Kimei aweka rekodi nyingine kwa kufanikisha mradi wa ukamilishaji daraja la Sembeti - Samanga

Kimei aweka rekodi nyingine kwa kufanikisha mradi wa ukamilishaji daraja la Sembeti - Samanga

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
Kutoka,
Sembeti, Marangu.

Kazi ya Ukamilishaji wa ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji vya Samanga na Sembeti uliosimama kwa takribani miaka 20 inaendelea baada ya kupata fedha toka mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kiasi cha shilingi milioni 103.5 Kuendelea na kukamilika kwa Mradi huu ni rekodi nyingine ya mafanikio ya Mbunge wa sasa Mhe Dkt Charles Stephen Kimei ambaye amejitanabaisha kuwa Mbunge wa vitendo zaidi kuliko maneno.

Pongezi za dhati kwa uongozi wa vijiji tajwa, diwani wa kata ya Marangu Mashariki Mhe Jonas Mawala na Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei kwa kuhakikisha fedha zinapatikana na Kazi hiyo inaendelea.

Shukrani za kipekee kwa serikali ya CCM Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipa Jimbo la Vunjo fedha nyingi za miradi ya Maendeleo.

Hakika

#VunjoTumechagua
#CCMTeamMaendeleo
#MaendeleoKwaVitendo
#KaziIendelee

IMG-20240618-WA0076.jpg
IMG-20240618-WA0075.jpg
IMG-20240618-WA0074.jpg
IMG-20240618-WA0073.jpg
IMG-20240618-WA0072.jpg
IMG-20240618-WA0071.jpg
 
Honestly vunjo watafute mtu mwingine si huyu mzee. Yes ana pesa ana ushawishi mkubwa but siasa is not his place
 
Habari za JUMIKATA utazijua tu. Halafu huwa hazina wachangiaji.
 
SEREKALI IINGIZE KAKODI KADOGO KWENYE PETROL NA DIESEL, KWA AJILI YA BARABARA NA MADARAJA YA VIJIJINI, BADALA YA KUSUBIRI KUOMBA PESA KWA TABU KWELI SEREKALI, KAKODI HAKO KAWE KANABAKIA NDANI YA MKOA HUSIKA,KASAIDIANE NA CHOCHOTE KITAKACHOPATIKANA SEREKALINI.
 
Kodi zote hizo kwenye mafuta bado unataka kuwe na kodi nyengine iongezwe? Hebu acha utani
 
Ofisi ya mbunge, imeshindwa kiutendaji kabisa, inamwangusha mbunge, iweke kazi zote za mbunge za miaka mitano (5) nakwenda kujiandikisha kama mpiga kura, kisambo.
 
Back
Top Bottom