SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Na Mwandishi Wetu
Vunjo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ameishukuru klabu ya Rotary ya Mwika kwa kujenga kivuko cha Koongo-Saghai kinachounganisha kata za Mwika Kusini na Mwika Kaskazini.
Ujenzi wa kivuko hicho umegharimu shilingi milioni 10.5 fedha zilizotolewa na klabu hiyo ya Rotary ambayo Mhe Mbunge ni mwanachama.
"Vunjo tunayoitamani itajengwa na kila mmoja wetu aliyopo ndani na nje ya Vunjo. Hivyo nawakaribisha wanavunjo wote wenye nia na dhamira njema ya kutaka kuweka alama katika maendeleo ya jimbo letu katika sekta za afya, elimu, barabara, michezo nk waje tushirikiane kuijenga Vunjo yetu. Hii ndiyo Vunjo Mpya!" Alisema Dkt Kimei
#PamojaTunaweza
Picha ya 1: Kilichokuwa kivuko cha Koongo-Saghai
Picha 2: Kinavyoonekana sasa kivuko hicho cha Koongo-Saghai baada ya ujenzi kukamilika.
KIMEI MITANO TENA