Uchaguzi 2020 Kimenuka Njombe. Wajumbe wavamia Ofisi za CCM, "Tutashusha bendera za CCM”

Uchaguzi 2020 Kimenuka Njombe. Wajumbe wavamia Ofisi za CCM, "Tutashusha bendera za CCM”

Libya

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2016
Posts
790
Reaction score
1,968
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,baadhi ya viongozi na wajumbe wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Mji Mwema mjini Njombe,wamesema wako tayari kwenda kushusha bendera za Chama chao na kuto shiriki shughuli za kampeni katika kata hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi kutokana na kutoheshimiwa maamuzi yao.

Wajumbe wa Kata hiyo wamelazimika kuweka wazi uamuzi wao kutokana na juhudi zao za kuzunguka kwa zaidi ya siku mbili mfululizo ngazi zote zinazohusu uchaguzi ngazi ya kata bila mafanikio.Wamesema wanashangazwa mgombea wao Nestory Mahenge aliyeshinda kura za maoni kushindwa kuteuliwa badala yake kuletewa mgombea aliyeshika nafasi ya pili Ndugu,Abuu Mtamike aliyehamia katika Chama hicho akitokea Chama kikuu cha Upinzani CHADEMA.

Hata hivyo wanasema kutokana na kuonyesha juhudi za malalamiko yao wamefanikiwa kukabidhiwa barua kutoka kwenye Chama chao lakini bado mpaka sasa wanasumbuliwa na kushindwa kupewa barua kutoka kwa msimamizi msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata hiyo

 
Libya,
Huyo babu yangu wa miaka 71 ameongea kwa uchungu mkubwa. Waje huku CHADEMA.

Wakati walipotulazimisha wenyeviti wa Mitaa na Vijiji ktk uchaguzi batili wa November 2019 kuwa viongozi wa maeneo yetu walishangilia, sasa wamkubali huyo walioletewa kwa lazima.
 

Wajumbe wamekatwa na wajumbe.
Yaani sasa hivi ndio naelewa maana halisi ya ule msemo kwamba "mjumbe hauawi", kumbe maana yake ni kwamba wajumbe hawauawi kwa sababu wao wenyewe ndio wauaji.
Mi nadhani sasa ni wakati wakuondoa hili suala la kura za maoni, maana naona nikuvunjiana heshima na kupotezeana muda tu. Hai ingii akilini uwakusanye watu wazima wafanye maamuzi halafu maamuzi yao yasiheshimike.

Kauli ya m/kiti kwamba wajumbe wapige kura na zihesabiwe kwa uwazi ilikuwa na maana gani?

Nimesikia kuna mgombea ambae amekatwa pamoja nakuwa mshindi kwa kura 152 nakupitishwa aliyeshika nafasi ya saba kwa kupata kura 12.
 
Wajumbe wamekatwa na wajumbe.

Kauli ya m/kiti kwamba wajumbe wapige kura na zihesabiwe kwa uwazi ilikuwa na maana gani?

Nimesikia kuna mgombea ambae amekatwa pamoja nakuwa mshindi kwa kura 152 nakupitishwa aliyeshika nafasi ya saba kwa kupata kura 12.
Shy town 😅🤣😂
 
Back
Top Bottom