Wajumbe pamoja umaarufu wote walioupata ktk ngazi ya wilaya na kata, kumbe zote zilikuwa ni kelele za chura tu, ona sasa tembo keshafanya vitu vyake, maji kayanywa na kuacha tope jingi mtoni.
Oil chafu kutoka CDM ni lulu kwa chama tawala, na ndiyo yenye thamani na hata kuaminika ktk awamu hii. Chaguo la wajumbe wa ngazi za chini si lolote wala chochote kile kwa wakubwa zenu. Tulieni tuli kama maji mtungini, ili mjipange upya na kuanza kusifu na kuabudu kwa mara nyingine tena.