Pre GE2025 Kimei amshukuru Rais Samia kwa mabilioni ya fedha miradi ya maendeleo Vunjo, amuomba Jenista kubeba yaliyosalia

Pre GE2025 Kimei amshukuru Rais Samia kwa mabilioni ya fedha miradi ya maendeleo Vunjo, amuomba Jenista kubeba yaliyosalia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
~ Atamba azi kubwa ya maendeleo iliyofanyika ni turufu ya ushindi kwa CCM na Rais Samia 2025

~ Aomba ukarabati kituo cha afya Mwika Msae
na upanuzi kituo cha afya Himo

~ Aomba pia barabara kwa kiwango cha lami Pofo - Mandaka - Kilema na nyingine zikamilishwe

~ Kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani iwafikie wananchi wa kata za Mwika Kaskazini na Mwika Kusini kwa kukamilisha miradi ya maji kwenye kata hizo

Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Mhe. Dkt Charles Stephen Kimei amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo kila sekta katika Jimbo hilo, Mkoani Kilimanjaro.

Ametoa shukrani hizo tarehe 06 Oktoba, 2024 wakati wa ziara ya mlezi wa maendeleo mkoa wa Kilimanjaro na Waziri wa Afya Mhe Jenista Joackim Mhagama Mb) kijiji cha Yamu Makaa kata ya Kirua Vunjo Kusini wakati wa ufunguzi wa shule mpya ya sekondari Pumuani.
IMG-20241007-WA0020.jpg
Akielezea miradi iliyotekelezwa katika jimbo lake la Vunjo amesema katika sekta ya elimu, Vunjo imekua kati ya majimbo 100 nchini ambayo Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kujengwa shule za sekondari za mafunzo ya amali ambapo tayari ujenzi wake umeanza katika kijiji cha Koresa na utagharimu shilingi milioni 584.

Amesema shule nyingine mpya ya sekondari inajengwa katika kijiji cha Mabungo kwa shilingi milioni 584 huku sekondari mbili zikiwa zilishakamilika na wanafunzi wanasoma tayari ambazo ni Njiapanda na Pumuani ambazo ujenzi wake umegharimu shilingi bilioni 1.084 Vile vile wamepewa fedha shilingi milioni 984 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kidato cha 5&6 katika mbili ya sekondari za Himo (kata ya Makuyuni) na Mangoto (kata ya Kahe)
IMG-20241007-WA0016.jpg
Aidha, Mhe. Kimei amesema, katika miaka mitatu ya Rais, Dkt. Samia amewezesha Jimbo hilo shilingi bilioni 44 za miradi ya maendeleo ambapo ni ujenzi wa vtuo vya afya 4, zahanati mpya 12, Ultrasound, Digital X-Ray, Mashine ya matibabu ya meno pamoja na shilingi zaidi ya bilioni 8 kwa ajili ya miradi ya maji safi na salama katika Jimbo hilo. Kadhalika, Dkt Kimei amesema bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka shilingi milioni 475 mpaka kufikia bilioni 2 kwa sasa,na ujenzi wa daraja la Marangu Mtoni.
IMG-20241007-WA0015.jpg
Dkt Kimei amesema pamoja na kazi kubwa na nzuri ya maendeleo ambayo Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia serikali ya awamu ya sita anayoiongoza ameifanya katika Jimbo hilo kwa niaba ya wananchi wa Jimbo hilo amemuomba Mhe Jenista asaidie kuwasilisha mambo machache yafanyiwe kazi ambayo ni ukarabati wa kituo cha Afya Mwika Msae, Upanuzi wa kituo cha Afya Himo, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ambazo ni Pofo - Mandaka - Kilema, Chekereni - Kahe - TPC, Uchira - Kisomachi - Kolarie, Nduoni - Marangu na ukamilishaji wa mradi wa maji kata za Mwika Kaskazini na Mwika Kusini.
 
Hivi hii ni nchi inayoendeshwa kwa Misingi ya Kupanga Bajeti na kupeleka Pesa kwenye Mahitaji au Monarchy mfalme anafanya anachotaka kufanya kwa sababu ya fadhila au ni kiasi gani mtu anabembeleza na kufanya uchawa...

Hayo juu yangekuwa hayana tatizo lolote iwapo baadhi ya hizo pesa zinazosambazwa (sio zote nyingine zinalambwa) zingekuwa ni pesa zao na sio za walipa kodi na hio miradi ingekuwa ni Hisani na sio wajibu....
 
Back
Top Bottom