Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kikao cha Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu kilichofanyika Machi 5, 2025, kiliibua hali ya sintofahamu baada ya kutokea mzozo mkali kati ya Katibu wa CCM wilayani humo, Ndg. Naborth Manyonyi, na Katibu wa Itikadi, Siasa, na Uenezi wa wilaya hiyo, Ndg. Julius Maunde.
Tukio hilo lilisababisha vurugu zilizowalazimu viongozi hao kutoka nje ya ukumbi na kuendelea na ugomvi wao mbele ya wananchi.
Kwa mujibu wa mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, ametueleza kuwa mvutano huo ulianza ndani ya kikao baada ya Mwenezi wa CCM, Ndg. Julius Maunde, kumtuhumu Katibu wa Wilaya, Ndg. Naborth Manyonyi, kwa kuruhusu baadhi ya watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani kufanya kampeni za mapema kinyume na Katiba ya CCM.
Maunde alidai kuwa Katibu na baadhi ya viongozi wengine wamekuwa wakishirikiana na watia nia hao katika kutoa hongo kwa wajumbe, jambo linalokiuka misingi ya chama.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Baada ya shutuma hizo, Katibu wa CCM Wilaya alikanusha vikali, hali iliyosababisha mvutano mkali kati yao. Malumbano hayo yaliendelea hata baada ya kikao kufungwa, ambapo wawili hao walisukumana na kutishiana kupigana hadi nje ya ukumbi, mbele ya wananchi waliokuwa wakishuhudia tukio hilo.
Katika mahojiano ya simu na Jambo TV, Ndg. Julius Maunde alikiri kutokea kwa mvutano huo lakini alidai kuwa ulikuwa ni "kutofautiana kwa kauli."
Alipoulizwa kuhusu tuhuma alizotoa dhidi ya Katibu wake, alisisitiza kuwa Katibu Manyonyi ndiye anapaswa kutoa ufafanuzi zaidi.
"Unakuta tu mtu anaanza kushikana na wewe bila sababu, sasa unakosa hata cha kueleza zaidi. Nashauri mmhoji yeye, ndiye atakayetoa majibu sahihi," amesema Maunde.
Kuhusu uwezekano wa kupatanishwa, Mwenezi huyo amesema kwa sasa kila mmoja ataendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa chama, na kwamba suala hilo linaweza kujadiliwa baadaye katika vikao rasmi.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Wilaya, Ndg. Naborth Manyonyi, alipopigiwa simu na mwandishi wetu, alikiri kutokea kwa ugomvi huo, akidai kuwa chanzo chake ni mgogoro wa muda mrefu kati yake na Ndg. Maunde.
Chanzo: Jambo TV