Kimeumana! Mbappe hataki kusaini mkataba mpya PSG, Real Madrid wadaiwa kumshawishi

Kimeumana! Mbappe hataki kusaini mkataba mpya PSG, Real Madrid wadaiwa kumshawishi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Hakuna maelewano mazuri kati ya Viongozi wa Real Madrid na PSG mpaka sasa, PSG wakiwashutumu Madrid kumlaghai kijana na ndio sababu amegoma kusaini mpaka sasa.

Taarifa za leo asubuhi ni kuwa, msimamo wa Mbappe upo palepale licha ya Messi kusainiwa ila yeye anahitaji kuondoka kujiunga na Real Madrid.

Mbappe yupo wazi kuwa hawezi kusaini mkataba mpya, kama hauzwi basi ataondoka bure mwishoni mwa msimu.

Mpaka sasa Madrid hawana presha yoyote, PSG waamue wao wachukue pesa au Madrid wachukue mtu wao bure.
 
PSG baada ya kumpata Messi wanajiona wao ndio klabu bora sasa 😂
 
Role model wa ronaldo uyo unategemea ataendelea kubaki psg mbele ya king!!😀
 
Taarifa kutoka kwa wachambuzi wetu zinadai Mbape ni mchezaji wa Monaco yupo PSG kwa mkopo, Wenye maamuzi ni Monaco na mchezaji Kama ata amua kumaliza muda wa mkopo au kurudi Monaco.
Bongo kunawachambuzi basi, lugha yenyewe tu kwao ngumu maana wangeweza hata ku google kupata ukweli
 
Kwani uongo, mwenyewe apo ukimpata kwenye timu lako mbona tutaisoma
Ngoja tusubiri wakati utasema...

Maana ni Messi huyo huyo alipokuwa akichezea chama langu Barca alikuwa mwiba...

Lakini Messi huyo huyo alipokuwa akichezea chama langu Argentina alikuwa kama mchezaji mwingine yoyote tu...

Hivyo naamini kuna mfumo uliokuwa unamsaidia Messi awe mwiba, na PSG itawalazimu wautengeneze mfumo huo
 
Bosi wa PSG amesema Mbappe alitaka timu iwe competitive now wameshamsajili Messi anadai Mbappe hana sababu nyingine yoyote ya kuondoka PSG.

Jamaa anasema PSG kwa sasa ndio the most competitive team in the world.

Mashabiki wa PSG wamevamia duka la klabu yao kununua jezi za Messi kwa fujo, jezi moja inauzwa sawa na shilingi laki mbili na kitu za kibongo.
 
Hakuna maelewano mazuri kati ya Viongozi wa Real Madrid na PSG mpaka sasa, PSG wakiwashutumu Madrid kumlaghai kijana na ndio sababu amegoma kusaini mpaka sasa.

Taarifa za leo asubuhi ni kuwa, msimamo wa Mbappe upo palepale licha ya Messi kusainiwa ila yeye anahitaji kuondoka kujiunga na Real Madrid.

Mbappe yupo wazi kuwa hawezi kusaini mkataba mpya, kama hauzwi basi ataondoka bure mwishoni mwa msimu.

Mpaka sasa Madrid hawana presha yoyote, PSG waamue wao wachukue pesa au Madrid wachukue mtu wao bure.
Hahah kweli kimeumana ila mbape hata akiondoka psg mwaka huu watabeba kombe lao la ligue 1 ila sio UEFA championsleague hiyo wawaachie chelsea tena [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom