamoja na ndani ya magari yao

Baadhi ya wakazi wamekwama katika maeneo ya chini ya nyumba zao yaliyofurika maji pamoja na ndani ya magari yao
Rais wa Marekani Joe Biden anasema "uwekezaji wa kihistoria " unahitajika kukabiliana na mzozo wa hali ya hewa, huku maeneo ya kaskazini-magharibi mwa nchi yakikabiliwa na mafuriko pamoja na vimbunga ambavyo vimewauwa watu wapatao 41.

Marekani inakabiliwa na uharibifu unaotokana na hali ya hewa kote nchini na kushughulikia uharibifu huo ni "suala la maisha na kifo ", alisema rais.

Majiji ya New York City na New Jersey yalishuhudia mvua kubwa ambayo haikutarajiwa.
Baadhi ya wakazi wamekwama katika maeneo ya chini ya nyumba zao yaliofurika maji pamoja na ndani ya magari yao.

Majimbo manne yamepoteza maisha ya watu:​

  • Gavana wa New Jersey Phil Murphy ameema kuwa takriban watu 23 wamefariki katika jimbo lake-wengi wao wakiwa ndani ya magari yao wakati maji yalipopanda.
  • Takriban watu 14 walipoteza maisha yao katika jimbo la New York City, akiwemo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili. Kumi na mmoja kati yao walizama wakati walipokuwa ndani ya maeneo ya chini ya nyumba ya kuegesha magari yaliyokuwa yamefurika, maafisa walisema.
  • Watu watatu walikufa karibu na Philadelphia, Pennsylvania, huku mtu mmoja akifariki katika mji wa Connecticut
Athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha vimbunga bado haiko wazi, lakini tunafahamu kwamba kuongezeka kwa viwango vya joto kwenye uso wa bahari vinachemsha hali ya hewa juu na kusababisha nguvu zaidi ya kusababisha vimbunga. Matokeo yake, yanaweza kuwa mabaya zaidi na kusababisha mvua kubwa kupita kiasi.

Residents of the Oakwood Plaza apartments react in the aftermath of flooding that was caused by the remnants of Tropical Storm Ida, which brought drenching rain, flash floods and tornadoes to parts of the northeast, in Elizabeth, New Jersey, U.S., September 2, 2021.


Wakazi wa Elizabeth, New Jersey, wakionekana kutafakari baada ya kuepuka dhoruba. Dunia tayari imekuwa joto kwa kiwango cha takriban nyuzijoto 1.2 tangu ilipoanza enzi ya viwanda na viwango hivyo vitaendelea kupanda iwapo serikali kote duniani hazitachukua hatua za kukata utoaji wa gesi chafu.

'Kupungua kwa viwango vya maji katika Niagara Falls '
Meya wa New York City Bill de Blasio aliwakosoa wataalam wa hali ya hewa, akisema kuwa utabiri wao ulikuwa "ukikejeliwa kwa kipindi cha dakika ". Amesema amekuwa akitahadharishwa na wataalam juu ya mvua ya kati ya inchi tatu na sita (kati ya sentimita 7.5 na 15 ) katika kipindi cha siku. Hatahivyo rekodi ya inchi 3.15 ilianguka katika Central Park katika kipindi cha saa moja tu .

" Tunahitaji kuanza kuwasiliana na watu kwamba mambo yatakuwa mabaya zaidi katika kila hali ," anasema. Gavana wa New York Kathy Hochul alisema: "tunahitaji kujua kwamba kati ya saa 8:50 na saa 9:50 jioni. usiku wa jana, kwamba anga zitafunguka na kuleta mvua ya viwango vya Niagara kwenye mitaa ya New York."

Damage to Wellacrest Farm in New Jersey

Kiwanda kikubwa zaidi cha maziwa cha New Jersey kiliharibiwa vibaya kutokana na kimbunga na mafuriko Wakazi wamekuwa wakitathmini hasara za mali.

Mwanaume mmoja wa eneo la Flushing, New York, alisema kuwa makazi yake yameharibiwa na mafuriko "lakini nilichokiona usiku uliopita sio cha kawaida ". "Sijawahi kuona maji yakiingia kutoka kila upande ," Tedla Asfaw, mwenye umri wa miaka 60, aliiambia BBC. " Kuna uharibifu mkubwa hapa . Ni pigo kubwa kwetu ." Katika New Jersey, kimbunga kiliangusha chini kiwanda kikubwa zaidi cha maziwa, na kung'oa paa za majengo.

Ng'ombe wengi walikwama chini ya nyumba zilizoanguka na baadhi walikufa, wamiliki wa shamba la Wellacrest waliandika kwenye ukurasa wa Facebook "Pamoja na hasara mbaya ya kupoteza nyumba katika eneo letu-sisi kama jamii, tumeathiriwa pakubwa na uharibifu wa shamba letu ."

Feri nyingi za New York City bado zimefungwa baada ya picha za mitandao ya kijamii kuonesha maji yakiingia kwenye kituo cha treni cha chini ya ardhi.

Picha nyingine ilionesha magari yakielea ndani ya maji ya barabara zilizofurika maji, huku vilio vya kuomba msaada "saidia" vikisika ndani ya magari hayo.
 
Back
Top Bottom